Hawa ndio jopo la Majaji watano watakaotoa hatima msimamo wa Kisheria kuhusu Ma-DED Kusimamia Uchaguzi.....

kasenene

JF-Expert Member
Jun 6, 2008
1,131
2,000
Wadau nimeamua kuwaletea List ya jopo la majaji watano (5) wa mahakama ya Rufani walioteluliwa kusikiliza rufaa ya sababu ya serikali kupinga hukumu ya mahakama Kuu inayowaengua Wakurugenzi katika jukumu la kusimamia uchaguzi kwa niaba ya Tume ya Taifa ua Uchaguzi (NEC).

Sina shaka na Mahakama zetu saana ila tunaelewa kuhusu "figisu figisu" ambazo zimekuwa zikifayika siku hizi kutokana na muhimili huo kuingiliwa na wanasiasa na mbaya zaidi mpaka kuingiliwa katika uteuzi wa nafasi zao .. Ifuatayo ni List ya Majaji hao na baadhi ya wasifu wao wachache

1. Jaji Rehema Mkuye Aliapishwa Tarehe 23:12:2016 Rais Mnamfahamu
2. Jaji Mwambegele Aliapishwa Tarehe 23:12:2016 Rais Mnamfahamu
3. Jaji Mugasha : Wa siku nyingi kidogo ila 24:03:2017 aliapishwa na Rais kuwa Kamishina wa tume ya Utumishi wa Mahakama
4. Jaji Richard Mziray: Jaji wa siku nyingi ila kuwakumbusha tu huyu ndiye jaji aliyetengua hukumu ya Feberuary 2016 iliyomwondolea DPP mamlaka ya kuzuia dhamana ya mshtakiwa bila hata kulazimika kutoa sababu na baadaye yeye kufanya uamuzi wa kumrudhisia madaraka hayo DP siku chache baada serikali kukata Rufaa mwaka huo huo (Haraka Haraka)
5. Jaiji Augustine Mwarija ; Huyu ni Jaji wa siku nyingi na ndiye atakayekuwa kiongozi wa jopo la Majaji

Msisitizo Katika hatua hii hukumu utolewa kwa kupiga Kura kwa Majaji mara baada ya kusikiliza pande zoote.. mie nimetoa list bila kufanya hitimisho ili kuwapa fursa ya kujiandaa kwa lolote lile litakalo tokea..

Hapa chini ni baadhi ya Makala zinazowahusu hao majaji:

http://kusaganews.blogspot.com/2018/02/mahakama-yatoa-uamuzi-mwingine-mamlaka.html

http://tanzaniajudiciary.blogspot.com/2017/03/jaji-mu-gasha-aapishwa-kuwa-kamishna-wa.html
 

TODAYS

JF-Expert Member
Apr 30, 2014
6,139
2,000
Kwenye hii bandiko nime_note kipengele cha "Aliapishwa na Rais" zaidi ya hapo labda jaji ajitoe mhanga.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom