Filosofia ya Rorya
JF-Expert Member
- Sep 20, 2021
- 3,216
- 3,585
Hivi hatuwezi kurejesha utaratibu wa Mwl Nyerere na Abeid Karume kuhusu mfumo wa muungano ambapo Rais wa Znz ndiyo lazima anakuwa Makamu wa Rais wa JMT?
Rais wa JMT akitoka Znz basi Makamu wake ndiyo atafutwe kutoka Bara. Mfumo wa Makamu wawili (wa Kwanza na wa Pili ungerejeshwa). Hivi sasa Rais akitoka Bara Makamu wake hawi Rais wa Znz bali anateuliwa toka miongoni mwa Wazanzibari.
Nadhani utaratibu huu wa waasisi wa Muungano ungeimarisha umoja wa kitaifa unaochagizwa na wapinzani na kuifanya agenda kuu; kwa sababu hata kama mpizani ndiye angeshinda kiti cha urais Znz lazima yeye ndiyo angekuwa Makamu wa Rais wa JMT hata kama nafasi ya rais wa JMT ingechukuliwa na chama tawala. Ya kale ni dhahabu!
Kwahiyo katika mazingira ya leo Makamu wa Pili wa Rais wa JMT angekuwa ni Rais wa SMZ Dr. Mwinyi.