Serayamajimbo
Senior Member
- Apr 15, 2009
- 191
- 38
Absalom Kibanda
RAIS Jakaya Kikwete ametangaza rasmi azma yake ya kugombea urais kwa muhula wa pili mwakani, huku akitangaza kaulimbiu mpya anayokusudia kuingia nayo katika mapambano hayo kuwa ni ile ya kuwatengea vijana nafasi kubwa zaidi ya uongozi.
Kikwete ambaye hakuna shaka kwamba moja ya sifa zake alizojitanabahisha nazo katika kipindi chake cha kwanza cha urais kuwa ni ile ya kusema maneno mengi ambayo matokeo yake ni vigumu kuyapima katika vitendo, alitoa wito huo wakati akizungumza na vijana katika moja ya matukio ya kisiasa katika kipindi cha wiki mbili au tatu zilizopita.
Nilipomsikia na kisha nikasoma katika vyombo vya habari kuhusu ahadi yake hiyo ya kikampeni sikutaka kuwa miongoni mwa watu wa kwanza kuchangia hoja hiyo, kwa maana ya ama kumuunga mkono au kumpinga kama alivyofanya yeye mwenyewe.
Hata hivyo, kwa makusudi niliamua kwa dhati kuliweka hilo kando na kuwageukia vijana ambao rais alikuwa akiwaangalia kwa kiwango cha kufikia hatua ya kuwaandalia fursa za kushika madaraka makubwa ya dola katika siku zijazo.
Haraka haraka nilianza kuangalia kwa kituo mchango wa kiuongozi na kimadaraka ambao umekuwa ukitolewa na vijana katika nafasi mbalimbali za kimamlaka wakati huu na nikarejea kidogo katika siku zilizopita.
Katika mwelekeo huo huo, nililigeukia Baraza la Mawaziri linaloongozwa na Rais Kikwete mwenyewe na kupepesa macho nikiwaangalia baadhi ya mawaziri na naibu mawaziri vijana ambao kwa miaka minne wamepewa fursa ya kuliongoza taifa hili.
Majina ya vijana yaliyonijia kichwani haraka haraka ni Lawrence Masha, Dk. Deodatus Kamala, William Ngeleja, Dk. Hussein Mwinyi, Emmanuel Nchimbi na Dk. Mathayo David Mathayo.
Nilipomaliza upande huo wa serikali, nilivigeukia vyama vya siasa, kikiwamo Chama Cha Mapinduzi (CCM) na nikawadadisi baadhi ya vijana machachari na ambao kwa namna moja au nyingine mchango wao umegusa hisia za wananchi walio wengi.
Katika kundi hili, nilikutana na baadhi tu ya majina kama yale ya akina John Mnyika, Halima Mdee, Januari Makamba, Zitto Kabwe, Nape Nnauye, Hussein Bashe, Peter Serukamba, Mhonga Said, Lucy Mayenga, John Mrema, David Kafulila, James Mbatia, Jussa Ismael Ladhu na wengine wengi.
Haraka haraka nilipoyaangalia majina haya na kuangalia namna kila mmoja wao alivyotoa mchango wake wa uongozi kama mwanasiasa - kwani kwa hakika hawa ndio ambao wanatoa mwelekeo wa kiwakilishi wa kundi la vijana aliokuwa akiwalenga Kikwete - mara moja nilibaini mambo kadha wa kadha.
Miongoni mwa mambo ambayo hakuna shaka yalikuja haraka haraka kichwani mwangu, ni kuwapo kwa vijana miongoni mwa hawa ambao pasipo kujali mchango wao katika medani ya uongozi, wawe ni kwa wema au kwa ubaya, wameonyesha nidhamu ya hali ya juu, wakiwa mfano wa kauli na matendo ndani na nje ya taasisi ambazo walikuwa wamepewa kuziongoza.
Katika kundi hili, nilikutana na majina kama ya Dk. Mathayo, Hussein Mwinyi, Nchimbi na Kamala ambao hakuna shaka katika kipindi cha uongozi wao wakiwa ama naibu mawaziri au mawaziri wameweza kuficha udhaifu wao na wakati huo huo wakionyesha nidhamu katika misingi ya uwajibikaji wa pamoja, na hivyo kuwaacha wakuu wao wa kazi, waziri mkuu, makamu wa rais na rais kuwa watu pekee wanaoweza kujua michango yao katika kuongoza.
Ukiwaacha hao, vijana wenzao wengine kama walivyo Ngeleja na Masha, kila mmoja katika eneo lake la uongozi kwa namna ya pekee, pengine ni kutokana na kuwa kwao katika wizara nyeti na zinazogusa hisia na fikra za watazamaji wengi, wamejikuta wakiingia katika mizozo na taswira za uwezo wao wa kiuongozi na uadilifu wao wa kimatendo na kifikra kutiliwa shaka sana.
Wakati Ngeleja akionekana dhahiri kupwaya katika kumshauri Rais Kikwete na wananchi katika kuchukua maamuzi thabiti ya kulinusuru taifa kutoka katika fedheha ya kutafunwa na giza nyuma ya kivuli cha mitambo ya Dowans na jinamizi la Richmond, Masha naye kwa zaidi ya mara moja ameonekana kuyumba katika kuisimamia Wizara ya Mambo ya Ndani anayoiongoza.
Watu wanaofuatilia mwenendo wa mambo na kuyatafakari kwa kina, wanaweza wakawa mashahidi wazuri kwamba, udhaifu mkubwa wa kiuongozi katika Wizara ya Nishati na Madini tangu Ngeleja aliposhika madaraka, ndiyo ambao umeharibu taswira ya kikazi ya Shirika la Ugavi wa Umeme nchini (TANESCO), hata kusababisha wananchi na wadau wengine wa kisiasa washindwe kuliangalia katika jicho sahihi la kihakiki.
Leo hii haiba ya kusakamwa anayoibeba Mkurugenzi Mtendaji wa TANESCO, Dk. Idris Rashidi pamoja na ukweli kwamba inatokana pia na staha yake ya uhafidhina katika misingi ya kiuongozi, ndani ya taasisi hiyo nyeti, bado ukweli ni kwamba, hulka ya kushindwa kuchukua maamuzi magumu ya Ngeleja akiwa waziri na mshauri wa rais katika masuala yanayohusu nishati, ndiyo ambayo yameichochea kwa kiwango kikubwa hali hiyo.
Kwa upande wake, Masha naye ambaye leo hii anaonekana kuwa kiongozi kijana na mbabe anayejiamini kuwa mfano wa watu bora katika taifa hili, anaingia katika kundi hilo hilo la uongozi, akijitwisha mzigo wa maswali mengi na kutoaminika, hali inayoanzia katika Jimbo la Nyamagana ambako yeye ni mbunge hadi ndani ya kuta za wizara yake.
Hulka yake ya kuwa mtu anayeonekana kutomhofia au kujali chochote na anayejiamini kupita kiasi, ambayo walakini alianza kuijenga tangu akiwa wakili katika kampuni ya uwakili ya IMMMA aliyoanzisha akiwa na wenzake kadhaa, ni mambo ambayo leo hii yanamfanya aonekane kuwa ni mtu tofauti na yule ambaye wakati fulani akiwa kijana zaidi alipata kuongoza shirika lililokuwa na misukosuko mingi la TOL.
Watu wanaomfahamu Masha kama kiongozi ni mashahidi wazuri kwamba, ile haiba ya kijana mtulivu na mwenye akili zinazochemka na nidhamu ya hali ya juu ya kazi aliyokuwa nayo akiwa mwanasheria na baadaye Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa TOL, ni tofauti kabisa na ile aliyoanza kuwa nayo tangu akiwa IMMMA na baadaye ndani ya mtandao wa ushindi wa Kikwete kabla hajapata fursa ya kuwa naibu waziri na kisha waziri kamili.
Ukiwaacha hao ambao leo hii wamepata fursa ya kuongoza ofisi za umma kwa kuteuliwa, wako vijana wengine nje ya wigo huo, hususan wale walio ndani ya vyama vya siasa, ambao nao tunao sababu za kutosha za kuwapima katika mizani ya kuandaliwa urithi aliowatangazia Kikwete.
Miongoni mwao, wale ambao majina yao nimeyataja hapo juu, wako wale ambao hakuna shaka ndani ya vyama vya upinzani wana kila sababu ya kutembea kifua mbele kwa sababu nyingi tofauti, baadhi kutokana na uwezo wao na matunda bora ya kazi zao, huku wengine wakiwa na sababu ya kufanya hivyo si kwa kuwa wanaweza, bali kwa sababu ya umaarufu wao mkubwa.
Miongoni mwa wale ambao wanaweza kutembea kifua mbele wakibeba sifa za kuwa viongozi bora, pamoja na kuwa wamepata kufanya makosa kadhaa ya kimaamuzi yanayoweza yakawa ni matunda ya udogo wa umri uliowakosesha uzoefu, wako Mnyika wa CHADEMA, Jussa wa CUF na Januari Makamba wa Ikulu.
Watu wanaozifahamu vyema siasa za vyama vya CUF na CHADEMA kwa mapana na marefu, ni mashahidi wazuri kwamba, nidhamu ya hali ya juu ya kazi, kujituma, ubunifu, umakini wa kutenda na uhodari wa kisiasa walionao vijana wawili; Mnyika na Jussa, ambao aghalab wanayo mapungufu, wanaweza wakawa ni mashahidi wazuri kwamba, vijana hao wanastahili kuwa warithi wa fursa za juu za kiuongozi ndani ya vyama vyao na katika taifa.
Ninao uhakika thabiti kwamba, kukosekana kwa vijana hawa wawili katika siasa za ndani ya Bunge au katika Baraza la Uwakilishi (kwa Jussa) ni moja ya mambo ambayo kwa kiwango kikubwa yametoa fursa kwa vijana wengine kuvuma na kuonekana kuwa maarufu kuliko walivyo wao.
Katika hilo ninao uhakika mwingine pia kwamba, iwapo vijana hawa wawili na wenzao wengine wengi wa ndani ya vyama vyao vyao na nje wangepata fursa za kiuongozi walizonazo akina Nchimbi, Ngeleja, Masha na wenzao wa aina yao, Rais Kikwete au yeyote ambaye angekuwa mkuu wa nchi, angekuwa akitembea kifua mbele kujivunia vijana hawa.
Japokuwa unaweza ukawa na mitazamo inayokinzana kuhusu silika zao za kiuongozi, leo hii Jussa ni tegemeo kuu la kiushauri, kimkakati na kivisheni ndani ya CUF na katika macho ya viongozi wakuu wa chama hicho kama Profesa Ibrahim Lipumba na Maalim Seif Sharif Hamad kijana huyo ni mfano wa kuigwa.
Kama ilivyo kwa Jussa ndani ya CUF, Mnyika ambaye mara zote amekuwa akikaimu ukatibu mkuu Dk. Willbrod Slaa anapokuwa nje ya ofisi za makao makuu ya CHADEMA, akiwaweka kando manaibu katibu wakuu wawili (wa bara na visiwani), akiwamo Zitto na Hamad Yussuf, ni mfano wa kiongozi kijana aliyejitwalia sifa za kupikwa kushika madaraka makubwa siku zijazo.
Nje ya vyama hivyo viwili vya siasa, yuko Januari Makamba ambaye wiki iliyopita nilimtaja katika safu hii, na kutosita kumpa sifa anayostahili ya aina ya viongozi vijana wenye visheni na ambao kwa bahati mbaya au nzuri ubora wao unafichwa na udhaifu wa viongozi walio juu yao. Sina sababu ya kumjadili.
Ukiwaacha hao, wako vijana wa aina ya Zitto, Kafulila na Nape ambao kwa hakika kila mmoja anao umaarufu wake katika jambo moja au mawili, na wote hao wakistawi si kwa sababu yoyote ile, bali misimamo yao ya kikauli na kimatamshi waliyopata kuitoa katika medani ya kisiasa.
Kwa kigezo cha umaarufu, juu yao vijana hao wote yuko Zitto ambaye hakuna shaka uwezo wake mkubwa wa kujenga hoja aliojitwalia ndani ya Bunge tangu zama za hoja ya Buzwagi vilimfanya aanze kuonekana kuwa tunda sahihi na urithi mwema ndani ya kambi ya upinzani, kabla sifa lukuki alizobeba na kubebeshwa na watu mbalimbali, mimi mwenyewe nikiwamo, hazijaonekana kumuelemea na kuelekea kumuangusha.
Nyuma ya umaarufu huo wa Zitto, akazaliwa Kafulila ambaye akitumia mgongo wa mbunge huyo wa Kigoma Kaskazini na uwezo wake binafsi wa kujenga hoja unaokwenda sambamba na hulka yake ya kutumia siasa za kichimvi na kupindisha mambo kama walivyo wanasiasa mabingwa wa fitina wa ndani ya CCM, akajijengea uhalali ndani ya CHADEMA kabla ya kuanguka na kukimbilia NCCR Mageuzi.
Katika minajili hiyo hiyo ya kutafuta umaarufu na kutumia kama kigezo cha uwezo wa kiuongozi, ndani ya CCM yuko Nape, kijana anayejijenga juu ya hoja za kurudiarudia mashambulizi yake dhidi ya aliyekuwa Waziri Mkuu Edward Lowassa kwa kiwango cha kutaka kumfanya ngazi ya kupandia kwake kisiasa. Vijana wa kundi hili la mwisho ambao kiwango chao cha kitaaluma si cha kutiliwa shaka, wanazo fursa nyingi za kuteka makundi tofauti ya watu kwa kiwango cha kuonekana kuwa ni aina ya viongozi wenye uwezo mkubwa wa kiuongozi, ilhali katika medani za kiuongozi baadhi yao kama si wote, kwa nyakati tofauti wamepata kuthibitisha kuwa si lolote si chochote. Katika mazingira ya namna hii ya kuwa na kundi dogo sana la vijana wenye nidhamu ya kazi na wanaofahamu misingi ya uwajibikaji wa pamoja, huku wengi wao wakiwa ni wale wanaojistawisha katika umaarufu waliojengewa au kujijengea kwa njia halali na haramu, taifa lina kila sababu ya kutafakari mara mbili kabla ya kuamua kuwapa dhamana ya kutuongoza katika siku zijazo. Eti hawa ndio warithi wa Kikwete.