Hatuwezi Kuwa na Muundo wa Kudumu wa Baraza la Mawaziri?

Nungunungu

JF-Expert Member
Feb 13, 2007
311
13
Invyoelekea ni kuwa Baraza letu la mawaziri litakuwa linachukua sura ya Raisi aliyepo madarakani.

Hivi hatuwezi kuwa na muundo wa kudumu wa baraza letu? Kama ndivyo chombo kipi kinastahili kusimamia jambo hilo, Bunge?

Nionavyo kuna haja ya kuwa na mjadala na maafikiano juu ya idadi na muundo wa wizara tunazopaswa kuwa nazo kulingana na mahitaji ya Taifa letu.

Siamini kama kuna watu wachache wanaweza kulifanya hilo ndani ya siku mbili-tatu na kutoa muundo unaokidhi mahitaji ya nchi.

Naomba kama kuna uwezekano basi tulisemee jambo hili ili kusiwe na mabadiliko ya mara kwa mara yasiyo na Ulazima.

JK kabadlisha mmundo ndani ya miaka miwili na kidogo. Tujitahidi kusisitiza mchakato wa hili ili Rais ajae 2010 ateue baraza kwa msingi huo.

Nawasilisha.
 
wazo lako ni zuri ila sio jipya! mjadala huu umeshaanza na unaendelea! john mnyika ameanza kwa kutaja ni vipi yeye anadhani baraza lina takiwa liwe na wengine wakaendeleza pale! nadhani ni vizuri na wewe ukienda kushiriki kwenye mjadala huko
 
Nafikiri swali la ku specify na kufix wizara zitakazokuwepo katika serikali linawezekana kabisa. Katiba ya nchi inaweza ku-specify idara/wizara zitakazo kuwepo. Nielewavyo mimi USA wizara/idara zao zilikuwa specified kwenye katiba au annexes za katiba na ni lazima kama kuna haja ya kuanzisha idara mpya basi inabidi Congress na ninafikiri all the states kuafiki pendekezo hilo kwa ku-ammend hiyo annex. Katika miaka arubaini iliyopita nafikiri hili limetokea mara mbili (1) wakati wa kuanzisha Department of Energy in 1975 baada ya Energy crisis ya 1973 na(2) wakati wa kuanzisha Dept. Homeland Security in 2002 baada ya 9/11. Kwa hiyo unahitaji emergency ya hali ya juu kabisa kwa USA kubadili au kuanzisha idara mpya yenye cabinet level authority.

Naamini kabisa Tanzania tumezidi kwa jinsi tunavyo badili wizara na mandates zake. Sasa hivi wati is kilimo in the USA & European sense[handled in one Ministry] is handled in seven ministries in Tanzania [i.e. Kilimo; Mifugo; Mali ya Asili; Maji[irrigation]; Viwanda na Masoko[Marketing]; Tamisemi [Extension Services at regional and District levels]; Infrastructure [rural roads and strctures]. Whether we need all these miminstries is nopt that clear to me.

Kudi Shauri
 
Mkuu NN,

Tatizo letu bongo, ni more than muundo wa kudumu, tatizo ni viongozi ambao ni competent kuwa mawaziri, Tanzania tumeushusha sana hadhi uwaziri.
 
ANGALIENI MBELE.. THE country's constituitional order has to allow adequate flexibility kufacilitate any required changes.. Matatizo ya nchi ni dynamic... Kuna mambo yale core lakini kuna uwezekano ikajitokeza hali itakayo hitaji Rais aunde wizara, ofisi ama tume yoyote ya mda mfupi ama yakudumu. Kinachotakiwa tu ni viongozi waache kutunga wizara zisizohitajika kwaajili yakuwapa washkaji zao nafasi. Tanzania tuna safari ndefu sana mpaka kuendelea kiufanisi, kwanza tatizo kuu la serikali, and \i dnt mean the political top tuu.... nikwamba watumishi wa serikali and thus wananchi ni waTUMIKIWA.. wana mentality yakutaka kunyenyekewa na wananchi.. Kinyume na inavyotakiwa kuwa. Kubadili mawaziri sio ishu, hakuna cha Zitto, wala Slaa, wala JK.. wote wanapenda utukufu. Africa tunaendekeza ujinga waku idolize viongozi wetu. Kwa mfano Kanisa Katoliki in the most ridiculous thing i have heard in a while, wanataka kumpa utakatifu mtu ambaye anajulikana kuwa alikua mchawi and everyone knows it, alifanya political assassinations lakini eti SAINT. Tuacheni ujinga wakuabudu viongozi... tuwaagize chakufanya, tuwachague kwa merits na tu wawajibishe kwa maamuzi yao... The notion of 'Mtukufu Rais' is still ripe in our minds... 2wafundishe watoto wetu kuwa na uhuru wa mawazo. Wasitumike bali wawe na uhuru wa fikra na hoja za maendeleo. Curriculum ya shule inahitaji kutazamwa upya.!!
 
Back
Top Bottom