Beatrice Kamugisha
JF-Expert Member
- May 18, 2019
- 762
- 6,980
1. Edward Lowassa - alikuwa na nguvu CCM , akawa na nguvu upinzani huku akihesabika Kama shujaa wa mabadiliko. Hakudumu kwenye huo ushujaa akakubali kurudi CCM hadhi yake ikaporomoka na sasa anafanya watu wanayotaka siyo yeye anayotaka. Kisiasa hana Tena ushawishi, anazeeka akiwa amepotea kwenye ramani ya siasa.
2. Dkt. Wilbroad Slaa - huyu aliupigania sana upinzani lakini chama chake kikasaliti maono yake, badala apigane akiwa ndani akapaniki na kukaa pembeni. Akiwa huko pembeni akaamua kujiunga CCM kupambana na upinzani lakini hakupata nafasi yakutimiza ndoto yake. Leo hii ni mteule kama Balozi na waliomteua ni ambao alikuwa anaamini wanavunja sheria, katiba na wanadhulumu watanzania. Hata Leo naamini anaona maovu kutoka kwa wale waliomteua lakini awezi Tena kuyasemea. Yupo kifungo Cha fikra na wale waliokuwa wanamuunga mkono wamepoteza imani naye.
3. Bernard Membe - alisifika Kama Jasusi lakini kwa hali yake ya Sasa nachelea kuamini kwamba ni jasusi kweli. Alikosa urais 2015 akakasirika na baadaye akajiunga upinzani akitegemea atasimamishwa kama mgombea pekee mwenye nguvu wa upinzani. Hakutumia ujasusi wake kumwona Lisu, na Kama alimwona akutumia ujasusi huo kuona nguvu ya Lisu dhidi yake. Leo mambo yamebadilika, Hakuna kampeni Wala ushawishi, kwa umri wake amepotea kwenye ramani ya siasa za Tanzania kwa kutokujua Nini afanye kwa wakati gani.
4. James Mbatia - Amesimamia kwa muda mrefu hoja ya mama Tanzania, Amesimamia elimu na kujipambanua kama mpinzani wa kweli. Mwaka huu wakamlaghai akawasaliti wapinzani wenzake na kujitengenezea NCCR yake akiamini anakwenda kuwa chama kikuu Cha upinzani Tanzania. Akapewa mashangingi akaanza kupambana na chadema Mbeya chini ya ulinzi wa Dola na akaelekea Mara kuvuna wanachama. Kwa wakati huo anayafanya hayo aliamini anakwenda kuwa chama kikuu cha upinzani hivyo akawashawishi baadhi ya wabunge wa CHADEMA wamfuate. Mara paap Lissu akaingia nchini akabadili upepo wa siasa nchini. Waliomwaid Mbatia wabunge wakajikuta wao wenyewe hawana uhakika wakushinda, wakaachana na mipango yote wakabaki kukipambania chama chake. Leo hii Mbatia na watu wake hata uwezo wakufany kampeni Jimbo moja hawana. Usaliti.mwisho amepotea kwenye ramani za siasa.
5. Fredrik Sumaye - Huyu tayari amekwama, Leo nimemsikia anauliza Mbowe anamsaidiaje Lisu kwenye kampeni badala yakueleza anamsaidiaje Mwenyekiti wake wa chama kushinda urais. Kwisha.
6. Mrema, Cheyo, Shibuda, Mtatiro, Kafulila, Nassary, Machali, Mkumbo, Lipumba nk. Walikua na maono wakawika ila walipokubali kuishi kwa kutamani wao tu ndo waonekana wanang'ara na kuwa kileleni kisiasa basi hakuna wanachosema chenye tija kwa Taifa bali wanatamka chenye tija kwa familia zao.
Mwenyenzi Mungu anapokutumia uwavushe watu kutoka sehemu moja kwenda nyingine usiweke tamaa, kubali kuishi kwa njaa ila utimize lengo na dhamira ya nafsi yako. Bora ujipe Likizo ya Muda usome upepo ila usiruhusu kununuliwa