Hawa ndio viongozi wa CCM wa sasa

Linguistic

JF-Expert Member
Mar 16, 2021
3,671
8,237
Wakuu M/kiti Wa CCM Mkoa Wa Mara namba tatu amemshauri Rais Samia Kuwaondoa Wateule Wote Wa Hayati Magufuli Maana Sio Wote Wanampenda.

 
Duuh! Kwani #3 yeye kaukwaa uenyekiti kipindi gani? Japo yeye siyo Mteule!
Kajitambua
drakelaugh.png
 
Baadhi ya Sera/Sheria mbovu za nchi ni kuwanyang’anya vijana uwezo.

Hapa naongelea vijana kuminywa kwa kuporwa haki zao, kunyimwa haki na kupuuzwa (hawasikilizwi). Naanza kwa Kuongezeka kwa Deni la Taifa na Propaganda mfu za Serikali, zenye lengo la kuhadaa umma ili kubaki madarakani tu. Serikali ya AWAMU YA 5 ilitamka kuwa inajenga miradi mikubwa kwa FEDHA za ndani. Asilimia kubwa ya Watanzania waliamini na kushangilia, na wale wachache wenye uelewa hawakupewa nafasi ya kuhoji. Imekuja kujulikana kuwa, FEDHA za Mifuko ya Jamii zilichukuliwa na Wafanyakazi wakaporwa haki zao za kulipwa FAO LA KUJITOA na kuchelewesha malipo ya Wastaafu.

Vijana wasomi, waliosoma sayansi na wenye ujuzi wameajiriwa kwenye Makampuni, Mashirika na Viwanda. Hizi ni talent, na hazina za wasomi kwa nchi, na walivyoajiriwa kwenye haya Makampuni na Viwanda, wamepata fursa ya kuongeza utaalamu na uzoefu. Hii ndio Econonomic interelligency ambayo Serikali ilipaswa kutumia ili kunyanyua uchumi wa nnchi through Innovation. Ajira na mikataba za hawa vijana (wenye utaalamu na uzoefu-Innovation) zilivyokoma, Serikali iliwanyima Akiba zao (PESA za NSSF). Kumbuka Serikali ilifuta fao la kujitoa mwaka 2018 na kuweka Fao la kukosa ajira. Watu wote skilled labour (wataalamu hawa), hawapewi akiba yao, Haki imepotea. Hawa watu wangelipwa fedha zao, wangeweza kujiajiri kwa kufungua makampuni, kujenga viwanda vidogo. Badala yake hawa skilled labour wanaambiwa wasubiri miezi 18 na kama hawataajiriwa, wakae hadi 55 years wastaafu.


Serikali ilitumia pesa za mifuko ya jamii (Kukopa au kupora kienyeji) ili kujenga miradi. Hapo awali serikali imesema inajenga miradi kwa pesa za ndani (propaganda)..Lakini ukweli wenyewe ni kupora haki za wafanyakazi vijana na mafao wastaafu. Pia Serikali ilikopa sana Nje na kwenye mabenki, ndio maana deni la taifa limepaa sana.


Serikali inapaswa kuwapa wafanyakazi akiba zao ili waweze kutumia skill zao na uzoefu waliopata katika makampuni/viwanda ili kufungua biashara mpya. Hii ndio namna ya kutanua wigo wa Kodi (MWugulu NCHEMBA TRA). Mitaji itatoka wapi ya biashara mpya kwa wazawa kama mikopo benki sio rafiki? Suluhisho ni Serikali kurejesha FAO LA KUJITOA NSSF na kulipa wafayakazi akiba zao kwa Haki.

Serikali inatakiwa kuwezesha vijana, kutoa International passport kwa graduate wote, ili wapambane fursa za ajira kokote duniani. Baadae watakuwa diapora kubwa inayotuma pesa Tanzania, kama ilivyo Zimbabwe, Kenya na India walivyoenda wengi Canada na UK. Serikali kurejesha Fao la Kujitoa, Hasa kwa Sekta binafsi, kwa kuzingatia kuwa Sekta binafsi Security ya ajira ni delicate sana.
 
Back
Top Bottom