Hawa ndio wachawi wa CCM

wakuu hivi yale majina matano pale dodoma yalitoka kwenye mfuko wa mkapa ama kikwete? nimesahau kidogo wakuu nikumbusheni...
 
hivi tokea lini serikali iingie hasara kiasi kikubwa kuliko bajeti yake ya mwaka? unajua bajeti ya Tz kwa mwaka 1 wa fedha ni sh ngapi? wizara ya nishati ilitengewa bajeti kiasi gani ili iingie hasara ya kiasi cha zaidi ya trillion 294?
Mkuu achana na huyo jamaa…anajua kabisa ukweli lakini anataka kutupotezea mda
 
Mkapa nae hata habadiliki!!yaani mpaka sasa huko kusini kawatukana watu….yaani kwa hadhi yake na cheo chake ilibidi awaachie akina kibajaji watukane na mama Mshamu…Yaani ni aibu sana CCM
 
Adui na bundi wa chama cha CCM wapo ndani ya CCM na sio nje ya CCM.
Hapa ni baadhi ya hao maadui nitajaribu kuwataja

1.Mkapa kajilimbikizia mali yeye,familia yake na marafiki zake na na akijua kuwa ni kinyume cha maadili ya CCM. Dharau, majigambo na matusi yalikuwa yakiwafanya baadhi ya wana CCM kujisikia kuwa hawana haki ya chama kilichokuwa kikiitwa chama cha wanyonge. Kibuli chake cha kutosikiliza wana CCM na Watanzania kiliwafanya wengi kukichukia chama cha CCM

2.Hapa Kikwete hawezi akakosekana..Kikwete kaiongoza nchi hii kiushikaji bila kujali hata maslahi ya wana CCM wenyewe..CCM alioianzisha Nyerere ilikuwa ni kwa maslahi ya wana CCM na Watanzania kiujumla…Kuna wazee wa CCM wamelitumikia taifa hili kwa juhudi zote lakini hawakufikiriwa kuongezewa maslahi yao na badala yake vijana au watoto wadogo ambao kwa mda mchache wamekuwa na utajiri wa kukithiri..Je kuna mtu ambae atawasahau wale wazee waliofanya kazi ktk Jumuia ya Afrika Mashariki???Wazee wengine wako mbele ya haki na hawajapata chochote…Masikini walimu na madaktari!!!

Kikwete kapuuzia maoni ya rasimu ya Katiba ilioandaliwa na Warioba..Hapa baadhi ya ana CCM wenye kuipenda nchi hii wakaanza kujitoa kwa kuona kuwa katiba iliyotungwa na Vijisenti na Sitta ilikuwa ni kwa ajili ya "wateule wachache"

Ufisadi mkubwa ambao ulikuwa wazi(RICHMOND,EPA,MEREMETA….ESCROW
NK)kaufumbia macho bila kuchukua hatua zozote

4. Makinda naye kaliendesha Bunge la Tanzania kama yuko ndani ya kikao cha chama cha CCM.Hakusikiliza hoja muhimu la taifa hili.Aliruhusu matusi na kejeli kutumika na akiwaachia wana CCM kuvunja kila aina ya kanuni pale mjengoni na huku akijua anakwenda kinyume na maslai ya taifa..wananchi wengi na hata wana CCM wengine hawakuridhishwa na utaratibu huo ambao mambo mengine yalikuwa ni maslahi mapana ya Taifa na sio ya chama cha CCM…Mswaada kama wa Mafuta na gesi umewaumiza wananchi wengi na hata wana CCM wenyewe

5.Sitta kawa ni adui mmoja mkubwa sana..Huyu hataweza kusahaulika kwa Watanzania wengi na hata kwa wana CCM..Huyu alisahau kuwa waliotoa maoni katika rasimu ya Warioba walikuwa pia wana CCM..mpaka sasa hivi yeye na baadhi ya wana CCM wanadhani rasimu alioiandaa Warioba ni ya maoni ya wana UKAWA peke yake na kwamba wana CCM hawakushirikishwa..Baadhi ya wana CCM na wapenda nchi hii ikabidi waichukie CCM na uongozi wake wakijua kuwa Rasimu ya Chenge ni kwa ajili ya "wateule" peke yao..
Sitta ndio alioisababisha kuzaliwa kwa UKAWA..Kwa hiyo kufa kwa CCM kumerahisishiwa sana na Sitta. Watanzania na wana CCM wengi hawataweza kumsahau Sitta kwa kuiua CCM mapema

3.Nape amekuwa akitoa matusi na kejeli sio kwa wapinzani peke yake bali hata kwa wana CCM…Hayuko mtu atakaesahau alivyosema CHADEMA ni chama cha Wachaga na huku akisahu kuwa ndani ya CCM kuna Wachaga…Mke wa Mkapa ni Mchaga..ndio kusema Wachaga walio ndani ya CCM inabidi watoke na waende kwa "wachaga" wenzio huko CHADEMA…na mbaya zaidi hivi kalibuni alivyomtukana mzee Warioba kuwa ni "ni mzee na anasubiri ……" sasa kwa kauri kama hizi ziliwafukuzisha baadhi ya makundi yaliyotengwa

4. Lugha,kejeli,majigambo, matusi nk ya viongozi wa CCM imewafukuzisha watu wenye busara zao kuona kuwa CCM sio ile ya Nyerere..Lugha kama "ninaapa kuwa Raisi hawezi kutoka kaskazini" imeua mori ya wana ccm na hata wale ambao wangeshawishika kujiunga au kukirudia hicho Chamahayuko mtu atakaesahau kauli kama
"hata nyasi mtakula lakini ndege ya Raisi itanunuliwa","kila mtu atabeba msalaba wake mwenyewe", "Vijisenti", "hela ya mboga",Kama huna nauli piga mbizi"," Buziku wanye barabarani wasambaze kinyesi iwe rami"

Hao ni baadhi ya maadui wa CCM…mengine malizia naenda kulala
Uzi pendwa
 
Hii ina maana kuwa Lowassa na hao maadui wengine wote hawatufai.

Kwa hiyo Watanzania tunatakiwa kumchagua mtu ambaye hana madoa ili tuanze nngwe mpya ya viongozi wasafi.

Magufuli amekuwa serikalini kwa miaka mingi na ameweza kuepuka vishawishi vya rushwa na ufisadi papa. Tumchague Magufuli na kuanza nngwe mpya ya viongozi wasafi na kuacha kulaghauliwa na mafisadi kama Lowassa na wapambe wake.
Huku kubadili rangi , ni shadow ban ya makusudi?
 
Adui na bundi wa chama cha CCM wapo ndani ya CCM na sio nje ya CCM.
Hapa ni baadhi ya hao maadui nitajaribu kuwataja

1.Mkapa kajilimbikizia mali yeye,familia yake na marafiki zake na na akijua kuwa ni kinyume cha maadili ya CCM. Dharau, majigambo na matusi yalikuwa yakiwafanya baadhi ya wana CCM kujisikia kuwa hawana haki ya chama kilichokuwa kikiitwa chama cha wanyonge. Kibuli chake cha kutosikiliza wana CCM na Watanzania kiliwafanya wengi kukichukia chama cha CCM

2.Hapa Kikwete hawezi akakosekana..Kikwete kaiongoza nchi hii kiushikaji bila kujali hata maslahi ya wana CCM wenyewe..CCM alioianzisha Nyerere ilikuwa ni kwa maslahi ya wana CCM na Watanzania kiujumla…Kuna wazee wa CCM wamelitumikia taifa hili kwa juhudi zote lakini hawakufikiriwa kuongezewa maslahi yao na badala yake vijana au watoto wadogo ambao kwa mda mchache wamekuwa na utajiri wa kukithiri..Je kuna mtu ambae atawasahau wale wazee waliofanya kazi ktk Jumuia ya Afrika Mashariki???Wazee wengine wako mbele ya haki na hawajapata chochote…Masikini walimu na madaktari!!!

Kikwete kapuuzia maoni ya rasimu ya Katiba ilioandaliwa na Warioba..Hapa baadhi ya ana CCM wenye kuipenda nchi hii wakaanza kujitoa kwa kuona kuwa katiba iliyotungwa na Vijisenti na Sitta ilikuwa ni kwa ajili ya "wateule wachache"

Ufisadi mkubwa ambao ulikuwa wazi(RICHMOND,EPA,MEREMETA….ESCROW
NK)kaufumbia macho bila kuchukua hatua zozote

4. Makinda naye kaliendesha Bunge la Tanzania kama yuko ndani ya kikao cha chama cha CCM.Hakusikiliza hoja muhimu la taifa hili.Aliruhusu matusi na kejeli kutumika na akiwaachia wana CCM kuvunja kila aina ya kanuni pale mjengoni na huku akijua anakwenda kinyume na maslai ya taifa..wananchi wengi na hata wana CCM wengine hawakuridhishwa na utaratibu huo ambao mambo mengine yalikuwa ni maslahi mapana ya Taifa na sio ya chama cha CCM…Mswaada kama wa Mafuta na gesi umewaumiza wananchi wengi na hata wana CCM wenyewe

5.Sitta kawa ni adui mmoja mkubwa sana..Huyu hataweza kusahaulika kwa Watanzania wengi na hata kwa wana CCM..Huyu alisahau kuwa waliotoa maoni katika rasimu ya Warioba walikuwa pia wana CCM..mpaka sasa hivi yeye na baadhi ya wana CCM wanadhani rasimu alioiandaa Warioba ni ya maoni ya wana UKAWA peke yake na kwamba wana CCM hawakushirikishwa..Baadhi ya wana CCM na wapenda nchi hii ikabidi waichukie CCM na uongozi wake wakijua kuwa Rasimu ya Chenge ni kwa ajili ya "wateule" peke yao..
Sitta ndio alioisababisha kuzaliwa kwa UKAWA..Kwa hiyo kufa kwa CCM kumerahisishiwa sana na Sitta. Watanzania na wana CCM wengi hawataweza kumsahau Sitta kwa kuiua CCM mapema

3.Nape amekuwa akitoa matusi na kejeli sio kwa wapinzani peke yake bali hata kwa wana CCM…Hayuko mtu atakaesahau alivyosema CHADEMA ni chama cha Wachaga na huku akisahu kuwa ndani ya CCM kuna Wachaga…Mke wa Mkapa ni Mchaga..ndio kusema Wachaga walio ndani ya CCM inabidi watoke na waende kwa "wachaga" wenzio huko CHADEMA…na mbaya zaidi hivi kalibuni alivyomtukana mzee Warioba kuwa ni "ni mzee na anasubiri ……" sasa kwa kauri kama hizi ziliwafukuzisha baadhi ya makundi yaliyotengwa

4. Lugha,kejeli,majigambo, matusi nk ya viongozi wa CCM imewafukuzisha watu wenye busara zao kuona kuwa CCM sio ile ya Nyerere..Lugha kama "ninaapa kuwa Raisi hawezi kutoka kaskazini" imeua mori ya wana ccm na hata wale ambao wangeshawishika kujiunga au kukirudia hicho Chamahayuko mtu atakaesahau kauli kama
"hata nyasi mtakula lakini ndege ya Raisi itanunuliwa","kila mtu atabeba msalaba wake mwenyewe", "Vijisenti", "hela ya mboga",Kama huna nauli piga mbizi"," Buziku wanye barabarani wasambaze kinyesi iwe rami"

Hao ni baadhi ya maadui wa CCM…mengine malizia naenda kulala
Paragraph ya pili itawatafuna Viongozi mpaka wanaingia Kaburini !
Dharau zao kwa wale waliokisaidia Chama na kuwakashifu itawatesa sana !!
Wamejilimbikizia mimali kibao lakini Mungu ni Fundi huenda akawalimbikizia Maradhi yasiyopona pia ili kulipa vilio vya wanaoteseka kwa madhila waliowafanyia wenzao !!
Mungu ni mwema na huwa hana haraka ! Muda utafika tu “ Karma “
 
Back
Top Bottom