Hawa madaktari wa kwenye magari vipi?

Sangarara

JF-Expert Member
Sep 29, 2011
13,100
5,649
Kwa muda sasa nimekuwa nikukutana na watu wanaojiita madaktari kwenye mabasi wakitoa elimu kwa abiria juu ya maswala ya afya.

Baada ya maelezo hayo wanatangaza dawa zao wanazodai kutibu magonjwa yote tena kwa mda mrefu.

Kwa mfano leo nimekutana na mmoja anayeiitwa dr.Nguda na dawa yake ya Sinnabilis power 10 juice.

Yeye badala ya kuwaonesha abiria wale cheti cha udaktari ama kibali cha kutoa huduma za kiafya,anatoa passport ya kusafia kuwa huwa anaenda Ulaya.

Hayuko consistent mahala zilipo ofice zake,mara kncu ,mara soko la kati.na dawa yake inanuniwa kweli.

Swali ni je,Hawa watu ikitokea amepata madhara,nani atalaumiwa? Inamaana watu watu wa serikali hawandi haya magari ili kuzuia uwezekano wa raia kutapeliwa?

Hawa jamaa wanapata hela kubwa kwa kuuza dawa ambazo ziko locally packed bila ya kodi,hili jambo ni sawa?

Mbaya zaidi wanataka watu wawasiliane naye kwa sms,ila nimejaribu mara kadhaa hawajibu.

NB.Senabillis power 10 juice ni juice ya mitishamba,haina kemikali yoyote ILA ISINYWEWE PAMOJA NA DAWA ZA MALARIA AMA TYPHOID.
 
TFDA walishawakataza wenye mabasi kuwaruhusu. Nilishawaona nkamwita konda kunwuliza akamnyamazisha chap. Change begins with you.
 
Binaa damu bana hawa ishwi jambo watu wakijiajiri mna anza kuwa uliza wamepata wapi ujuzi sasa inakuwaje apo ajira hamtak kutoa?
 
nadhani tuwaache watoe kwa sababu watu wenyewe wananunua kwa hiari yao wenyewe!
ila niliongea na mmoja kafunguka kuwa nia silimia ndogo tu ya wanayoyasema huwa na ukweli.
 
Leo nimechukua pakiti Moja Ili nisome internet kuhakiki Yale Dr Ng'unda amewaambia abiria ndani ya Bus La Lakrome Moshi to Karatu (Usafiri Maridhawa). Sasa sijaona zaidi ya Google kunituma kwenye huu Uzi.

Hebu mashuhuda wa hii dawa njooni hapa.
 
Back
Top Bottom