Hawa ndio vijana walioshika vibuyu wakati wa tukio la Muungano.

MsemajiUkweli

JF-Expert Member
Jul 5, 2012
13,172
23,975
Cg8mMMPW4AEvrqC.jpg


VIDEO:


Wakati Watanzania wakiadhimisha miaka 53 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar, siku ulipochanganywa udongo wa pande mbili za Muungano kulikuwa na mazingira ya ajabu na mabadiliko ya vipindi vya hali ya hewa vilivyowababaisha na kuwashangaza watu wengi waliohudhuria sherehe hizo.

Sherehe za kuchanganya udongo wa pande mbili uliowekwa kwenye vibuyu viwili tofauti zilifanyika Aprili 26, 1964 kwenye Uwanja wa Taifa, jijini Dar es Salaam na Mwalimu Nyerere alichanganya udongo kwa kuumimina ndani ya chungu kuashiria Muungano wa Tanganyika na Zanzibar.

Mmoja kati ya watu waliobeba udongo wa Zanzibar na kuchanganywa na ule wa Tanganyika, Hassan Omar Mzee (69) kutoka Kibweni nje ya Mji wa Unguja, anaitaja siku hiyo ilikuwa ya aina yake atakayoikumbuka maishani. Wakati wa tukio hilo alikuwa na umri wa miaka 16.

Hassan anasema kazi ya kuchanganya udogo wa Tanganyika na Zanzibar ilianza saa tatu asubuhi na kukiwa na manyunyu ya mvua, jua lisilounguza likiwaka na kupotea na mawingu yaliyokuwa na kivuli cha ubaridi yakiwa yametulizana juu ya anga huku ukimya ukitawala eneo la uwanja.

Anasimulia kuwa lilikuwa tukio la aina yake ambalo liliwashangaza viongozi wengi wa nje na ndani, waliohudhuria na kushuhudia kitendo hicho cha kijasiri na cha kihistoria kilichofanywa na viongozi wa mataifa ya Tanganyika na Zanzibar, Mwalimu Julius Nyerere na Sheikh Abeid Amani Karume.

Mshangao huo unatokana na mazimio ya harakati za vikao vingi vya viongozi wa Kiafrika, walikuwa na lengo la kuungana baada ya kujikomboa kutoka kwenye ukoloni, lakini maazimio hayo yaliwashinda viongozi wengi pia Nyerere na Karume walitekeleza kwa vitendo.

Anasema siyo Mwalimu Nyerere wala Mzee Karume walionekana kuwa na hofu ya kupoteza madaraka ya nchi zao, hawakutaka kuendekeza fahari ya vyeo vyao na badala yake walichokitanguliza mbele ni nia na azma ya kujenga umoja wa kitaifa wa watu wao.

Jamhuri ya watu wa Zanzibar na ile ya Tanganyika ndipo zilipokufa. Mabeberu na wakoloni wakipigwa na butwaa kuona kitendo hicho kikitokea na viongozi wa pande mbili wakiwa na nyuso za furaha na bashasha pia wananchi wengine wakionekana kutokwa na machozi ya furaha kutokana na tukio hilo.

Akielezea tukio hilo, Hassan anawataja wenzake wengine watatu walioshiriki katika kazi ya kubeba udongo wa pande mbili za Muungano ni Hassan Kheir Mrema na Sifaheri Kunda kutoka Tanzania Bara na Khadija Abbas kutoka Zanzibar.

Wenzao wanawake walibeba vibuyu vidogo na vikubwa vyenye udongo na wanaume walibeba chungu kimoja kilichochanganyiwa udongo, tukio lilifanyika katikati ya Uwanja wa Taifa ambako jukwaa maalumu lilijengwa.

“Siku hiyo tuliamka mapema tukiwa tumepewa mavazi maalumu, wanaume tulivaa shati na suruali zilizoshonwa kwa vitenge, wenzetu wa kike walivaa mavazi maalumu ya khanga zilizozingatia utamaduni wa Mwafrika,” anaeleza Hassan.

Anasema kabla ya kazi hiyo kufanyika, kulikuwa na mazoezi ya vitendo wiki moja nyuma yake, jinsi ya utaratibu mzima utakavyokuwa hadi kuchanganywa udongo wakiongozwa na Bi Mwakemwa, ndiye aliyekuwa mwenyeji wao tokea walipowasili Dar es Salaam na kupiga kambi Uwanja wa Taifa.

Hassan anaeleza ilipofika saa tatu juu ya alama wananchi kutoka Tanganyika na Zanzibar walikusanyika na kukaa kwenye jukwaa la Uwanja wa Taifa kwa utulivu, wakisubiri kuona na kushuhudia tukio la kihistoria likifanyika ili kuziunganisha nchi mbili kuwa Taifa moja.

Anaeleza baada ya kazi hiyo kukamilika, akiwa na wenzake waliondoka hadi kwenye jukwaa kuu wakiwa na vifaa vilivyotumika kubeba udongo na baadaye kwenda kukaa sehemu waliopangiwa kabla ya kuanza safari ya kuelekea Ikulu ya Dar es Salaam.

Anaeleza walipofika Ikulu kulikuwa na tukio kubwa la kihistoria ambapo ulipandwa mti wa mwembe wa kumbukumbu ya Muungano, uliopandwa na Mwalimu Julius Nyerere akishirikiana Mzee Karume, ukapewa jina la mwembe wa Muungano kwa sababu ulitumika udongo kutoka Tanganyika na Zanzibar .

“Mimi nilimkabidhi galoni lililokuwa na maji Mwalimu Nyerere ili kuumwagia mti uliopandwa, Hassan Kheri alimkabidhi Mzee Karume galoni jingine na kuumwagia mwembe huo, hadi leo mwembe huo upo, ni mkubwa kuliko yote ndani ya uzio wa Ikulu,” anasema Hassan.

Baada ya kumalizika kazi hiyo, sehemu ya udongo uliobakia na vifaa vilivyotumika vilipelekwa kwenye Makumbusho ya Taifa, hadi leo vitu hivyo vinaoonekana na kushuhudiwa na wanaokwenda kuitembelea makumbusho hiyo.

“Udongo wa Zanzibar uliochanganywa na ule wa Tanganyika ulitoka eneo la Kizimbani Unguja, ule wa Tanganyika ulichotwa maeneo ya Dar es Salaam, udongo toka maeneo hayo sasa umeliunganisha taifa zima na mipaka yake, sasa tuna Taifa moja la Tanzania na kiti kimoja Umoja wa Mataifa, ” anasema Hassan.

D92A0542.jpg


Picha ya mti wa mwembe uliopandwa Ikulu Dar es Salaam.
 
Sasa tunawataka wautenganishe huo mchanga na kuikata Miti yote iliyoota kwenye mchanga huo ili tuuvunjilie mbali huo muungano wa bandia
 
Sasa tunawataka wautenganishe huo mchanga na kuikata Miti yote iliyoota kwenye mchanga huo ili tuuvunjilie mbali huo muungano wa bandia
Badala ya kuwataka wao wakufanyie hiyo kazi, kwa nini wewe usiifanye?

Yaani tatizo lako unataka utatuliwe na mtu mwingine? Huu ni uvivu wa kiwango kikubwa kifikra achilia mbali kimwili!
 
Sasa tunawataka wautenganishe huo mchanga na kuikata Miti yote iliyoota kwenye mchanga huo ili tuuvunjilie mbali huo muunga
no wa bandia
Unawataka akina nani ? si ukakate kama kweli wewe kijeba, kujiona unaweza kumbe huna uwezalo zaidi ya kupakata lapyako na kutoa mashuzi ovyo hapo.
 
hahhaahhaaa hatari sana maaana masuala ya muungano yamekua mazito sana
 
Kwani mimi ndiye nilichanganya huo mchanga acha uvivu wa kufikiri
Mvivu wa kusoma, kufikiri na kuandika ni wewe!

Umeambia mchanga na mti uko Ikulu. Vifaa vilivyotumika viko makumbusho.

Nenda Ikulu ukautenganishe huo mchanga.

Nenda makumbusho ya Taifa ukachukue hivyo vibuyu ili ukamilishe zoezi lako lililobebwa na fikra za alinacha.
 
Sasa tunawataka wautenganishe huo mchanga na kuikata Miti yote iliyoota kwenye mchanga huo ili tuuvunjilie mbali huo muungano wa bandia

1. Kila mara watu wanahangaika kutafuta vazi la taifa kumbe hizi zinaweza kuwa reference
2. Huo mwembe nao unatakiwa utunzwe vizuri either kwa prunning au thinning afu eneo linalozunguka lingefanyiwa landscapping kidogo.

Ni story nzuri, pia anayeijua story ya nembo ya taifa: Adam na Hawa naye angetupatia.
 
Zanzibar ilitembelewa na Myunani Plotemy akitokea Misri karne ya pili tuu tangu kuzaliwa Yesu na hata injili nyingine hazikuwa zimeandikwa na kukuta taifa la Wazanzibar.Tanganyika ilichukua maelfu ya karne kuwa taifa baadaye
Walihitaji wa nini muungano huu
Barghash
 
kilikuwa kitendo cha ujinga!! Mambo ya udongo yakazi gani? Tulipaswa unganisha nguvu ya kutafuta maendeleo siyo viudongo chyaa!
 
Badala ya kuwataka wao wakufanyie hiyo kazi, kwa nini wewe usiifanye?

Yaani tatizo lako unataka utatuliwe na mtu mwingine? Huu ni uvivu wa kiwango kikubwa kifikra achilia mbali kimwili!
Hayo ya miaka ya sitini hayatuhusu Sisi tunajua Tanzania hata kama walipandishwa Mbuzi dume na Jike Sisi hatukuwepo, Vijana wengi hayo mambo ni historia Ndio maana Tundu lisu alijenga hoja hazikujibiwa kuhusu muungano
 
22/04/1964 Mkataba wa Kuitawala Zanzibar na 26/04/1964 kuanzisha rasmi ukoloni wa Tanganyika huko Zanzibar
 
Zanzibar ilitembelewa na Myunani Plotemy akitokea Misri karne ya pili tuu tangu kuzaliwa Yesu na hata injili nyingine hazikuwa zimeandikwa na kukuta taifa la Wazanzibar.Tanganyika ilichukua maelfu ya karne kuwa taifa baadaye
Walihitaji wa nini muungano huu
Barghash
Kasumba: Myunani aliyetokea Misri kuja Zanzibar karne ya pili ana significance gani kwa taifa huru la Zanzibar au insignificance gani kwa taifa la Tanganyika. Huyo Myunani aliomgeza nini Zanzibar au kupunguza nini Tanganyika? Nchi zote za Afrika zilikuwepo hata kabla ya ujio wa wapelelezi na wamisionari kutoka Ulaya, Mashariki ya Kati au Mashariki ya mbali. Tunapaswa kujivunia mataifa yetu, na hasa baada ya kupambana kujikomboa na kuwa mataifa huru badala ya kudhani kuwa kutembelewa na wageni hao (wengine wakiwa wamepotea njia tu, kwa mfano, lama Christopher Clumbus alivyopotea njia akaiahia kwenda Amerika nadala ya India) kuwa alama ya umashuhuri wa mataifa yetu.
 
Back
Top Bottom