Hawa Ghasia sikia hii-Watumishi wa Halmashauri za Wilaya Wananyanyaswa sana. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Hawa Ghasia sikia hii-Watumishi wa Halmashauri za Wilaya Wananyanyaswa sana.

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by Ledio, Jul 14, 2011.

 1. L

  Ledio Member

  #1
  Jul 14, 2011
  Joined: Jun 15, 2011
  Messages: 30
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Napenda kutoa kilio changu kwa waziri wa Ofisi ya Rais, Menejiment ya utumishi wa Uma, juu ya mambo wanayotendewa watumishi walioko katika Halmashauri za wilaya. Huwa sipendi kuropoka na nalisema hili kwa ushahidi kwa kuwa sasa nina experience zaidi ya 10yrs nikiwa mtumishi katika Halmashauri hizi. Wakuu Idara katika Halmashauri zetu wamekuwa Miungu watu na pindi mnapofanya ziara katika Halmashauri huwa hampendi kusikiliza watumishi wengine hivyo hampati picha halisi ya manyanyaso wanayopata watumishi hao.
   
 2. e

  eedoh05 JF-Expert Member

  #2
  Jul 14, 2011
  Joined: Apr 20, 2011
  Messages: 633
  Likes Received: 39
  Trophy Points: 45
  Hawa Ghasia ana sifa na tabia kama jina lake lilivyo. Yeye mwenyewe ni mchafu hawezi kuona uchafu kwa mwenzie. Fuatilia alichokifanya kwenye kura za maoni alipokuwa anaomba awe mgombea ubunge kupitia ccm. Ukiyajua hayo, utafahamu kuwa Ghasia sio yeye peke yake ila ghasia wengine walishamtangulia.

  KWA UFUPI HIYO NDIYO CCM NA UFISADI WAKE, HADI NDANI YA HALMASHAURI.
   
 3. L

  Ledio Member

  #3
  Jul 15, 2011
  Joined: Jun 15, 2011
  Messages: 30
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  eedoh
  Inawezekana ni kweli unayosema lkn hayo ni upande wa siasa hayatakiwi kufungamana na utendaji kazi. Hebu jaribu kufanya mazungumzo na watumishi wa Halmashauri zilizo karibu nawe ili mradi tu wasiwe wakuu wa idara watakuambia kero wanazopata. Huku kwetu mtumishi wa kawaida kupata activity ni ndoto na hata ukiipata mpaka uje upate Hundi/Cheque ya malipo ni kuanzia wiki 3-miezi 2 wakati wakuu wa idara huwachukua masaa 2-3 kupata hizo cheque. ukweli ni kwamba Halmashaur zetu zimeoza yapo mambo mengi tu
   
 4. L

  Ledio Member

  #4
  Jul 15, 2011
  Joined: Jun 15, 2011
  Messages: 30
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mhe Hawa Ghasia kama unasoma huu ujumbe katika mtandao huu au kama kuna subordinate wake aniPM ili nimwambie manyanyaso wanayopata watumishi katika Halmashauri nayofanyia kazi.
  Wana JF wenzangu mimi naamin JF ndio kimbilio pekee la watz wanyonge katika kuelezea Shida na Matatizo yao wanazopata naomba tushirikiane kwa pamoja katika kutatua tatizo hili na kulifikisha mahala husika.
   
 5. m

  mchafukuoga Member

  #5
  Jul 24, 2011
  Joined: Apr 17, 2011
  Messages: 26
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  mkuu bora umesema ila hali ni mbaya kufanya kazi halmashauri ni kama jela.
  mtu anakaa zaidi ya miezi saba hujalipwa posho ya kujikimu wakati wa kuanza kazi,
  pia pesa ya usafiri ndio usisema ukiomba hela wanasema oc haina hela.
  hawa jamaa ni zaidi ya wanyama.
  mapunjo ya mishahara ndio kabisa miezi mpaka 3.
  jamani mimi naona kama huku zuluma imezidi sana.
  huyu waziri haoni haya.
   
Loading...