Haunted houses zipo, chukua hatua

Sijui why leo nipo kwenye mood ya kuongelea hii Topic , I hope itagusa watu na kuwasaidia kuchukua hatua. Mara nyingi tumekua tukiangalia Film’s za kutisha huko Hollywood kuhusu hizi haunted houses na mikasa ya kutisha kuhusu hizo nyumba zilizotawaliwa na ma roho /majini/ mapepo machafu. Na wengi wetu tumekua tukifikiria tu kuwa hizo ni hadithi na kamwe matukio kama hayo hayapo kwenye ulimwengu wetu.

Watu wengi wamejikuta wakipata mikosi kwenye maisha yao, nuksi kwa kuhamia , kupanga or kununua nyumba zilizofanyiwa mazindiko ya kishetani pasipo wao wenyewe kujua.

Unakuta mtu unapanga nyumba, ghafla mambo yako yanaanza kwenda hovyo, matatizo kazini, ndoa hakuna mawasiliano mazuri, mara ukiamka asubuhi unakuta umenyolewa nywele, mara unakua mvivu mvivu tu , biashara haiendi Sawa yani kila kitu kwako kinakua hovyo mwanzo mwisho , pesa zinakukimbia, marafiki hamna

Tuwe Makini sana na nyumba tunazohamia, Ni vizuri mtu kufanya spiritual cleansing before kuhamia kwenye nyumba za kupanga kila mtu kulingana na imani yake kama muislam, mkristo au mshirikina, kwa sababu hatujui hizo nyumba zimefanyiwa manuizi au matambiko na sisi bila kujua tunahamia tu , kwa vile nyumba iko masaki , mbezi beach tunaamini huko hakuna mambo ya kishirikina wakati wamiliki wengi wa hayo maeneo wanafuga majini kwa ajili ya kulinda mali zao , unajikuta mtu huna hili wala lile unahamia kwenye apartments hapo ndo unakua mwanzo wa mabalaa na nuksi katika maisha yako .
Tafuta pesa sheikh hakuna Cha mchawi Wala nini?hv umeishawahi kujiuliza kwanini mauza uza na zile Swaga za Yule mzee manyau huwa hazitokei Wala haIfanywi mikocheni,masaki,oyster bay,upanga?
Swaga na story za kichawi utazisikia Kawe,manzese,Tandale,buguruni,
 
Hauna knowledge ya kutosha kuhusu mambo ya Giza, hujui unachokiongea
 
Tafuta pesa sheikh hakuna Cha mchawi Wala nini?hv umeishawahi kujiuliza kwanini mauza uza na zile Swaga za Yule mzee manyau huwa hazitokei Wala haIfanywi mikocheni,masaki,oyster bay,upanga?
Swaga na story za kichawi utazisikia Kawe,manzese,Tandale,buguruni,
images-2.jpeg
images-1.jpeg

Lambertville High School
Hii ni shule ipo USA ilifungwa kutokana na mauzauza.

images-5.jpeg
images-4.jpeg

Yorktown Memorial Hospital ipo texas ulikuwa kama una tattoo ama umetoboa sehemu yeyote ya mwili wako ukiingioa humo hospital unakufa ukafungwa.

Tafta na hizi 👇👇👇
👉🏾ancient ram inn
👉🏾Wicklow Gaol
👉🏾chateau de chateaubriant

Sasa hapo jiulize kama kwa wazungu mwenye utajiri kuzidi hao wa masaki na oysterbay kuna haya mambo vipi kwa waafrika itakuweje?
Kama halijakufika ni bora unyamaze tu
 
Tafuta pesa sheikh hakuna Cha mchawi Wala nini?hv umeishawahi kujiuliza kwanini mauza uza na zile Swaga za Yule mzee manyau huwa hazitokei Wala haIfanywi mikocheni,masaki,oyster bay,upanga?
Swaga na story za kichawi utazisikia Kawe,manzese,Tandale,buguruni,
Kama hayajakukuta mkuu tulia, na omba Mungu yasikukute. Mimi nishakutana na haya mambo live. na huu ubishi wa kutokuamini ndo ulinifikisha huko
 
Labda kwasababu sijaelezea mazingira na muonekano wa hiyo nyumba ndio maana naonekana kama mzushi tu

Nyumba yenyewe kwa nje ya geti imezungukwa na vichaka hadi njia ya kuingilia haionekani, ndani ya geti ni vichaka vitupu, vioo vya madidirisha vilishapasuka yani kiufupi ni kama gofu.
Na Lulu yananunua kabisa
 
Kwa kuwa kuna binadamu na majini kwa baadhi tunavyoamini
Kweli majini wapo kila sehemu na tunaishi nao
Pia wengine wanaamini kuna mizimu na kama wazungu wanaamini kuna Nafsi zilizouliwa kwenye baadhi ya nyumba

Mimi binafsi kuna hotel nililala lakini cha ajabu nilikuwa naona kila wakati kama kuna kitu kinakatisha pembeni yangu ( kimvuli)
Sikushtuka sana kwani napenda sana kukutana na mambo kama hayo na nafsi hizo
Nilijaribu kuongea nae bila kupata jibu, nikalala zangu
Ila haya mambo yapo sana na nikipata fursa ya kupata haunted house ntaenda nikaone

Acha ufala Mkuu .. eti “Nilijaribu kuongea naye bila kupata jibu”.

Binafsi hapa ninapokaa sipaelewi elewi yaani.! Juzi juzi nilichelewa kulala, ilikuwa mida ya saa nane hivi ndio nikaenda kulala basi na pembeni kwangu nikaweka PC juu ya kistuli cha pembeni mwa kitanda.! Nilizima taa, na ule mwanga wa PC nikauelekeza kwangu nanikaupunguza kidogo. Lengo nikuwa naangalia kuna kitu nilikuwa nakipakuwa.
Nikajilaza ubavu ubavu nikaelekeza kichwa upande wa Ukutani. Sasa wakati nangojea kasingizi .. macho makavu mara nikaona kivuli kama mtu amevalia nguo kajifunika kichwa amekatiza mbele ya Pc na kivuli chake nikakiona huku ukutani. Sikugeuka haraka haraka, nikawa nimevunga kama sijaona chochote nikarudisha kichwa pole pole kuangalia sikuona chochote. Niligeuza pc ika face away. Nikaomba kimoyo moyo siku hiyo ikapita.
Na pia hii Nyumba nakaa sijui ina nini, ila Mungu naamini ananitumiaga walinzi, kuna wakati nahisi kabisa kuna vitu mle ndani. Kwa mfano, Kila ninapokuwa nataka kuingia ndani hata kabla sijagusa kitasa utasikia Mlango umejitikisa as if mtu ameusukuma alfu ukiwa umefungwa. Kuna muda huwa ikafanya hivyo natamkaga *Fucccccck * basi tu kujikaza na nimezoea tu sio siku moja mara kwa mara yaani.

Hizi Nyumba hizi mmh acha tu, ila kikubwa uzima. Kama unaamka salama hakuna shida nikumshukuru Mungu
 
Haya mambo yapo sana na tunaishi nao ila wapo wanaojali mambo yao ila kuna wengine wakorofi hawataki uishi nao

Hapo naona wamekuona huwa mind sana ila wape Hi kila wakati wanasikia ila wakikujibu usikimbie ndio madili hayo
 
Yalinikuta haya wakati nahamia kwangu, kila siku ya Mungu naota misiba huko nyumbani. Maisha yakawa magumu kupitiliza, pesa haikai mwisho wa siku wakaninyoa nywele pande mbili za kichwa. Nikaenda kunyoa zote. Zimeota tena kidogo wakaninyoa tena, ilibidi niende kwa wazazi kupumzisha akili yangu pamoja na kupata ushauri wa nini nifanye,.
Nilivyohamia kwangu kila usiku wadogo ni kuweweseka baadae ikahamia kwangu mandoto ya kula vyakula na "mzigo" na kuendesha gari usiku, asubuhi nakuwa mchovu hatari, nikaona isiwe tabu... Nikafanya mambo, baada ya siku kadha nasikia stori za kiwaki mtaani, nikajua mbaya anajitangaza
 
Mbaya Nipo nae jirani kabisa, na ndo huyu huyu aliniuzia eneo
 
Back
Top Bottom