Hatuwezi kuuza nchi yetu vipande vipande kwa wageni

Mathayo Fungo

JF-Expert Member
Nov 13, 2018
299
500
Imeandikwa na Felician Andrew
Chuo Kikuu Mzumbe, Morogoro“Kuna watu wamechukulia mikopo mikubwa ya fedha kwenye mabenki ya ulaya huku dhamana zikiwa ni ardhi ya Tanzania hivyo wakishindwa kurejesha mikopo hiyo maana yake ardhi yetu itakuwa ni mali za mabenki hayo ya ughaibuni”

Nimeamua kuanza na nukuu hiyo ili uone mahala ambapo nchi yetu imefika kiwango ambacho watu wachache wenye uwezo wa kifedha wanaweza wakaweka rehani ardhi ambayo mababu zetu na wapigania uhuru walimwaga damu zao ili leo hii iweze kuwanufaisha watanzania wote. Ukaribu kabisa wa jambo hili linafanana na mkataba wenye masharti ya kinyonyaji ambao kampuni ya kibepari ya China Merchants Port Holdings Company Limited yenye Makao yake makuu Hong Kong inataka Tanzania kuingia mtego na mwisho kujimilikisha ardhi na mali za taifa hili kwa muda mrefu.

Historia inaonyesha ya kuwa mjerumani Karl Peters maarufu kama Mkono wa Damu akiwa na umri wa miaka 28 katika mwaka 1884 alisafiri kutoka Ujerumani akijifanya fundi makenikia (Machenical Engineer )hadi kufika Zanzibar na baadae kuingia bara katika mwaka huo huo. Walifika Saadani mkaoni Tanga wakasafiri tena hadi Uzigua ambako hapo ndio walimsainicha Chifu Mbwela wa Uzigua mkataba wa kwanza na kila walikopita waliwasainisha machifu mikataba ya ulaghai iliyokuw an alengo la kuina ardhi kutoka mikononi mwa wazawa na kwenda chini ya himaya ya ujerumani.

Mkataba maarufu unaotajwa sana ni ule wa Chifu Mangungo wa Msovero na Karl Peters uliofanywa Novemba 1884, sehemu ndogo ya mkataba huu ilisema ya kuwa….
“Mangungo offers all his territory with all its civil appurtenances to Dr. Karl Peters, as the representative of the Society for German Colonization, for the exclusive and universal utilization for German colonization.” Kwa tafisiri rahisi ya Kiswahili ilimaanisha ya kuwa “Mangungo amekubali kutoa himaya yake yote pamoja na watu wake na hadhi yake kwa Dk. Karl Peters, kama mwakilishi wa Umoja wa Ukoloni wa Kijerumani (Society for German Colonization), kwa ajili ya matumizi ya moja kwa moja ya koloni la Kijerumani.”

Sehemu kubwa ya wizi na uporaji wa haki ya watu hawa waliokuwa chini ya Mangungo ulifanywa na aliyekuwa mkalimani aliyejulikana kwa jina la Ramzan ambaye kwa sehemu kubwa alimpotosha Mangungo mpaka kuingia kwenye Maktaba huu wa ulaghai na mwisho kkujikuta wamegawa kwa wajerumani sehemu yote ya ardhi pamoja na watu wao.

KISA CHA MANGUNGO NA BANDARI YA BAGAMOYO
Mwaka 2015 serikali ya Tanzania chini ya Rais wa awamu ya nne Jakaya Kikwete iliingia makaubaliano ya ujenzi wa bandari ya Bagamoyo ambayo ilikuwa inagharimu zaidi ya shilingi za kitanzania trlliioni 22. Kwa mujibu wa makubaliano ya Mradi huu kampuni ya China Merchants Port Holdings Company Limited iliyoanzishwa mwaka 1997 ndio ilikuwa na jukumu la ujenzi huku fedha nyingine zikiwa ni ushirikiano baina ya serikali ya Oman na Tanzania.

Mradi huu ambao kwa muonekano wa kibiashara ni mzuri na wenye faida nyingi lakini ndani yake ulijaa masharti magumu ambayo yangepelekea mpaka kukamilika kwa ujenzi wake basi Tanzania isingekuwa na uwezo wa kulipa deni hilo na mwisho bandari hiyo kurudi tena mikononi mwa kampuni hii kubwa ya China ambayo imekuwa ikifanya michezo hii kwa mataifa mengi duniani.

Masharti yaliyomo kwenye mkataba au makubaliano haya yanailazimisha serikali ya Tanzania kuwa tayari kuachia bandari kuendeshwa na wachina kwa muda wa miaka 33 hadi 99 mpaka pale kampuni hoiyo itakapokuwa imerudisha fedha zake; mtego huu ndio sababu ya watanzania wote tuatakiwa kusimama na kumuunga mkono Rais Magufuli kwani kama serikali ingekubali mradi huu kutekeelzeka kwa matakwa ya kampunii hii basi sehemu yote ya Bandari hiyo ingekuwa chini ya umiliki wa Kampuni hii ya China kwa muda mrefu mpaka miaka 99.

Huu ni mfano tosha wa mkataba wa Uchimbaji wa gesi kule mkoani Mtwara ambapo katika mkataba sehemu ya gesi iliyokuwa inachimbwa ilitakiwa kusafirishwa kwenda nchini China.

Serikali ya Tanzania chini ya Rais Magufuli kukataa masharti ya kinyonyaji yaliyomo ndani ya mikataba hii ya makampuni makubwa kunamfanya Rais Magufuli kuishi maneno ya Mwalimu Nyerere baada ya kukataa makampuni ya kinyonyaji kuchimba madini na kusema tutachimba madini siku tukiwa tayari tukiwa na vizazi vyenye uwezo wa kusimamia madini yao na tukiwa na wataalamu wakutosha kuongoza sekta hiyo ya madini nchini. Hata sasa Rais Magufuli amehakikisha jambo hili halifanyiki kwani kama angekubali basi taifa linhekuwa limeingia katika mtego wa kuingia kwenye mkataba wa ulaghai.


Kisa cha Djibout na Kampuni ya China Merchants Port Holdings Company Limited
Hadi kufikia Februari 2019, nchi ya Djibout iliiingia kwenye mgogoro mkubwa wa umiliki wa Bandari iliyojengwa na kampuni hili kubwa ya kichina ambayo ilipelekea nchi ya Djibout kukosa uhalali wa umiliki wa bandari yao ambayo ndio bandari kubwa kabisa katika rasi ya afria Mashariki.

Kupitia mikataba hii ya kilaghai viongozi wa taifa la Djibout wamejikuta sasa wana deni kubwa ambalo ni sawa na asilimia 44 ya Mapato ya taifa hilo yaani GDP fedha ambayo inaifanya basnari hiyo kuw achini ya umiliki wa ampuni hii yakichina kwa muda wa miaka 30 huku kampuni hiyo ikiw ana uwezo wa kujenga tena na kupanua au kufanya biashara kwenye badnari hiyo kadriwatakavyo bila kuingiliwa na nchi ya Djibout. UNaweza ukashangaa mambo haya yanafanyikaje katika dunia ya leo ila huu ni mfano halisi wa mikataba ya ulaghai ambayo nchi masikini au zinazoendelea zimekuwa zikiingia mkenge kwenye kampuni hili kubwa la China.

Kisa cha Bandari ya Sri lanka na Kampuni ya China Merchants Port Holdings Company Limited
Mwaka 2017 serikali ya Sri Lanka iliingai makubalinao na kampuni hii kwa ajili ya ujenzi wa Bandari iliyojulikana kama Hambantota Port huku makubaliano yakiwa yanahusisha utaoji wa mkopo wa dola za kimarekani bilioni 1.2 kwa mkataba wa miaka 99 huku kampuni hiyo ikiwa inachukua asilimia 85 ya umiliki wa Bandar na eneo la zaidi ya hekari 15000.

Kutokana na uharaka wa viongozi wa Sri Lanka na kwa kuwa walikuwa wakielekea kwenye uchaguzi wakajikuta wanaingia makubaliano yale na kusaini kuuza ardhi na bandari yao kwa kampuni hii ya kichina kwa muda wa miaka 99 kutokana na deni hilo kukua kwa kasi kulinganisha na uwezo wa taifa hilo kulipa deni hilo kubwa.

Ni mikataba kama hii ndiyo imeifanya leo nchi jirani ya Zambia kuwa katika hatari kubwa ya kuporwa Shirika lake la Umeme (ZESCO), Shirika la Utangazaji Zambia (ZNBC) pamoja na Airpot ya Keneth Kaunda ili kufidia deni ambalo lilikopwa na serikali ya Zmabi kutoka China

Nchi ya Angola imepata pia pigo kama hilo baada yakushindwa kulipa deni lae na kujikuta ikitakiwa kutoa sehemu kubwa ya mafuta yanayozalishwa nchini humo kupelekwa China kama sehemu ya kupunguza deni ambalo wanadaiwa na makampuni ya fedha ya nchini China ikiwemo EXIM BANK CHINA, Benki ya Viwanda na Biashara ya China na Beki ya Maendeleo ya China yenye thamani ya dola za marekani bilioni 14.5 na jambo hili sasa linaifanya China kuwa taifa la pili kwa usambazaji wa mafuta duniani nyuma ya Saudi Arabia.

Yako mataifa mengi ambayo yameingia katika mikataba hii ya ulaghai na kampuni hii kubwa ya ujenzi wa Bandari kutokea China ambayo ni moja katik ya makampuni makubwa duniani yenye uwezo mkubwa wa kifedha huku India ikiwa ni moja kati ya mataifa ya mfano duniani kukataa ofa kama ile waliyopewa Sri Lanka ya ujenzi wa bandari.

Mwisho:
Rais Magufuli kwa niaba ya watanzania wote ameweka mbele maslahi ya nchi hii na muda wote amesimamia maslahi ya nchi yetu kwa kupigania na kuwapinga wanyonyaji hadharani. Uhuru wa nchi yetu na rasilimali zake lazima ulindwe kwa gharam zote kwani ni jambo la aibu kuingia makubaliano ambayo mwekezaji atakuwa mamlaka makubwa ya kiwango ambacho ndiye atakua mmiliki wa bandari na atakuwa mwenye mamlaka ya kupnaga kiwango cha tozo badnarini, atakuwa na mamlka ya kukusnya tozo za bandarini na kuusimamia mradi bila kuingiliwa na mtu yeyote mpaka hapo atakapokuwa amerejesha gaharama zake. Mikataba ya hivi ni mikataba ya kikoloni yenye lengo ya kuzirudisha nyuma nchi za kiafrika katika zama za ukoloni.

Kwa mantiki hii tuwakatae wanasiasa wote wanaotumika na makampuni haya makubwa ili kushinikiza utekelezaji wa miradi hii ya kinyonyaji nchini na kujikuta tunaingia kweny emitego kama ambayo nchi nyingine duniani na afrika zimeishaingia.

Tanzania ni moja, na Hakuna Tanzania nyingine hivyo miradi yote na mambo yote lazima yazingatie maslahi mpana ya taifa letu kama ambavyo amefanya Rais Magufuli.
Nasimama na Rais Magufuli, Nachagua kuwa Mzalendo.
 

Salary Slip

JF-Expert Member
Apr 3, 2012
39,343
2,000
Usiri wa mikaba bado unaendelea hivyo hakuna la maana tunalo-achieve hapa.

Nitajieni mkataba hata mmoja wa hii serikali na wawekezaji uliowekwa wazi kwa umma.

Kama hakuna,wewe unaesifia hii serikali hujui unalosimamia na huenda tu unajipendekeza upate uteuzi.

Tuache unafiki!
 

Shingamagadi

Member
Jul 12, 2018
37
125
Usiri wa mikaba bado unaendelea hivyo hakuna la maana tunalo-achieve hapa.

Nitajieni mkataba hata mmoja wa hii serikali na wawekezaji uliowekwa wazi kwa umma.

Kama hakuna,wewe unaesifia hii serikali hujui unalosimamia na huenda tu unajipendekeza upate uteuzi.

Tuache unafiki!
Bwana mkubwa unaroho ngumu kweli, ungeendelezwa pia mngejificha kwenye upande wa changamoto za ubaya wa mkataba huu. Hii mikataba mbona wanaharakati walioko bungeni wanayo ila hawataki kabisa kuweka jicho upande huu wa masharti maana utawapunguzia cha kusema.
 

mkma

Senior Member
Feb 27, 2018
125
250
Usiri wa mikaba bado unaendelea hivyo hakuna la maana tunalo-achieve hapa.

Nitajieni mkataba hata mmoja wa hii serikali na wawekezaji uliowekwa wazi kwa umma.

Kama hakuna,wewe unaesifia hii serikali hujui unalosimamia na huenda tu unajipendekeza upate uteuzi.

Tuache unafiki!
WEWE MKATABA HUO PIA HAUJAUSOMA

SWALI NI:-KAMA HATA WEWE MKATABA HAUJASOMA PAMOJA NA MFALME WAKO ZITTO KWA NINI SASA MNAIPINGA SERIKALI KWA ILICHOKIFANYA KANA KWAMBA UMEUONA KUWA UKO SAWA???

WEWE HAUJASOMA MKATABA.. LKN UNAIPINGA SERIKALI TENA KWA MATUSI NA KEJELI

WAKATI HUOHUO HUYU ANAUNGA MKONO SERIKALI ILICHOKIFANYA NDIPO UNAINUKA KUWA ANAUNGA MKONO BILA KUUSOMA MKATABA!!!!

JIONE ULIVYO BOYAAA!!!!
UNAYEKULA MATAPISHI YOTE ANAYOTAPIKA MFALME WAKO ZITTO

Kwa mtu muelewa ungekuwa Katikati.. Bila kuitukana serikali wala Kumuunga Mkono Zitto HUKU UKISISITIZA MKATABA UWEKWE WAZI KILA MMOJA AUSOME

NA ILI HILO LIFANIKIWE MAANA YAKE SERIKALI IPELEKE MSWADA BUNGENI KUBADILI USIRI WA MIKATABA KAMA HII KUWEKWA WAZI NA KUPITIWA NA KUJADILIWA NA BUNGE KWA NIABA YA WANANCHI

LKN KWA KUWA WEWE NI MPINGA KILA IFANYACHO SERIKALI L..
UNAJIONA KUWA NA HAKI YA KUITUKANA SERIKALI KUKOSEA KUSITISHA MKATABA HUO KANA KWAMBA UMEUOSOMA!!!

WAKATI HUO UKIMTUKANA KILA MTU ANAYEUNGA MKONO SERIKALI KUUSITISHA HUKU KIGEZO CHAKO CHA KUPINGA NA KUTUKANA KIKIWA MKATABA HAUJULIKANI!!!

ACHENI UKICHAA NA UMAVI!!!!!
Komaeni Kifikra na UJITEGEMEE KATIKA KUFANYA MWAMUZI
 

Man in the Middle

Senior Member
Feb 26, 2019
126
250
Usiri wa mikaba bado unaendelea hivyo hakuna la maana tunalo-achieve hapa.

Nitajieni mkataba hata mmoja wa hii serikali na wawekezaji uliowekwa wazi kwa umma.

Kama hakuna,wewe unaesifia hii serikali hujui unalosimamia na huenda tu unajipendekeza upate uteuzi.

Tuache unafiki!
very good, hv kwann kusiwe na utaratibu wa mikataba kupitia bungeni kujadiliw kabla ya kusign
 

mtzedi

JF-Expert Member
Dec 13, 2011
3,591
2,000
Kama tuna nia ya dhati ya kuilinda na kuijenga Tanzania kwa manufaa ya leo na kesho,waliosaini iyo mikataba wakamatwe wafikishwe mahakamani.
Yote yanayoendelea sasa ni matokeo ya kusainiwa kwa mikataba.
 

Alvajumaa

JF-Expert Member
Jul 5, 2018
3,182
2,000
Mwandishi ni Felician Andrew Kitole, zao la Azaboi 2005/08 -2009/11
Sema bado kwenye maada kuna vitu vimekosekana.....
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom