Hawa mafisadi wataendelea kuichezea Serikali mpaka lini? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Hawa mafisadi wataendelea kuichezea Serikali mpaka lini?

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by BAK, Jan 16, 2010.

 1. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #1
  Jan 16, 2010
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,780
  Likes Received: 83,133
  Trophy Points: 280
  Jeetu Patel, Manji wawatikisa wabunge

  Na Ramadhan Semtawa
  Mwananchi
  16/Jan/2010


  VITA ya kibiashara kati wafanyabiashara maarufu nchini, Yusuph Manji na Jayantkumar Chandubhai Patel, maarufu kama Jeetu Patel, inayotokana na zabuni ya kuingiza matrekta ya mpango wa Kilimo ya Kwanza, jana iliitikisa kamati ya Bunge ya Kilimo, Chakula na Mifugo.

  Zabuni hiyo ya kuingiza matrekta 1,000 yenye thamani ya zaidi ya Sh50 bilioni iliibua mjadala mzito katika kikao hicho na kumlazimisha mwenyekiti wa kamati hiyo kutumia mamlaka yake kuuzima.

  Tayari kumeibuka hisia nyingi kuhusu zabuni hiyo iliyoingiza wafanyabiashara hao wenye asili ya Kiasia katika mgogoro mkubwa, huku ikielezwa kuwa Ikulu imeingilia kati baada ya Rais Jakaya Kikwete, kusitushwa na taarifa hizo.

  Jana wabunge wa kamati hiyo waliibua upya sataka hilo baada ya kumbana Naibu Waziri wa Kilimo, Chakula na Ushirika, David Mathayo atoe kauli kuhusu mgogoro huo.

  Mbunge wa Chambani (CUF), Hemed Salim Hamis alikuwa wa kwanza kuibua sakata hilo baada ya kumtaka Mathayo aeleze mgogoro kati ya wafanyabiashara hao wakubwa.

  Hamisi hakuwataja kwa majina wafanyabiashara hao. Alihoji: "Swali la nyongeza liko katika matrekta 1,000 yanayopaswa kuingizwa na sekta binafsi. Kuna taarifa za mgogoro wa zabuni kati ya wafanyabiashara wawili wakubwa, mfanyabiashara Y na X sitaki kutaja majina yao wanajulikana, je unaweza kueleza kamati ukweli ni upi?"

  Baada ya swali hilo Waziri Mathayo alionekana kushusha pumzi na kusema: "Eheee!...Huo mgogoro unashughulikiwa kati ya Wizara na SUMA JKT ambao ndiyo walihusika moja kwa moja na zabuni."

  Hata hivyo, Hamis alimwuliza tena naibu waziri huyo akisema: "Ina maana, wizara ya Kilimo haihusiki?"

  Mathayo alifafanua kwa kukiri nafasi ya wizara yake katika mchakato huo, lakini akasisitiza kwamba mambo ya zabuni hiyo kwa kuwa yanahusu fedha nyingi zaidi, yanashughulikiwa na hazina na SUMA JKT.

  Naibu waziri huyo, ambaye aliongozana na wataalamu mbalimbali wa wizara alisema, wazo la SUMA JKT kutaka kuwa sehemu ya uingizaji huo matrekta hayo kwa kutumia Mfuko wa Pembejeo, lilikuwa zuri.

  "Wenzetu SUMA JKT walikuja na wazo zuri kutaka wasaidiane na taasisi nyingine kuingiza matrekta kupitia mfuko wetu wa pembejeo. Tulikubali kwa kuwa ni wazo zuri na kwamba yangekuwa yakiunganishwa Nyumbu," alitetea Suma JKT.

  Hata hivyo, mbunge wa Ubungo ambaye aliwahi kuwa Waziri wa Kilimo katika serikali ya awamu ya tatu, Charles Keenja alizidi kupigilia msumari baada ya kuhoji "kwanini fedha hizi zichukuliwe na kuingizwa tu katika jeshi.

  "Huku ni kuishi kwa matumaini tu, kuamini Nyumbu wanaweza kuunganisha matrekta yote 1,000 wakati ukiangalia uwezo wao wa vitendeakazi si mkubwa. Kwanini msipeleke TAMCO (Kibaha) ambao wana uwezo mkubwa?"

  Lakini, Mathayo alijaribu kutetea akisema si tu kwamba serikali imechukua fedha hizo na kuziiingiza jeshini kwa kuwa SUMA JKT pia imekuwa ikishiriki hata katika mradi wa kuingiza mbegu bora.

  Bado baada ya majibu hayo, Keenja alinyoosha tena mkono na kutaka kuendelea kumbana Mathayo, ndipo mwenyekiti wa kamati hiyo, Gideon Cheyo, alipozima mjadala akisema utajadiliwa zaidi mbele.

  "Inatosha, nafikiri tutajadili zaidi mbele ya safari. Hili ni suala ambalo ni pana tutalijadili tu waheshimiwa, kwa sasa tuendelee na mengine," alifafanua Cheyo.

  Awali, Hamis alitaka kujua idadi ya matrekta ambayo yataingizwa nchini kuanzia ngazi zote ikiwemo katika halmashauri mbalimbali za wilaya kwa ajili ya Kilimo Kwanza.

  Waziri Mathayo, ambaye alikuwa akiwasilisha Taarifa ya Mpango na Utekelezaji wa Bajeti kwa kipindi cha Julai hadi Desemba 2009, alisema jumla ya matrekta madogo (power tillers) yanayotarajiwa kuingizwa katika halmashauri ni 1,628, makubwa 28, wakati kati ya hayo 1,000 ndiyo hayo yatakayoingizwa na sekta binafsi, 400 mkopo kutoka Benki ya Exim India.

  Kuhusu upotevu wa vipuri kwa baadhi ya matrekta, alisema hilo linafanyiwa kazi na kuongeza kwamba, wiki moja ijayo kutakuwa na mkutano mkuu wa wadau ambao jambo hilo litazungumzwa kwa kina.

  Mgogoro wa Manji na Jeetu umekuwa ukichukua sura mpya kila kukicha. Tayari Manji aliwahi kunukuliwa akisema anajiandaa kuweka wazi jinsi Sheria ya Manunuzi ya Umma ya mwaka 2004, ilivyokiukwa wakati wa mchakato wa utoaji zabuni hiyo.
   
 2. Kigogo

  Kigogo JF-Expert Member

  #2
  Jan 16, 2010
  Joined: Dec 14, 2007
  Messages: 20,498
  Likes Received: 1,453
  Trophy Points: 280
  Serikali yenyewe legelege itashindwaje kuchezewa.rais kutwa kuzunguka kwenye ndege nchi linaoza huku yeye ana kazi ya kwenda kubembea
   
 3. Ndahani

  Ndahani JF-Expert Member

  #3
  Jan 16, 2010
  Joined: Jun 3, 2008
  Messages: 14,333
  Likes Received: 1,795
  Trophy Points: 280
  Tunavuna yale tuliyopanda. Na bado,safari ndo kwanza inaanza!
   
 4. Pakawa

  Pakawa JF-Expert Member

  #4
  Jan 16, 2010
  Joined: Mar 11, 2009
  Messages: 3,741
  Likes Received: 3,178
  Trophy Points: 280
  Ni mpaka pale watanzania watakaposema "sasa imekwisha"
   
 5. L

  Lori Member

  #5
  Jan 16, 2010
  Joined: Jan 14, 2010
  Messages: 13
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Wenyewe tunalea 'UKICHEZA NA POPI, UTAINGIA NAYE IBADANI'
   
 6. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #6
  Jan 17, 2010
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,780
  Likes Received: 83,133
  Trophy Points: 280
  Nangoja kusikia Ikulu baada ya kustushwa na kuamua kuingilia kati huu ugomvo wa "kilimo kwanza" kati ya mafisadi wakubwa wawili nchini itaamua nini. Maana wote hawa wanaogopwa na uVDG hivyo labda atawaambia huo mkataba wa kuleta matrekta ya bilioni 50 wagawane 50% kila mmoja ili kumaliza "ugomvi' huo.

  Niliandika hapa miezi michache iliyopita kwamba hii kauli mbiu ya "kilimo kwanza" ni bora ibadilishwe na kuitwa "mafisadi kwanza" niliandika kwa kejeli nikitegemea labda safari hii Serikali itafanya kweli na kusimamia mradi huu vizuri, lakini kejeli zangu naona kama zitakuwa kweli na mafisadi kuchukua kipaumbele katika mradi huu wa kilimo kwanza.
   
 7. The Invincible

  The Invincible JF-Expert Member

  #7
  Jan 17, 2010
  Joined: May 6, 2006
  Messages: 4,723
  Likes Received: 1,218
  Trophy Points: 280
  "Hawa mafisadi wataendelea kuichezea Serikali mpaka lini?"

  Ni mpaka pale watanzania, wenye nchi na serikali yao, watakapoamka kutoka usingizini
   
 8. Che Guevara

  Che Guevara JF-Expert Member

  #8
  Jan 17, 2010
  Joined: May 22, 2009
  Messages: 1,178
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 145
  Hao akina Manji na Jeetu Patel hawaichezei Serikali, ni kama wako nayo bega kwa bega (wanajuana), tokea wakati wa kampeni zilizopita.

  Majuto ni mjukuu, na kweli tumejuuuuta, ila kuna nafasi tena kwa watanzania mwaka huu 2010 kuchagua Rais na Wabunge.

  Kwanini dili/tenda zote kubwa ni wahindi walewale watuhumiwa wa ufisadi na mafisadi papa? Tena wale walio karibu zaidi na wanamtandao?
  Je zile za EPA, Mifuko ya Hifadhi, Richmond/Dowans haziwatoshi tu?

  Kweli wahindi wanatawala nchi kwa Remote control.

  Tuzinduke sasa!
  Kura yako ndiyo itakukomboa.
  Kuwang'oa mafisadi kwa kura inawezekana.
   
 9. Kang

  Kang JF-Expert Member

  #9
  Jan 17, 2010
  Joined: Jun 24, 2008
  Messages: 5,122
  Likes Received: 617
  Trophy Points: 280
  Mafisadi na Serikali ni kitu kimoja, sasa sidhani kama mtu unaweza kujichezea mwenyewe!!!
   
Loading...