Hawa Ghasia asema wengi wanasema hana uwezo kuongoza TAMISEMI

Kilasi Mkuu

JF-Expert Member
Nov 25, 2013
2,325
719
Waziri anaye shughulikia wizara ya TAMISEMI amesema ameambiwa hana uwezo wa kuiongoza TAMISEMI kawni wizara hiyo inahitaji mtu makini mwenye weledi na nikubwa mno.

Taarifa yake ilikuwa kama utetezi kwamba hasimamii utendaji wa halmashauri na hasa wakurugenzi wake.

Amesema yeye anajitahidi kuwauliza wabunge kama halmashuri zao zina wakurugenzi mizigo,anasema wengi wa wabunge wamemwambia halmashauri zao zina wakurugenzi wazuri tu,sasa angechukueji hatua.

Hii imekuwa kama kujibu mwito wa yeye pamoja na waziri Mkuu Pinda kufukuzwa kazi kwa utendaji usio ridhisha.Wabunge walisema Pinda na mama Ghasia hawatoshi kenye nafasi.
 
Ghasia nilisoma nae Mzumbe university mpaka leo sielewi alipenyaje hadi kupata hadhi ya kuingia baraza la mawaziri....empty set yule
 
Muungwana akivuliwa nguo hadharani huchutama.

Busara ni kuchutama sasa.

Kama ana uwezo mdogo apumzike tu.
 
Ghasia nilisoma nae Mzumbe university mpaka leo sielewi alipenyaje hadi kupata hadhi ya kuingia baraza la mawaziri....empty set yule

wewe unataka kujua alipenya vipi kwani wewe ndiye uliyekuwa unatunga mitihani ya mzumbe na kuteua mawaziri kwanza uko nje ya topic unaonekana kama unachuki binafsi na ghasia kuwa mtu mzima basi.
 
wengi huonge kirahisi sana wakiwa nje ya uwanja akiingia hata kucheza mpira kumbe hajui lakini kwa kelele hajambo.
 
Waziri anaye shughulikia wizara ya TAMISEMI amesema ameambiwa hana uwezo wa kuiongoza TAMISEMI kawni wizara hiyo inahitaji mtu makini mwenye weledi na nikubwa mno.

Taarifa yake ilikuwa kama utetezi kwamba hasimamii utendaji wa halmashauri na hasa wakurugenzi wake.

Amesema yeye anajitahidi kuwauliza wabunge kama halmashuri zao zina wakurugenzi mizigo,anasema wengi wa wabunge wamemwambia halmashauri zao zina wakurugenzi wazuri tu,sasa angechukueji hatua.

Hii imekuwa kama kujibu mwito wa yeye pamoja na waziri Mkuu Pinda kufukuzwa kazi kwa utendaji usio ridhisha.Wabunge walisema Pinda na mama Ghasia hawatoshi kenye nafasi.

Amesahau ule usemi, "Wengi Wape"!!
 
Sina shaka sana huyu mheshmiwa ila kauli yake kuwa wabunge hawajampa kadoro ya wakurugenzi ni udhaifu mkubwa. Anapaswa kwenda kwa wananchi ndio enye matatizo sio wabunge
 
Mwenyekiti wa Kamati ya Hesabu za Serikali za Mitaa amependekeza mawaziri wa TAMISEMI wajiuzulu nafasi zao kwa kushindwa kusimamia wizara hiyo.
 
Hawa Ghasia!!! Aptitude tests zinahitajika kutumika hapa Tanzania katika kuteua watendaji wakuu wa wizara na taasisi za serikali.
Ni kipimo tosha kujua pumba na mchele. Kenya wameanza na mbinu fulani, nasi tunaweza ondokana na hili OMBWE. Kama Waziri analalamika uwezo duni, watendaji walioko kwenye halmashauri zetu ambao wengi uwezo ni duni (experienced ones) na watemi (walio na mtandao ambao hata ukiwaripoti hawafukuziki wala hawaambiliki) watakuwa na yepi?
Tupa jalalani kama ni bovu.
 
mwenyekiti wa kamati ya hesabu za serikali za mitaa amependekeza mawaziri wa tamisemi wajiuzulu nafasi zao kwa kushindwa kusimamia wizara hiyo.

hivi unafikiri hili litakuwa suluhu la tatizo?

Aliondolewa maige tukidhani kagasheki atakuwa suluhu lakini hakuna.

Aliondolewa ngeleja tukidhani muhongo atakuwa suluhu lakini ndio kwanza hari ni mbaya?

Kufukuza mawaziri si suluhu kabisa. Hivi kama pesa zinaibwa huko almashauri,hivi hao wabunge wetu wanakuwa wanafanya kazi gani kwenye vikao na madiwani.

Lazima tushughulikie mizizi ya matatizo haya kwani kabla ya hao mawaziri hayo matatizo yalikuwepo.
 
Sawa amejitetea lakini suala la msingi ni matatizo yaliyomo kwenye wizara yake anayoingoza. je, anathibtisha vipi uwezo wa kuyakabi kama waziri. majibu ya wabunge hayaondoi matatizo yaliyopo na suala la kuyaondoa au kuwajibika. mfano kama wanafunzi wanafeli halafu waziri anamuuliza afisa elimu kama walimu wanafundisha akiambiwa ndiyo tatizo la kufeli litakuwa limeondoka?
 
Ghasia nilisoma nae Mzumbe university mpaka leo sielewi alipenyaje hadi kupata hadhi ya kuingia baraza la mawaziri....empty set yule

Hukusema mengi ambayo tunayahitaji lakini kwa hayo machache, naweza kupata picha ya ubora wa mama huyu.
Hebu angalia utetezi wa kizembe ambao hauna mchango wowote wa kujenga hoja hapo chini. Ukiwa na wachangiaji wa aina hii ktk blog, hata siku moja hutabadili uelewa wako.

People are talking money,you are talking non sense

wewe unataka kujua alipenya vipi kwani wewe ndiye uliyekuwa unatunga mitihani ya mzumbe na kuteua mawaziri kwanza uko nje ya topic unaonekana kama unachuki binafsi na ghasia kuwa mtu mzima basi.
 
wekeni ushahidi wa tuhuma muwasaidie hao wanaosema hawajapata taarifa. Wengi wao ni wanachama humu watasoma tu !!!
 
Waziri anaye shughulikia wizara ya TAMISEMI amesema ameambiwa hana uwezo wa kuiongoza TAMISEMI kawni wizara hiyo inahitaji mtu makini mwenye weledi na nikubwa mno. Taarifa yake ilikuwa kama utetezi kwamba hasimamii utendaji wa halmashauri na hasa wakurugenzi wake. Amesema yeye anajitahidi kuwauliza wabunge kama halmashuri zao zina wakurugenzi mizigo,anasema wengi wa wabunge wamemwambia halmashauri zao zina wakurugenzi wazuri tu,sasa angechukueji hatua. Hii imekuwa kama kujibu mwito wa yeye pamoja na waziri Mkuu Pinda kufukuzwa kazi kwa utendaji usio ridhisha.Wabunge walisema Pinda na mama Ghasia hawatoshi kenye nafasi.
Hawa Ghasia na Pinda hawastahili sio wizara ya TAMISEMI tu bali hata Uenyekiti wa kijiji hawastahili. Cc: ritz, simiyu yetu
 
Ghasia nilisoma nae Mzumbe university mpaka leo sielewi alipenyaje hadi kupata hadhi ya kuingia baraza la mawaziri....empty set yule
Yule si alikuwa anafundisha primary na Salma. Nchi haiwezi kuongozwa na marafiki wa ikulu halafu tukaendelea hata siku moja. Never....
 
Back
Top Bottom