Hausigeli! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Hausigeli!

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Mbu, Feb 6, 2009.

 1. Mbu

  Mbu JF-Expert Member

  #1
  Feb 6, 2009
  Joined: Jan 11, 2007
  Messages: 12,729
  Likes Received: 187
  Trophy Points: 160
  ...hivi inakuwaje, mbona kina mama wengi wanawapelekesha puta sana hawa watumishi wa majumbani?

  ...utakuta matha-hausi wengine wanadiriki hata kuwalamba makofi hawa mabinti, na kashfa nyingi oooh, "ulipokuja hapa ulikuwa umepauka!" mara oooh, "...nipishe huko, usinitie shombo...!" nk nk...

  eti, nini tatizo?...

  hamuoni huruma hawa mabinti ni uwezo mdogo tu wa maisha ndio wakaamua kufanya kazi hizo? imagine; wao ndio wanaowapikia, kuwalelea watoto, kutunza nyumba mkiwa hampo,... mateso ya nini?
   
 2. Saikosisi

  Saikosisi JF-Expert Member

  #2
  Feb 6, 2009
  Joined: May 4, 2007
  Messages: 528
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Ndio ujue binadamu hatupendani. Kuwa m-mwenye nyumba ni kama kuwa kiongozi; watu kama hao ndio wakiwa wenyeviti wa vijiji wanawazaba vibao wananchi. Kuna akina mama/baba wazuri vilevile wanawa-treat h/g kama watoto wao.
   
 3. Pundamilia07

  Pundamilia07 JF-Expert Member

  #3
  Feb 6, 2009
  Joined: Oct 29, 2007
  Messages: 1,433
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  Hicho ndiyo moja ya vipimo halisi vya tabia ya binadamu. Ukimuona mtu ananyanyasa house maid wake basi huyo ndivyo alivyo kabisa na wala asikwambie kitu.

  Mtu mwenye tabia ya upendo wa kweli huwa nayo wakati wote wa maisha yake.

  Natoa wito kwa kuanzia kwa wanaJF tupinge unyanyasaji wa aina yeyote ile kwa hawa wanajamii wenzetu. Tuanze kwa kuangalia nyumba zetu je tunawatendea haki?
   
 4. Dark City

  Dark City JF-Expert Member

  #4
  Feb 6, 2009
  Joined: Oct 18, 2008
  Messages: 16,277
  Likes Received: 241
  Trophy Points: 160
  Kuna sababu nyingi, kubwa ni ile tabia yetu ya kuonesha ubabe na kutaka mtu ajue kuwa wewe ni mwajiri wake; na una nguvu kubwa/mamlaka makubwa sana juu yake. Kwamba ukiamua unaweza kuitoa hata roho yake, kwa hiyo akikuona akae mbali na wewe. Hii si kwamba watu hawajui kuwa wanamuhitaji sana huyo beki 3.

  Lakini kuna suala la akina mama kutaka beki 3 akae mashakani ili asije kumwibia. Kwa mwanamke kila mtu mwenye jinsia ya kike anayekaa karibu na mume wake ni hatari sana! Ndio maana akina mama wanawaogopa hata wifi zao!
   
 5. Nyamayao

  Nyamayao JF-Expert Member

  #5
  Feb 6, 2009
  Joined: Jan 22, 2009
  Messages: 6,980
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 0


  nampenda binti yangu wa kazi kama mdogo wangu, alikuja mdogo sana mpaka akaolewa na akaenda kijijini kuniletea mdogo wake ambaye nipo nae mpaka sasa, sema kweli wapo wasichana watulivu/wavumilivu sana na kuna wengine machakaramu hawashikiki, kuna wa rafiki yangu alikuwa na tabia ya kumchukua ka kijana wanakuja kulala nae ndani wakati mama/baba wapo kazini na mtoto ni mdogo, mara amfungie mtoto ndani akazurure huko mara katembea na baba mwenye nyumba, vurugu kabisa....
   
 6. Eeka Mangi

  Eeka Mangi JF-Expert Member

  #6
  Feb 6, 2009
  Joined: Jul 27, 2008
  Messages: 3,182
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 135
  Hi ni kumjenga hofu huyu GK3. Anajaribu kumweka mbali na amana zake ili asije akawa karibu na mzee. Maana ukweli ni kuwa ma-GK3 wakiaanza kupendeza huwa wanapendeza hasa. Mama akiona hivi du! Karoho kanamtoka ile mbaya,,,, anaanza kumpelekapeleka mtoto wa watu,,, na hasa kama mzee ana tabia ya ukipanga,,,, mama lazima awe macho sana na hawa mabinti. Ni mtizamo tu!!!!!!!!!!!!!!!
   
 7. Mbu

  Mbu JF-Expert Member

  #7
  Feb 6, 2009
  Joined: Jan 11, 2007
  Messages: 12,729
  Likes Received: 187
  Trophy Points: 160
  ...yaani hiyo familia haioni fahari kubadili maisha ya mtanzania mmoja akapendeza jamani? Mtanzania akifanya kazi ya uboi na uyaya kwa muhindi karaha, akifanya kwa mtanzania mwenzake dhahma,...waende wapi jamani? kwani kuna ubaya gani hausigeli akipendeza?

  ...naamini huo uvunjwaji wa maadili na kukiukwa heshima na tadhima ndani ya nyumba hiyo hakukuuanza hivi hivi tu, chanzo kilikuwa huyo huyo matha hausi... Kama binti anajua fika majukumu yake ndani ya nyumba, anafanyishwa kazi kwa masaa ya kibinaadamu, katika kila juma moja ana siku yake maalumu ya kutoka na kujifanyia mambo yake ya kibinaadamu, siamini angefikia jeuri ya kukimwagia kitumbua chake mchanga kama hivyo!
   
 8. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #8
  Feb 10, 2009
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,806
  Likes Received: 83,184
  Trophy Points: 280
  Ni roho mbaya na ukatili waliokuwa nao hao akina mama. Wengi wanawalalia sana hawa mabinti kwa visingizio mbali mbali inapokuja kwenye mishahara na labda wanadhani kuwatisha na kuwanyanyasa kunaweza kuwafanya wasiseme kuhusu kulaliwa huko.

  Kama binti hawezi kazi basi muachishe na siyo kumnyanyasa siku nzima kwa matusi, kejeli na wakati mwingine hata vipigo huko ni kukiuka haki za binadamu.
   
 9. Mbu

  Mbu JF-Expert Member

  #9
  Feb 10, 2009
  Joined: Jan 11, 2007
  Messages: 12,729
  Likes Received: 187
  Trophy Points: 160
  ...wengine wanaonikera ni mabosi ambao wanakwenda Bar na madereva wa magari ya ofisi, halafu wanakata kinywaji hukooo... dereva anaumwa na mbu tu ndani ya gari mpaka usiku wa manane, asubuhi ya kumi na mbili dereva awe nje anamsubiri na gari iwe ishakoshwa!

  ...Kuhusu ma hausigeli, angalau serikali imeingilia kati kwa 'wanaoishi kazini' mshahara uwe 25,000/=, na wale wanaokwenda na kurudi 75,000/= sasa sijui kweli wote wanalipwa hivyo au ndio akidai kamshahara analipwa kwa makofi, matusi na vitisho. Kina mama wengine...:(
   
 10. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #10
  Feb 11, 2009
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 33,572
  Likes Received: 5,761
  Trophy Points: 280
  tatizo moja la hawa mabinti ni moja

  tunawaseema wamaza lakini hawa wamekuwa nyoka nowdays,,zamani mtu unajitahidi kutuma hadi nauli akifika anaulizia hakuna wahehe jamani,wagogo,wachaga,wakijuana kosa!!!huyo si wako...akikunusuru kaondoka na TV,,kwa hiyo wengi wanafanya kazi kwa malengo yao binfsi wengine wamediriki hadi kuingilia ndoa zetu,,,he Babu hivihivi,,,,,
   
 11. Buswelu

  Buswelu JF-Expert Member

  #11
  Feb 11, 2009
  Joined: Aug 16, 2007
  Messages: 1,989
  Likes Received: 42
  Trophy Points: 145
  Nilitaka kushangaa...uko wapi kueleza ambacho unahisi ni kweli.Kikawaida...hata wamama,wadada uwaweke wawili kwenye nyumba si rahisi kuishi bila...vurugu na mwishoe wakashidana tena hapo kila mtu ana uwezo na kazi yake...Sijui kwanini wanawake japo si wote ku match hawawezi kabisa.Sebuse house akubaliane na mama mwenye nyumba si rahisi.
   
 12. M

  Mahmoud Qaasim JF-Expert Member

  #12
  Feb 11, 2009
  Joined: Nov 3, 2007
  Messages: 922
  Likes Received: 246
  Trophy Points: 60
  Tatizo limeanza kwenye tabia ya uvivu tulionao waTanzania wengi. si Hausigeli pekee hata maHausiboi pia wanapata mateso wanapokuwa bado hawajajazia mwili.
  nasema hili kwa sababu hawa "wasaidizi wa majumbani" wengi wetu tunawaona ni wafanyikazi za ndani badala ya wasaidizi sasa kazi zote tunawaachia wafanye wao na hatuwasaidii hata kuondosha kijiko kilichoanguka chini ya meza maadam kuna mfanyakazi basi ni kazi yake afanye kazi zote bila kusaidiwa, na ikitokea familia ambayo msaidizi anasaidiwa kazi basi kutokana na tabia hii ya uvivu wa kiTanzania basi naye anaanza kutegea kazi akitarajia kusaidiwa basi matatioz juu ya matatizo yanatokea chanzo UVIVU.
   
 13. Next Level

  Next Level JF-Expert Member

  #13
  Feb 11, 2009
  Joined: Nov 17, 2008
  Messages: 3,159
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  Mkuu malizia basi.....kwani mahouseboy waliyojazia wanamadhara tofauti na wasiojazia ndugu yangu.......!
   
 14. Kituko

  Kituko JF-Expert Member

  #14
  Feb 11, 2009
  Joined: Jan 12, 2009
  Messages: 9,366
  Likes Received: 7,008
  Trophy Points: 280
  mi nadhani hizi ndio zile zinaitwa ajira zisizo rasmi, kwamba hakuna chombo wala mahali pa kukimbilia kwa hawa house girls,hebu chukua mfano huu labda mtu na mkewe wanaenda kazini huku nyuma mmemwachia HG nyumba na mali zote lakini kikubwa ni watoto, sasa yeye ahakikishe wamekula, wameoga na kila kitu kipo safi nyumbani kuanzia asubuhi mpaka jioni, pamoja na hayo yote mama mwenye nyumba akirudi ni vibao tu, alafu akigeuka nyuma anadai usawa kwa wanawake.
  na hizi ajira ambazo zisizo rasmi ambazo mfanyakazi hana haki kwa Tanzania ni nyingi tu, angalia makonda na madereva wa daladala same case
   
 15. Bazazi

  Bazazi JF-Expert Member

  #15
  Feb 13, 2009
  Joined: Aug 18, 2008
  Messages: 2,030
  Likes Received: 564
  Trophy Points: 280
  Ni uwendawazimu wa kinamama na huku wakisahau kuwa uhai wa jamii (familia) yao umebebwa na huyo Hg na akiwa na roho mbaya au mazingira (ya kunyanyaswa) yanaweza kumfanya akafanya kitu mbaya sana. Je bado mnakumbuka mauaji ya mtoto mdogo pale Manzese? kisa ni deni la mshahara wa miezi sita (shilingi tisini elfu).

  Naomba mkubaliane nami kuwa wanawake wana upole wa nyoka kifutu.
   
 16. Scientist

  Scientist JF-Expert Member

  #16
  Feb 13, 2009
  Joined: Feb 7, 2009
  Messages: 392
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Kuna watu wanakaa vizuri tu na hawa watumishi wa nyumbani yaani wanawatunza km watoto wao/ndugu zao! Ila sio siri wapo ambao hata uwafanyie nini wataharibu tu ndio maana wengi wa waajiri huwa wanajaribu kuwa wakali (wanaume kwa mahouseboy/wanawake kwa mahousegirl). Wengi wameshahatarisha ndoa za watu mitaani.

  Ushauri: Akina mama msipende kuwa karibu sana na mahouseboy wanaume hupata wivu na pia akina baba kaa mbali na hausegirl vinginevyo mama ataua. Hii hutokea hata km wanaishi nae/nao vizuri kiasi gani!!!!
   
 17. MwanajamiiOne

  MwanajamiiOne Platinum Member

  #17
  Feb 13, 2009
  Joined: Jul 24, 2008
  Messages: 10,478
  Likes Received: 82
  Trophy Points: 145
  Ni kweli kabisa uhai wa nyumba yako uko mikononi mwa mtumishi wako wa kazi anaweza akakuua au akakunenepesha. Ewe mmama/mbaba unayemnyanyasa msaidizi wako wa ndani jua tu kuwa hutendi haki na pia malipo ni hapahapa duniani.
   
 18. Mbu

  Mbu JF-Expert Member

  #18
  Feb 17, 2009
  Joined: Jan 11, 2007
  Messages: 12,729
  Likes Received: 187
  Trophy Points: 160
  ...kuna nyumba unaweza kwenda ukajikuta unamsalimia hausigeli; "...hujambo shemeji!" maana kapendeza, mkarimu na mtanashati kuliko matha-hausi :D
   
 19. J

  Japhet Member

  #19
  Feb 17, 2009
  Joined: Jan 26, 2009
  Messages: 43
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Unyanyasaji huo wa wamaza unatokana na hofu za kuibiwa mahusband zao na ma GK3...lakni nadhani dhana kubwa ni ukosefu wa upeno tu..wamaza unakuta wengine wamepitia maisha ya shina na kunyanyaswa kabla ya kuolewa na kupata hifadhi kwa madingi..lakini maisha yao yakishakuwa supa wala hawakumbukia shida alizozipata....nomaaa
   
 20. ChaMtuMavi

  ChaMtuMavi JF-Expert Member

  #20
  Feb 17, 2009
  Joined: Oct 15, 2008
  Messages: 333
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Jamani, binadamu ndivyo tulivyo. Inategemeana mtu na tabia yake. Utakuta bosi mwenye roho nzuri basi mfanyakazi anataka awe yeye ndiye msemaji wa mwisho. Bosi akiwa chui basi mfanyakazi kaumia. Hiyo ina-apply kote tu. Lakini ndiyo yanayofanya dunia izunguke, Patamu hapo.

  Ni sawa na wanandoa, baba akiwa mpole mama anataka baba aoshe vyombo n.k. Mama akiwa mpole basi baba analeta mpaka mke wa pili na watatu, na wa nnee...

  That is a law of nature. Cha msingi binadamu tujielewe, usichotaka utendewe basi usimtendee mwenzako!!!Subiri Yesu arudi, hicho kipimo unachotumia kipimia wenzako basi hichohicho nawe utapimiwa.
   
Loading...