Hawa ndio Wafadhili wakuu wa CHADEMA ambao Mbowe hataki kuwataja hadharani

Wadau amani iwe kwenu.

Mtakumbuka hivi karibuni, Mwenyekiti wa CHADEMA, FREEMAN MBOWE amenukuliwa akisema kuwa chama hicho kina wafadhili watano ambao hatawataja hadharani kwa kuhofia vyombo vya dola kuwafuatilia. Binafsi nilishtushwa sana na kauli hii ya Mbowe na nilijawa na shauku ya kujua ni akina nani hao na kama wanasaidia chama kwa good faith, iweje wafuatiliwe na vyombo vya dola? Mbona Mustapha Sabodo amekuwa akikisaidia chama hicho hadharani na wala hajawahi kuguswa na vyombo hivyo?

Kutokana na kauli hiyo ya Mbowe, kama kawaida yangu niliingia chimbo ili kuwafahamu wafadhili hao na kwa nini Mbowe hataki kuwaweka hadharani.

Wakati nikiendelea na chimbo langu, licha ya kuwabaini wafadhili hao, nimebaini kuwa wafadhili wakubwa wa chama hicho, taasisi ya Ujerumani ya KAS, imesitisha kufadhili chama hicho mara baada ya uamuzi wa CHADEMA kumsimamisha Lowasa kuwa mgombea Urais badala ya Dr Slaa ambaye amefanya kazi na taasisi hiyo kwa muda mrefu. Ni kutokana na hali hiyo, ndipo Mbowe alipomtumia Lowasa kupata wafadhili wa ndani ili kuziba pengo hilo. Wafuatao ni baadhi ya wafadhili hao nami najitolea kuwaweka hadharani.

1. ROSTAM AZIZ
Huyu ndiye mfadhili namba moja wa CHADEMA kwa sasa. Ufadhili wa Rostam kwa CHADEMA unatokana na uswahiba wake kwa mgombea Urais wa chama hicho, Edward Lowasa. Wawili hawa ni wahanga wa siasa ndani ya CCM na kutokana na jeuri ya pesa waliyokuwanayo ndani ya chama hicho, walidhani kuwa wao ndo kila kitu. Hata walipoambiwa wajivue gamba, Rostam alitii amri ila Lowasa aliendelea kuwa mkaidi kwa kuamini kuwa pengine chama kingelegeza msimamo juu yake.

Kwa sasa Rostam, ametoa fedha kiasi cha shilingi milioni 50 kwa kila jimbo ambalo CHADEMA wamesimamisha wagombea Ubunge. Hata hivyo, Rostam hajatoa fedha kwa majimbo ya wabunge wa vyama vingine washirika wa UKAWA. Pia Rostam ametoa dola za Kimarekani milioni 20 ili kufadhili kampeni za Lowasa.

2. YUSUPH MANJI
Huyu ni mfadhili namba mbili wa CHADEMA ijapokuwa ni mgombea Udiwani kwa tiketi ya CCM kata ya Mbagala Kuu. Ukaribu wa Lowasa na Manji ndio uliomfanya akageuka kuwa mfadhili wa chama hicho na ufadhili wake unaishia Oktoba 2015. Manji ametoa shilingi bilioni 12 kusaidia harakati za Lowasa kwenda Ikulu na wanaojua fedha hizo ni Mbowe na Lowasa tu.

3. REGINALD MENGI
Mengi ametokea kuwa na mahaba na CHADEMA kutokana na sababu za kihistoria na kijiografia. Jukumu alilokabidhiwa Mengi ni kuhakikisha kuwa Media zote hasa zile za marafiki zao zinakuwa na msimamo wa aina moja huku Lowasa akipewa kavareji ya kutosha kuliko wagombea wengine.

4. NAZIR KARAMAGI
Naye yupo kwenye hiyo orodha ya Mbowe. Karamagi anashirikiana kwa karibu na akina Hamis Mgeja kuhakikisha kuwa kanda ya Ziwa, Lowasa anapata kura za kutosha. Karamagi ndiye aliyetoa milioni 23 kule Geita wakati wa ziara ya Lowasa mkoani humo ili zitumike kuhamasiaha watu waende kwa wingi kumpokea Lowasa. Kilichotokea ni kwamba watu walikula fedha na hawakufanya kama walivyokubaliana. Pia Karamagi ametoa shilingi kama hizo kwenye mikoa ya Shinyanya, Mwanza, Kagera na Simiyu.

5. RESERVED

Wadau, hawa ndio wafadhili wa Lowasa na CHADEMA. Wengi kati ya hao taswira yao kwenye jamii ni mbaya na ndo maana Mbowe anakuwa na kigugumizi kuwataja waziwazi kwa kuhofia kupoteza idadi kubwa ya wapiga kura
Duh! wewe kweli ni kiona mbali, kwa hali ilivyo sasa hivi ktk kumpinga Raisi kutekeleza yale waliokuwa wanapigia kelele ni wazi wafadhili wao ndio hao wapiga deal.
 
Back
Top Bottom