Hawa matapeli wanaojifanya wanachezesha bahati nasibu mtaani wamerudi kwa kasi

hamis77

JF-Expert Member
Aug 20, 2013
11,642
19,017
Kuna hawa MATAPELI kipindi Cha JPM walikimbia mji kabisa, walibanwa kende wakapotea

Hawa MATAPELI wanapewa vibali kabisa kutoka Serikalini vya kujifanya wanachezesha bahati nasibu

Hawa MATAPELI walijaa sana Dar, miaka ya 2005-2016, alipoingia JPM walipotezwa kimya kimya wakaacha kabisa

UTAPELI wao upo hivi; wanakuwa na asset kama redio, mabeseni, TV, n.k wanakuwa wanajifanya wanachezesha kwa mfumo wa namba, ukishinda kwa buku unaondoka na Redio au hela yenye thaman ya Redio au kitu ulichoshinda

UTAPELI wao upo hivi, wanakuja na rundo la watu wao, wakiwa asilimia kubwa wadada wa mjini, wamama watu wazima, vijana, huwa Ni kundi la watu hadi 50. Jion hulipwa.

Hawa ni watu wao, kwahiyo hawa ndio huonekana kama wanashinda, lengo ni kuvutia wasiojua wakiingia mtego, hasa wanaotoka mkoani. Enzi za nyuma walitega Sana hapo Ubungo

Ukijichanganya ukasogea unazungukwa unapewa kadi ya kucheza kilazima, hapo utaambiwa umeliwa utanyang'anywa Simu na pesa

Na Kama ujuavyo watu wa Dar hawana msaada.

Hawa MATAPELI wamerudi kwa Kasi, baada ya JPM kuwatokomeza na wakapotea kabisa. Kwa Sasa Wapo hapo Karume Kama unataka kuingia TFF, mlangoni pemben Kuna kituo Cha Polisi,m

Pia karibu na shule ya Uhuru wasichana. Pia wapo michezo yao Ni hiyo hiyo

Watu wasiolewa wanaumizwa Sana, wanaporwa Simu, wakizingirwa na hawa wanaojifanya wanashinda kumbe wenzao,

HAWA wenzao Kuna watu wazima wamama, Kuna mabint na wake za watu,

Serikali ipo ,watu wanaporwa mchana kweupe kwa kigezo Ni bahati nasibu. Hawa MATAPELI wamerudi kila Kona ya Dar .

IMG_2720.jpg
 
Walikuwepo hata wakati huyo jpm yupo.
Tena walikua pale mnazi mmoja toka 2017 hadi nadhani mwaka jana ndo nahisi wamehamia huko karume.
 
Back
Top Bottom