Thomas Laiser
Member
- Nov 9, 2016
- 64
- 124
Bila shaka ni wakati mzuri wa viongozi na watumishi wa umma kuujua ukweli kwamba ni vigumu kuzuia kusemwa. Tufanyapo jambo zuri watu watasema kwa uzuri wake na tufanyapo jambo ambalo sio sawa kwa mujibu wa mtazamo wa watu tutasemwa vibaya. Kamwe hatuwezi kuzuia kusemwa kwani mwanadamu hakuumbwa kunyamaza. Jaribio la Mkuu kuvikemea vyombo vya habari vinavyoandika tofauti na maoni yake haliwezi kufanikiwa. Dawa ni kutenda mambo SAHIHI ambayo wakijitokeza watu kulaumu wataonekana wajinga wakisutwa na dhamiri zao. Lakini tukifanya lisilopasa au lile tu tulionalo kuwa ni jema machoni petu pasipo kuzingatia uhalisia, watu wasema vibaya na watakuwa na haki ya kusema.