Hatuwezi kutatua matatizo yetu kwa kujidanganya kuwa hayapo- Mwalimu J. K Nyerere

Bujibuji Simba Nyamaume

JF-Expert Member
Feb 4, 2009
75,203
157,369
16105969_10206208729456660_8389378104875528706_n.jpg

Hali ya ukame tunaiona.
Mvua za vuli hazijanyesha, Rais wetu mpendwa anasema hakuna ukame.
Najiuliza sana, sijui ni ukame gani anaoungelea?
Sijui ni ule ukame wa mabao kwenye mechi ya Simba na Yanga hadi wakaenda kwenye matuta?
Yaani sipati jibu kamili kwa kweli.
 
kwa hiyo unataka kumlazimisha naye auone UKAME!, Hataki sas! amekataa ye hauoni ukame, kwa lazima kumlazimisha!? unajua mshahara wake kwa mwezi? marupurupu? !0%?... halafu unamng,ang,aniza eti aone ukame, HATAKI!
 
Hakujiandaa kuongoza nchi ndo maana anashindwa kuelewa jinsi yakunena yaliyo mema taifa linapokuwa ktk dilemma na haya ndo matatizo ya watu waliookota dodo chini ya m'buyu..unashindwa kuelewa mtu anakataa vipi hakuna ukame ilhal hata zilipo office zake kuu kuna ukame mvua hazijanyesha.
 
Na pia hatuwezi kutatua matatizo yetu bila kuwaambia wananchi ukweli hata kama ukweli huo unaumiza.
 
Mkuu hataki kusikia uwepo wa NJAA yeye anachojua ni kazi tu wakati wakulima hawana pa kufanyia hiyo kazi.

Ndo maana anakuja na slogan ya KUFA-KUFAANA
 
kwa hiyo unataka kumlazimisha naye auone UKAME!, Hataki sas! amekataa ye hauoni ukame, kwa lazima kumlazimisha!? unajua mshahara wake kwa mwezi? marupurupu? !0%?... halafu unamng,ang,aniza eti aone ukame, HATAKI!
Unavyomwuona yupo sawa sawa kichwani mwake?em tuanzie hapo kwanza!
 
16105969_10206208729456660_8389378104875528706_n.jpg

Hali ya ukame tunaiona.
Mvua za vuli hazijanyesha, Rais wetu mpendwa anasema hakuna ukame.
Najiuliza sana, sijui ni ukame gani anaoungelea?
Sijui ni ule ukame wa mabao kwenye mechi ya Simba na Yanga hadi wakaenda kwenye matuta?
Yaani sipati jibu kamili kwa kweli.
Mlisema huyu mzee alizoea vya kunyonga, kuchinja hawezi.....leo ndo mnamgeukia hadi kuchukua nukuhu zake..
Chukua jembe kalime wewe hakuna msaada safari hii
 
Hakuna njaa sababu mie sijui kwenda sokoni wala bei ya vyakula siijui.Hivi Umeme mnanunua kiasi gani vile!Siku nikikosa Chakula huku Black House ndipo mseme kuna njaa.

Kwani kama hamna ugali si mle wali??
 
Mlisema huyu mzee alizoea vya kunyonga, kuchinja hawezi.....leo ndo mnamgeukia hadi kuchukua nukuhu zake..
Chukua jembe kalime wewe hakuna msaada safari hii

Siku wazazi wako wakikosa chakula ndipo utajua kama Kachumbari yaweza kuwa mboga.
 
Wanafiki walikuwa wanamfananisha bwana yule na Nyerer Mungu akaona hili ni tusi kaamua kuwaonesha mwenyewe kuwa hakika huyu hawezi hata kufunga kamba za viatu vya Nyerere, ukweli huwa haujifichi.
 
acha porojo kuhusu ukame ajakataa, alichokataa ni kuwepo kwa njaa. Na ni kweli njaa bado hamna tanzania isipokuwa kuna tishio la kutokea kwa njaa. Ila bado haijatikea.
 
Back
Top Bottom