Hauwa Ali Mariri: Mwanamke aliyeolewa na wanaume wawili Nigeria

Nyendo

JF-Expert Member
Jun 4, 2017
1,189
4,103
Mgogoro mkali wa kimapenzi umeibuka katika jimbo la Kano nchini Nigeria ambapo wanaume wawili walimuoa mwanamke mmoja wakati tofauti.

Katikati ya mgogoro huo ni mwanamke kwa jina Hauwa Ali Mariri mwenye umri wa miaka 32 ambaye sasa anahofia adhabu iwapo atapatikana na hatia ya kuwadanganya wanaume hao.

Kano ni mojawapo ya majimbo kadhaa ya Nigeria ambayo yanaongozwa kupitia sheria ya Kiislamu na ni makosa kwa mwanamke kuolewa zaidi ya mwanamume mmoja.

Mambo yalibadilika na kuwa mabaya wakati Bello Ibrahim mwenye umri wa miaka 40, mume wa kwanza wa Mariri aliporudi nyumbani na kumpata mwanamume mwengine amelala katika kitanda chake.

Ibrahim alikuwa ameugua kwa muda mrefu na alikua amesafiri kijijini ili kupata matibabu ambapo alikaa huko kwa takriban miaka miwili.

Anamtuhumu Mariri kwa kufunga ndoa bila yeye kujua. Lakini aliambia BBC kwamba walitalakiana.

''Alisema kwamba ameniwacha kabla aende kijijini. Ndio maana nilifunga ndoa na Bala, nilihisi kwamba nilikuwa huru aliposema kwamba amenipa talaka'', alisema.

Hata hivyo Ibrahim amekana hilo akisema kwamba hakumpa talaka na kwamba bado anamchukulia kama mkewe.

Walioana kwa takirban miaka 17 na wakajipatia watoto sita.

''Sikumuwacha. Iwapo anasisitiza kwamba nilimpa talaka ushahidi uko wapi, barua niliomuandikia iko wapi?'',

Talaka nyingi nchini Nigeria hutolewa kwa mdomo ama kupitia barua.

Ibrahim aliyevunjika moyo aliwasilisha malalamishi yake kwa polisi wa jimbo hilo ambapo kisa hicho k inachunguzwa na wote watatu wamechunguzwa.

Bala Abdulsalam mwenye umri wa miaka 35 ,mwanamume wa pili katika hadithi hiyo, alisema kwamba Mariri alimwambia kwamba alikuwa amewachana na mumewe na kwamba alikuwa tayari kufunga naye ndoa.

Anasema kwamba alimtumia dola 50 za Marekani kusimamia ndoa hiyo pamoja na mahari.

''Nilikuwa nje ya mji wakati nilipomtumia fedha hizo, niliporudi Kano alikuwa mke wangu'', aliambia BBC.

Anahofia kuadhibiwa iwapo mahakama za sheria zitampata na hatia za kumuo mke wa mtu mwengine.

Uhusiano huo wa miaka miwili ulisababisha mtoto kuzaliwa na sasa Mariri ni mjamzito na mtoto wa pili.

Mariri ameondoka katika nyumba hiyo, akiwawacha nyuma watoto sita na Ibrahim, huku Bala akiambiwa na polisi kutoondoka Kano kwa kuwa wanaendelea kuchunguza kesi hiyo.

Gwani Murtala, Kamanda wa kituo cha polisi cha Kumbotso ambapo tukio hilo lilitokea aliambia BBC kwamba kesi hiyo ni ya kwanza kuwahi kufanyika na kwamba hakujua jinsi itakavyoisha
 
Miaka 32 ana watoto 6 na mume wa kwanza na tayari ana mtoto na mimba ya mume wa pili! Nimemkubali!
 
Back
Top Bottom