Hawa ndio Wafadhili wakuu wa CHADEMA ambao Mbowe hataki kuwataja hadharani

Lizaboni

JF-Expert Member
Feb 21, 2013
33,894
20,372
Wadau amani iwe kwenu.

Mtakumbuka hivi karibuni, Mwenyekiti wa CHADEMA, FREEMAN MBOWE amenukuliwa akisema kuwa chama hicho kina wafadhili watano ambao hatawataja hadharani kwa kuhofia vyombo vya dola kuwafuatilia. Binafsi nilishtushwa sana na kauli hii ya Mbowe na nilijawa na shauku ya kujua ni akina nani hao na kama wanasaidia chama kwa good faith, iweje wafuatiliwe na vyombo vya dola? Mbona Mustapha Sabodo amekuwa akikisaidia chama hicho hadharani na wala hajawahi kuguswa na vyombo hivyo?

Kutokana na kauli hiyo ya Mbowe, kama kawaida yangu niliingia chimbo ili kuwafahamu wafadhili hao na kwa nini Mbowe hataki kuwaweka hadharani.

Wakati nikiendelea na chimbo langu, licha ya kuwabaini wafadhili hao, nimebaini kuwa wafadhili wakubwa wa chama hicho, taasisi ya Ujerumani ya KAS, imesitisha kufadhili chama hicho mara baada ya uamuzi wa CHADEMA kumsimamisha Lowasa kuwa mgombea Urais badala ya Dr Slaa ambaye amefanya kazi na taasisi hiyo kwa muda mrefu. Ni kutokana na hali hiyo, ndipo Mbowe alipomtumia Lowasa kupata wafadhili wa ndani ili kuziba pengo hilo. Wafuatao ni baadhi ya wafadhili hao nami najitolea kuwaweka hadharani.

1. ROSTAM AZIZ
Huyu ndiye mfadhili namba moja wa CHADEMA kwa sasa. Ufadhili wa Rostam kwa CHADEMA unatokana na uswahiba wake kwa mgombea Urais wa chama hicho, Edward Lowasa. Wawili hawa ni wahanga wa siasa ndani ya CCM na kutokana na jeuri ya pesa waliyokuwanayo ndani ya chama hicho, walidhani kuwa wao ndo kila kitu. Hata walipoambiwa wajivue gamba, Rostam alitii amri ila Lowasa aliendelea kuwa mkaidi kwa kuamini kuwa pengine chama kingelegeza msimamo juu yake.

Kwa sasa Rostam, ametoa fedha kiasi cha shilingi milioni 50 kwa kila jimbo ambalo CHADEMA wamesimamisha wagombea Ubunge. Hata hivyo, Rostam hajatoa fedha kwa majimbo ya wabunge wa vyama vingine washirika wa UKAWA. Pia Rostam ametoa dola za Kimarekani milioni 20 ili kufadhili kampeni za Lowasa.

2. YUSUPH MANJI
Huyu ni mfadhili namba mbili wa CHADEMA ijapokuwa ni mgombea Udiwani kwa tiketi ya CCM kata ya Mbagala Kuu. Ukaribu wa Lowasa na Manji ndio uliomfanya akageuka kuwa mfadhili wa chama hicho na ufadhili wake unaishia Oktoba 2015. Manji ametoa shilingi bilioni 12 kusaidia harakati za Lowasa kwenda Ikulu na wanaojua fedha hizo ni Mbowe na Lowasa tu.

3. REGINALD MENGI
Mengi ametokea kuwa na mahaba na CHADEMA kutokana na sababu za kihistoria na kijiografia. Jukumu alilokabidhiwa Mengi ni kuhakikisha kuwa Media zote hasa zile za marafiki zao zinakuwa na msimamo wa aina moja huku Lowasa akipewa kavareji ya kutosha kuliko wagombea wengine.

4. NAZIR KARAMAGI
Naye yupo kwenye hiyo orodha ya Mbowe. Karamagi anashirikiana kwa karibu na akina Hamis Mgeja kuhakikisha kuwa kanda ya Ziwa, Lowasa anapata kura za kutosha. Karamagi ndiye aliyetoa milioni 23 kule Geita wakati wa ziara ya Lowasa mkoani humo ili zitumike kuhamasiaha watu waende kwa wingi kumpokea Lowasa. Kilichotokea ni kwamba watu walikula fedha na hawakufanya kama walivyokubaliana. Pia Karamagi ametoa shilingi kama hizo kwenye mikoa ya Shinyanya, Mwanza, Kagera na Simiyu.

5. RESERVED

Wadau, hawa ndio wafadhili wa Lowasa na CHADEMA. Wengi kati ya hao taswira yao kwenye jamii ni mbaya na ndo maana Mbowe anakuwa na kigugumizi kuwataja waziwazi kwa kuhofia kupoteza idadi kubwa ya wapiga kura
 
Awataje itusaidie nini watanzania. Sisi tunataka mabadiliko ccm iondoke madarakani ww unakuja na ngonjera za kumezeshwa uongo,fitina,ghiliba,uzadiki,chuki na unafiki. Mabadiliko na lowasa Ni lazima tushawachoka ccm. Tunataka new begining kwa maendeleo,utendaji kazi WA kweli na uwajibikaji wa kweli na kutukuka.
 
Wafadhili wa ccm ni wananchi wote

Reserved my foot ,mzushi na mzandiki kweli wewe....
IMG-20150921-WA0072.jpg
 
Kama kweli mfadhili wa lowasa kwa sasa ni Rostam mbona chanel yake ya Chanel Ten haimsaidi kumtangaza lowasa na ukawa kila kukicha kumualika Slowslow aje amjeruhi lowasa kwa maneno pingili?
 
Good question; na hilo ndio tatizo la mtu mmbea na muongo; you can not keep track of your statements and reconcile them!!!

Goo
Umesema Manji ametoa shilingi Billion 12 na wanaozijua hizo fedha ni Mbowe na Lowassa tu!(Only)
Swali:
Wewe umezijuaje?
 
Lizaboni

Huwa hamuweki kumbukumbu katika mambo yenu na ndio maana hamuachi kuandika ujinga hata uwe wa kujirudiarudia
Reginald Mengi Ajitoa Rasmi Kwa Lowassa






Tangu mbio za Urais zianze kushika kasi mkurugenzi wa IPP Media ndugu Regnald Mengi alionekana wazi wazi kuiunga mkono timu ya UKAWA

Ghafla Mkurugenzi huyo ameamua kujitoa kwenye timu hiyo baada ya kuona anapoteza nguvu zake wakati ana uhakika wa 100% kuwa Magufuli ndiye Rais wa awamu ya tano. Mengi amesema haoni faida ya kupoteza muda wake kumuunga mkono mtu mwenye uhakika wa kushindwa. Mengi amekubali wazi kuwa ushindi wa kiti cha Urais 2015 ni wa Magufuli... "kama hawa jamaa watashinda nafasi ya Urais basi ni baada ya miaka 10 siyo hivi sasa, huu mwaka ushindi utakuwa wa Magufuli tu tutake tusitake"

Pigo kubwa kama hilo limeambatana na kuondoka kwa wasanii mbalimbali waliotimkia kambi ya Ndugu Magufuli akiwemo Aunt Ezekiel, Ray na Juma Nature. Mshirika wake mkuu Hussein Bashe nae amejiweka pembeni na kuutangazia umma kuwa "ili wananchi wawe salama ni lazima kiti cha urais kikabidhiwe kwenye mikono salama, kinyume chake wananchi hawatokuwa salama, na mikono salama ni ya ndugu Magufuli tu"

Mwaka wa kufa nyani miti yote huteleza, EDO keshaanza kufa na miti yake pia imeanza kuteleza taratibu


 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom