Hausigeli Azikata Kwa Kisu Nyeti za Mwarabu

kilimasera

JF-Expert Member
Dec 2, 2009
3,068
268
Mfanyakazi wa ndani toka Ethiopia aliyekuwa akinyanyaswa sana na bosi mwarabu wa Dubai, amelipiza kisasi kwa kuzikata kwa kisu na kuzinyofoa sehemu za siri za bosi wake.
Mwanamke raia wa Ethiopia aliyekuwa akitafuta riziki zake mjini Dubai kwa kufanya kazi za ndani, anashikiliwa na polisi baada ya kuzikata kwa kisu sehemu za siri za bosi wa kiume ambaye alikuwa akimnyanyasa sana,

Kwa mujibu wa gazeti la kila siku la Dubai la 7Days, msichana huyo aliamua kuzikata kwa kisu na kuzinyofoa kabisa sehemu za siri za bosi wake kama kisasi kwa mateso aliyokuwa akiyapata toka kwa bosi wake huyo.

"Polisi walimkuta mwanaume huyo akiwa amepoteza damu nyingi sana, mfanyakazi wake wa ndani aliukata kwa kisu uume wake", ilisema taarifa ya polisi wa Dubai.

"Mfanyakazi wake wa ndani alisema kuwa bosi wake alikuwa akimnyanyasa sana na siku ya tukio bosi wake alimtaka amfanyie masaji ambapo mfanyakazi huyo wa ndani alikasirika na kuamua kwenda jikoni kuchukua kisu, alimshambulia bosi wake na kisha kuzikata kwa kisu nyeti zake", ilisema taarifa ya polisi.

Mfanyakazi huyo wa ndani anashikiliwa na polisi kwa kosa la kufanya shambulio la kudhuru mwili wakati bosi wake amelazwa hospitali akipatiwa matibabu.

Haijajulikana wazi kama kipande cha nyeti zake kilichofolewa madaktari waliweza kukiunganisha tena au la.

Nchi za kiarabu zimekuwa zikikosolewa katika siku za karibuni na taasisi za kutetea haki za binadamu kutokana na matukio ya unyanyasi wa wafanyakazi wa ndani ambayo yamekuwa yakitokea mara kwa mara katika nchi hizo.
5601806.jpg
 
huyo amearibu angezila kabisa hawana adabu ..we unakata unaziachia zinarudishwa unameza kabisa wakapasue tumbo wazitoe
 
Back
Top Bottom