Hawa ndio vijana wamenivutia katika miongo miwili hii tuliyonayo

mtimawachi

JF-Expert Member
Apr 1, 2020
2,017
3,037
Habari wanajukwaa!

Leo nimeona niwalete kwenu vijana wenzetu ambao kwa namna moja ama nyingine wametoa mchango katika taifa letu.

Kwanza niwe wazi katika siasa mimi ni mshabiki wa CCM,na kisoka nipo Msimbazi(simba)

Katika kipindi hiki cha miongo miwili ninakiri kuna vijana wengi tumejitahidi kulitetea/kulijenga taifa letu katika moyo wa kizalendo ila hawa wenzetu wamebahatika kuonekana zaidi

(1) ZITTO KABWE
Hakuna asiyejua mchango wa huyu kijana akiwa pale chadema chini ya uongozi wa Mbowe na Slaa

(2) NAPE NNAUYE
Huyu naye tunajua misimamo yake,nadhani tuna kumbukumbu nzuri kipindi kile cha kujivua gamba

(3) MBWANA SAMATA
Kwa wapenzi wa michezo tunajua nini kijana wetu anakifanya

(4) HALIMA MDEE
Ni mwanamke ambaye ameonyesha ujasiri mkubwa sana katika siasa za upinzani hadi kupelekea baadhi ya wanaume kuogopa kupeleka posa kwa kudhani maisha yake kisiasa ndio atakayoleta ndani

(5) JANUARY MAKAMBA
Huyu naye amejitahidi hasa katika siasa zisizo na mipasho

(6) TUNDU LISSU
Ni mwanasheria lakini bingwa wa siasa za amsha amsha

(7) HUMPHREY POLEPOLE
Nadhani kila mtu alimsikia huyu kijana hasa katika rasimu ya katiba ya mzee Warioba

(8) PAUL MAKONDA
Najua wapo watakaobeza hapa lakini kiutendaji huyu kijana amejitahidi

(9) JOHN MNYIKA
Kama ilivyo kwa Zito,Mdee Mnyika.Vijana hawa wamesaidia sana kuwaamsha ccm ambao walikuwa usingizini.Nakumbuka kipindi nipo Mtwara kipindi cha bunge wakisimama hawa vijana watu walikuwa wanashangilia kama limeingia goli langoni kwa yanga

(10) NASSIB ABDUL
Huyu dunia inamtambua kama DIAMOND PLATNUM,licha ya tabia zake za kifuska lakini ameutendea haki mziki

(11) ROSE MHANDO
Huyu aliitendea haki miziki ya injili

(12) HAJI MANARA
Huyu ni msema hovyo wa klabu ya simba.Ameleta hamasa kubwa sana kwa mashabiki hadi tunajikuta tanagombania kujaza uwanja

(13) JERRY MURO
Kama ilivyo kwa Haji,huyu naye alikuwa msema hovyo wa upande wa yanga na ni watani wa jadi
Nadhani tunamkumbuka Muro na kipindi chake cha 'Usiku wa habari' pale TBC

(15) NANCY SUMARY
Alishindana miss world na kututoa kimasomaso,na katika mamiss huyu namzimikia sema mazingira hayaniruhusu kumfikia

(16) MOHAMED DEWJI
Huyu ni kijana ametutoa kimasomaso katika utajiri

(17) VICENT KIGOSI
Anatambulika kama RAY.
Mchango wake tumeuona katika filamu

Orodha hii nimezingatia walio hai tu

NB: Hizo namba hazimaanishi kwamba nimewapa ubora kwa namba,hapana ni mtiririko tu
NAOMBA ieleweke huu ni mtazamo wangu mimi mtimawachi na chanzo ni mi mwenyewe

KARIBUNI
 
Usimuache na huyu Comrade.
ElmwDDRUcAAeHkP.jpg
 
JIDE




Namkubali sana huyu yaani ye anajua kusimamia kipaji chake hana shobo na siasa pia hafanyi biashara za kuigaiga. Yaani kiufupi ye ni herself.
 
Nimemweka Lisu kwa sababu mkuu,miaka kumi nyuma alikuwa na umri nilionao sasa na ndio kipindi ambacho kipo ndani ya mada
Hiyo miaka 10 nyuma alikuwa akisikika slaa yeye kaja kuibuka na kick za risasi tu.
 
Millard Ayo
Huyu anaitendea vyema tasnia ya habari kama mwandishi wa kujitegemea.
 
Back
Top Bottom