Hatuwezi kuwa na upinzani wa kweli kwa kuwa na utitiri wa vyama vingi vinavoshindwa hata kujipambanua kiitikadi. Vyama hivi vinadhoofisha upinzani

Jelavic

Senior Member
Dec 28, 2016
180
380
Ukifatilia kwa ukaribu vyama karibu tisa au kumi kati ya 15 vilivyotoa uwakilishi katika uchaguzi huu utagundua havikuwa na itikadi na muelekeo na nia thabiti ya kuongoza nchi, matokeo yake uchaguzi unaisha wote wanakuwa hawana tofauti na kina Waziri Jenister na kina waziri Kabudi wamekua wadogo mbele ya mshindani wao, wameonyesha udhaifu mkubwa sana, hata ukuu wa wilaya hawastahili.

Wengine wanaomba kazi hadharani kabisa, oooh mm bado kijana niko tayati kutumika, mpka unajiuliza au waliingia kwenye kinyang'anyiro ili wapate platform ya kuomba kazi kwa mh rais au vipi.

Hatujaona chama kikubwa kama Republican au Democratic baada ya uchaguzi wananyenyekea hivi kwa aliyeshinda, watu huwa wanatulia wanajipanga wanarudi tena kwa wananchi.

Uchanga wa vyama vyenu isiwe sabab ya kuua au kudhoofisha UPINZANI WA KWELI.
 
Halafu kuna raia wanapiga kura kwa Chauma,Sau,Tadea najiuliza ina maana hawaoni picha halisi ya siasa za Tanzania kwamba ni Chadema dhidi ya C CM? kwanini wanapoteza kura zao
 
Vyama ni Chadema na ACT wengine ni mapandikizi ya CCM
Chama cha upinzani hapa Tanzania ni Chadema tu,hiyo ACT ilikuwa inasemwa ni ya Kikwete na Membe. Chadema ishavituhumu vyama vyote hivyo kuwa vinatumika tu na serikali kwahiyo utaona Chadema tu ndio yenyewe inajiona ni upinzani halisi.
 
Halafu kuna raia wanapiga kura kwa Chauma,Sau,Tadea najiuliza ina maana hawaoni picha halisi ya siasa za Tanzania kwamba ni Chadema dhidi ya C CM? kwanini wanapoteza kura zao
Ndio ujue huko mtaani kuna watu hawamuelewi huyo Magufuli wala Lissu,na usikute wamepiga kura zao huko kwa kuona ni bora kupeleka kura zao huko kuliko kuwapa hao wawili yani Lissu na Magu.
 
Ndio ujue huko mtaani kuna watu hawamuelewi huyo Magufuli wala Lissu,na usikute wamekapiga kura zao huko kwa kuona ni bora kupeleka kura zao huko kuliko kuwapa hao wawili yani Lissu na Magu.
Hao raia ndio wanaochangia nchi kupata viongozi wabovu, Tume nayo uchaguzi ukimalizika wanajifungia ofisini tu, Wakati wangetakiwa kuendelea kutoa elimu kwa raia kuhusu umuhimu wa kuchagua viongozi na kuhakikisha kura zao hazipotei, Lakini utawasikia tu wakati wa uchaguzi utafikiri ni watu wapya kumbe ni wale wale wa kila awamu
 
Ukifatilia kwa ukaribu vyama karibu tisa au kumi kati ya 15 vilivyotoa uwakilishi katika uchaguzi huu utagundua havikuwa na itikadi na muelekeo na nia thabiti ya kuongoza nchi, matokeo yake uchaguzi unaisha wote wanakuwa hawana tofauti na kina Waziri Jenister na kina waziri Kabudi wamekua wadogo mbele ya mshindani wao, wameonyesha udhaifu mkubwa sana, hata ukuu wa wilaya hawastahili.

Wengine wanaomba kazi hadharani kabisa, oooh mm bado kijana niko tayati kutumika, mpka unajiuliza au waliingia kwenye kinyang'anyiro ili wapate platform ya kuomba kazi kwa mh rais au vipi.

Hatujaona chama kikubwa kama Republican au Democratic baada ya uchaguzi wananyenyekea hivi kwa aliyeshinda, watu huwa wanatulia wanajipanga wanarudi tena kwa wananchi.

Uchanga wa vyama vyenu isiwe sabab ya kuua au kudhoofisha UPINZANI WA KWELI.
Walaumu chadema hao hao, kujifanya wababe! Walimfukuza zito akaanzisha act, 2015 ukawa ikawabeba wakajiona vidume, ruzuku wakala peke yao wakawasahau cuf, nccr na nld! Waache ubinafsi kwanza na kugeuza chama Sacco's! RIP chacha wangwe!
 
Hao raia ndio wanaochangia nchi kupata viongozi wabovu, Tume nayo uchaguzi ukimalizika wanajifungia ofisini tu, Wakati wangetakiwa kuendelea kutoa elimu kwa raia kuhusu umuhimu wa kuchagua viongozi na kuhakikisha kura zao hazipotei, Lakini utawasikia tu wakati wa uchaguzi utafikiri ni watu wapya kumbe ni wale wale wa kila awamu
Na ndio maana kila mtu akawa na haki ya kuchagua kiongozi aonae yeye kuwa ndio anafaa,sasa wengi tunakosea kwa kudhani kuwa viongozi wazuri ni kutoka katika vyama vikubwa tu yani Ccm na Chadema tu basi.
Sasa raia kaangalia mwenyewe kaona hao wagombea wa vyama vikubwa wote hawafai sasa hawezi akaamua kuwapigia tu hao wakati yeye anaona hawafai hivyo kwake yeye atakuwa anachangia kuweka viongozi anaoamini si sahihi.
 
Mkuu watu walishaamka.
i). Je, kadri demokrasia ya vyama vingi inavyozidi kuenea mataifa mbalimbali ni nani anayenufaika?
ii). Je, kwakumjua mnufaika huoni unaikanyaga ardhi yako kupigania maslahi ya taifa la wenzio?
iii). Je, kwakuujua werevu utajilazimisha kuendelea kuufanya ujinga?

MAGUFULI4LIFE.
 
MAGUFULI4LIFE
 
Hao raia ndio wanaochangia nchi kupata viongozi wabovu, Tume nayo uchaguzi ukimalizika wanajifungia ofisini tu, Wakati wangetakiwa kuendelea kutoa elimu kwa raia kuhusu umuhimu wa kuchagua viongozi na kuhakikisha kura zao hazipotei, Lakini utawasikia tu wakati wa uchaguzi utafikiri ni watu wapya kumbe ni wale wale wa kila awamu
Mkuu unazungumzia tume gani
 
4 Reactions
Reply
Back
Top Bottom