Hauna Rafiki?, Kuna Marafiki wa Kukodisha Siku Hizi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Hauna Rafiki?, Kuna Marafiki wa Kukodisha Siku Hizi

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Dr. Chapa Kiuno, Sep 24, 2009.

 1. Dr. Chapa Kiuno

  Dr. Chapa Kiuno JF-Expert Member

  #1
  Sep 24, 2009
  Joined: Sep 11, 2009
  Messages: 445
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Thursday, September 24, 2009 5:36 AM
  Kama siku utaamua kutembelea Japan na hauna rafiki yoyote unayemjua nchini humo usitie shaka hata kidogo kwani kuna makampuni mengi yanayotoa marafiki feki wa kukodisha ambao unaweza ukatumia nao muda kwenye shughuli zako za kila siku.


  Kutokana na maisha ya kazi za Japan yanayowafanya watu wengi wawe wapweke, makampuni yanayotoa marafiki wa kukodisha nchini humo yameongezeka kwa kasi sana siku za karibuni.

  Kama unahitaji watu watakaojifanya kuwa marafiki zako wa karibu sana wakati unapopiga misele kwenye mitaa ya Japan basi usitie shaka kwani kuna makampuni mengi yapo yanatoa huduma ya kukodisha marafiki feki.

  Makampuni hayo yanatoa watu watakaojifanya marafiki au hata ndugu wa karibu kwenye misiba na hata sherehe za harusi.

  Ukitaka hata mtu wa kujifanya mume wako au mke wako usiwe na hofu kwani kampuni za marafiki feki zitakutatulia tatizo hilo.

  Kampuni ya kwanza ya marafiki feki ilianzishwa nchini humo miaka tisa iliyopita lakini hivi sasa kuna kampuni kubwa zaidi ya 10.

  Mojawapo ya kampuni hizo inayoitwa Hagemashi Tai ikiwa na maana ya "Nataka kukufurahisha" huwatoza wateja wake sawa na Tsh. laki mbili kwa rafiki mmoja feki wa kupiga naye misele.

  Kama unahitaji rafiki feki wa kujifanya rafiki wa karibu na kutoa hotuba ya kukusifia kwenye harusi yako basi kuna malipo ya ziada ambayo hutolewa.

  Mfumo wa maisha ya kisasa ndio unaosemekana kuchangia watu wengi kuwa wapweke na kuwa na marafiki wachache sana wanaowazunguka hivyo kuhitaji marafiki zaidi feki wa kupiga nao stori au kuwa karibu nao wakati wa sherehe au kwenye misiba.

  Hiroshi Mizutani, mmiliki wa kampuni ya marafiki feki ya Office Agents yenye wafanyakazi 1,000 alisema kwamba marafiki feki anaowakodisha kwa watu huwa wanavaa nadhifu na huonyesha furaha wakati wote kama vile watu wenye kazi bora duniani.

  Iwapo marafiki feki watahitajika kusimamia harusi basi hujifunza historia ya wanandoa mapema kabla ya kuhudhuria harusi.

  Wasanii wengi wa maigizo wamekuwa wakilichangamkia dili hilo la marafiki feki na makampuni mengi bado yanahitaji wasanii zaidi watakaoigiza kama marafiki feki katika maisha ya kweli ya kila siku.
  </SPAN>

   
 2. amu

  amu JF-Expert Member

  #2
  Nov 2, 2013
  Joined: Aug 8, 2012
  Messages: 7,979
  Likes Received: 157
  Trophy Points: 160
  huku bongo kuna kikundi cha kukodi kulia harusini,kuwaachanisha wapenzi na mkodombwe
   
 3. Wapoti

  Wapoti JF-Expert Member

  #3
  Nov 2, 2013
  Joined: Aug 28, 2013
  Messages: 2,824
  Likes Received: 417
  Trophy Points: 180
  Yaambie hayo makampuni yaje yawekeze Tanzania manake hawa marafiki wa hiari ni majanga bora wa kukodi hata akikugeuka utajua ni sawa tu
   
 4. M

  MOSSAD II JF-Expert Member

  #4
  Aug 24, 2014
  Joined: Apr 14, 2013
  Messages: 3,974
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 135
  akikugeuka unadai pesa zako!!
   
 5. Heart

  Heart JF-Expert Member

  #5
  Aug 24, 2014
  Joined: Nov 29, 2011
  Messages: 2,659
  Likes Received: 895
  Trophy Points: 280
  Hao mkodombwe ndo wakoje....?
   
 6. The Boss

  The Boss JF-Expert Member

  #6
  Aug 24, 2014
  Joined: Aug 18, 2009
  Messages: 37,826
  Likes Received: 22,465
  Trophy Points: 280
  sad life indeed...............
   
 7. j

  jokalakibisa Member

  #7
  Aug 24, 2014
  Joined: Aug 20, 2014
  Messages: 24
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  nikiwahitaji tutawacliana
   
 8. utafiti

  utafiti JF-Expert Member

  #8
  Aug 24, 2014
  Joined: Jul 18, 2013
  Messages: 12,831
  Likes Received: 92
  Trophy Points: 0
  Hiki kipindi kigumu sana tunavyoishi
   
 9. G bznes

  G bznes JF-Expert Member

  #9
  Aug 24, 2014
  Joined: Jul 19, 2014
  Messages: 648
  Likes Received: 210
  Trophy Points: 60
  Me nataka la wapenzi feki kw hapa tz linaweza likaeepo kwel?
   
 10. utafiti

  utafiti JF-Expert Member

  #10
  Aug 24, 2014
  Joined: Jul 18, 2013
  Messages: 12,831
  Likes Received: 92
  Trophy Points: 0
  Kinondoni, buguruni
   
 11. G bznes

  G bznes JF-Expert Member

  #11
  Aug 24, 2014
  Joined: Jul 19, 2014
  Messages: 648
  Likes Received: 210
  Trophy Points: 60
  Hapana siyo hao banna walioko kweny Kampun naenda nachukua halaf na signe
   
 12. NGUVUMOJA

  NGUVUMOJA JF-Expert Member

  #12
  Aug 24, 2014
  Joined: Jul 1, 2011
  Messages: 1,353
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  Ajira za kulazimisha hizo. Utakuwa na urafiki wa mshiko tu sio moyoni!!!
   
 13. kabanga

  kabanga JF-Expert Member

  #13
  Aug 25, 2014
  Joined: Dec 12, 2011
  Messages: 29,803
  Likes Received: 3,702
  Trophy Points: 280

  The Boss waonaje kaka tukafanya partnership katika Biashara hiyo....?
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 14. The Boss

  The Boss JF-Expert Member

  #14
  Aug 25, 2014
  Joined: Aug 18, 2009
  Messages: 37,826
  Likes Received: 22,465
  Trophy Points: 280
  how??............
   
 15. kabanga

  kabanga JF-Expert Member

  #15
  Aug 25, 2014
  Joined: Dec 12, 2011
  Messages: 29,803
  Likes Received: 3,702
  Trophy Points: 280
  kuanzisha kampuni katika Kutoa huduma ya marafiki, wakuajiri kibao mjini hapa...
   
 16. The Boss

  The Boss JF-Expert Member

  #16
  Aug 25, 2014
  Joined: Aug 18, 2009
  Messages: 37,826
  Likes Received: 22,465
  Trophy Points: 280
  utaweza kuigiza urafiki wa kulipwa? mimi marafiki wangu wa ukweli tu wanapata shida kunielewa..
   
 17. kabanga

  kabanga JF-Expert Member

  #17
  Aug 25, 2014
  Joined: Dec 12, 2011
  Messages: 29,803
  Likes Received: 3,702
  Trophy Points: 280
  Sasa ndio kazi, kazi yenyewe ya kuigiza na waigizaji wapi kibao mjini....
   
 18. M

  MOSSAD II JF-Expert Member

  #18
  Aug 25, 2014
  Joined: Apr 14, 2013
  Messages: 3,974
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 135
  hata hao marafiki ulionao kama hawakuelewi basi na wao ni waigizaji tu! they are fake!
   
Loading...