love life live life
JF-Expert Member
- Sep 12, 2021
- 2,529
- 2,896
Sikuelewi hayo makosa Magufuli aliyafanyia wapi mpaka kila siku mkumbushe watu kuwa alikosa sana.Makosa ya utawala wa awamu ya 5 yatamkwe kwa lengo la kujua maeneo ya kurekebisha, na siyo kuhukumu. Marehemu hahukumiwi.
Mijadala inakuwa mingi na mirefu kwa sababu ni dhahiri kuna makosa mengi yalifanyika wakati wa awamu ya 5 yanayotakiwa kurekebishwa, lakini kuna watu wanataka kuonesha kuwa hakuna kosa lolote lililofanyika wakati wa awamu ya 5. Hawa wanaona awamu ya 5 ulikuwa utawala mtakatifu. Hawa hawana maana wala hoja, na ndio wanaofanya jina la marehemu litajwe mara kwa mara na hata kuhukumiwa na kukejeliwa. Watu kama walikuwa wamepumbazwa au kufitishwa akili, sasa warudi kwenye akili zao. Wajadili kwa kutumia akili zao kuliko kukaa na fikra kuwa Marehemu Magufuli kila alichofanya kilikuwa sahihi au kilikuwa kibaya.
Makosa gani ambayo wewe unayajua ambayo mtanzania mwingine hayajui mpaka mijadala ya kurudia rudia
kila uchao.
Kama makosa yapo basi ni bayana haina haja ya threads 1000 ku-prove ubaya wake.
Hamhangaiki kujadili makosa yake bali kuprove ubaye wake na mara zote mmeshindwa.
Fact moja inatosha kuprove ubaya wake na sio idadi ya watesi wake.