Hawa ndio wachina tunaotaka kuwapa ardhi yetu

Mimi sijawahi kumkubali mchina. Hakika ni mara 100 uibiwe na mzungu kuliko mchina. Mzungu ana aibu katika uizi, anakofaidi anakutengeneza,yaani tungekuwa bado na wazungu mpaka sasa hii nchi ingekuwa kama ulaya,lakini tumewakaribisha hawa wachina,hawa wanakwangua kila kitu lakini hawaleti maendeleo wenyewe wanakubana kwenye mikataba migumu,isiyowezekana. Ona wanavyoiba mpaka magogo,madini,mali asili,lakini hakuna maendeleo wanayotuachia. Sijui kwa nini viongozi wetu hawamuoni mchina kwa jicho la pili? Wako kimaslahi zaidi
 
Africa tutaendelea kuibiwa tu maana viongozi wetu wengi wapo kimaslahi zaidi,ukiona mradi Africa unakataliwa jua ten percent haipo
 
Okay.
Mimi sijawahi kumkubali mchina. Hakika ni mara 100 uibiwe na mzungu kuliko mchina. Mzungu ana aibu katika uizi, anakofaidi anakutengeneza,yaani tungekuwa bado na wazungu mpaka sasa hii nchi ingekuwa kama ulaya,lakini tumewakaribisha hawa wachina,hawa wanakwangua kila kitu lakini hawaleti maendeleo wenyewe wanakubana kwenye mikataba migumu,isiyowezekana. Ona wanavyoiba mpaka magogo,madini,mali asili,lakini hakuna maendeleo wanayotuachia. Sijui kwa nini viongozi wetu hawamuoni mchina kwa jicho la pili? Wako kimaslahi zaidi
Umesomeka.
Halafu wengi mlioandika kujibu huu Uzi naona mnamiliki simu za Kichina sasa hakuna namna ndo maana mnawatetea tu!
 
Mababu zetu walijengewa makanisa na wakapewa bibles wazungu wakachukuwa nchi.

Sisi tunajengewa madaraja na majumba marefu, Wachina wanachukuwa nchi.
 
katika vitu ambavyo mchina hana shida navyo ni ardhi,china ni kubwa mno,na mpaka kuna ghost cities huko,yaani unakuta mji mkubwa,majengo ya hatari yako matupu hayana watu,leo aje kuiba heka mia za kwamtogole kweli?
China hataki ardhi, anataka resources zilizoko chini ya ardhi. Sasa kama hizo ghost cities kama washazinyonya mpaka kuzimaliza kwao za kazi gani? Ndio uone kwamba wanapomaliza haja zao basi wanakuwachia magofu yako wanasonga mbele!
 
ardhi sio ishu kwa mchina,mchina anatafuta mahali pa kufanya biashara,serikali ya china haiwezi kuifanyia kitu mbaya Tanzania hata siku moja,zingine ni propaganda tu za watu,wala china haitapata hasara kutowekeza hapa kwani wanawekeza kila kona ya hii dunia
 
@ikipendaroho,hizo ghost city ni brand news houses,sio kwamba zimezeeka zikaachwa,yaani wamefocuss miaka mia mbele na wanaweka mazingira tayari ili vizazi vijavyo visikose makazi
 
Propaganda za kimagharibi.. Mbona walitujengea Tazara na hatukuibiwa
Waulize Sri Lanka kama ni propaganda, wachina wamehukua bandari yao kwa miaka 99, wanafanya wanachotaka, wanaingiza na kutoa vitu watakavyo bila serikali ya Sri Lanka kujulishwa chochote, hata kama ni wanyama wanaweza toa kimya kimya.
Usicheze na wachina kabisa hawa jamaa ni worse kuliko West.
Ukweli hakuna wa kutusaidia ni kusimama wenyewe na kupiga kazi sio kutegemea wengine, wao nao wana wananchi wao wana matatizo yao.
 
katika vitu ambavyo mchina hana shida navyo ni ardhi,china ni kubwa mno,na mpaka kuna ghost cities huko,yaani unakuta mji mkubwa,majengo ya hatari yako matupu hayana watu,leo aje kuiba heka mia za kwamtogole kweli?

Hua mnanishangaza sana watu ambao mnaongea vitu toka vichwani mwenu bila proof yoyote wala data, msifanye mambo kiholela mtakufa masikini.
Hakuna kitu mchina anathamini kama ardhi, mnaoamini wachina ni very ignorant. Huoni visiwa wanavyoiba huko southeast asia, wanajenga vingine karibu na nchi za watu kujaribu kuexpand territory yao, port waliyochukua sri lanka kwa miaka 99, ardhi waliyochukua zambia? Mic walizoweka jengo la AU baada ya kulijenga wakawa wanaspy mazungumzo yote yanayoendelea, na walikamatwa wakakiri.

Unadhani sisi ndiyo special sana kwa wachina kwamba watuachie kila kitu burebure tu? Nyie mkiona mtu anawachekeachekea mnamuona wa maana mnataka mumpe kila kitu. Soma acha kuongea mambo juujuu, njoo na real data. China is worse than western countries sasa hivi.
 
shida ni kwamba mambo mazito ya hii nchi yanajadiliwa katika vikao ambavyo moja ya wajumbe wake ni Ndugai, Lusinde, Kangi Lugola, Msukuma, Sugu, na wasomi wengine waliotanguliza njaa na ustawi wao mbele kama Prof Kabudi
 
Waulize Sri Lanka kama ni propaganda, wachina wamehukua bandari yao kwa miaka 99, wanafanya wanachotaka, wanaingiza na kutoa vitu watakavyo bila serikali ya Sri Lanka kujulishwa chochote, hata kama ni wanyama wanaweza toa kimya kimya.
Usicheze na wachina kabisa hawa jamaa ni worse kuliko West.
Ukweli hakuna wa kutusaidia ni kusimama wenyewe na kupiga kazi sio kutegemea wengine, wao nao wana wananchi wao wana matatizo yao.
Naomba kasoro zilizopo kwenye mkataba wa ujenzi wa bandari bagamoyo .

Hapa kuna watu watageuzwa tena kama chapati. Watu hawajajua upande wa kusimamia hadi Sasa! Na ni makada.
 
Hivi sugu nayeye ana njaa desaini ya hao wengine..?
shida ni kwamba mambo mazito ya hii nchi yanajadiliwa katika vikao ambavyo moja ya wajumbe wake ni Ndugai, Lusinde, Kangi Lugola, Msukuma, Sugu, na wasomi wengine waliotanguliza njaa na ustawi wao mbele kama Prof Kabudi
Huyo kabudi naona kama anapigwa mawe yasiyostahili.

Akiwa msomi na mwajiliwa wa serikali ameonekana kufaa atumike nafasi ya juu kama aliyopo now, sasa 'mfano' ulitaka akatae uteuzi huo ili iweje?
 
Wachina wanamitego mingi sana,ukizingatia viongozi wa Africa walivyo, ni bayana wanataka kuja kuimiliki Africa
 
@kichomi,kuna tofauti kubwa kati ya mitego ya mchina na ya nchi za magharibi,wakkati US amebase kusambaza majeshi kila kona ya dunia,mchina kabase kusambaza makampuni na kujenga miundombinu ya silk road
 
Back
Top Bottom