Hatuwezi kuendelea kuilaumu Kenya na Mabeberu kwa matatizo binafsi ya Tanzania: 'We are paying the price of our own Wrongdoings!'

Hivi kila siku mnaijadili nchi jirani hamchoki! Nchi zinatofautiana kule mabepari wamewekeza sana na nchi inachukua kodi, ndiyo kinachowasaidia. Sasa povu jingi kusema elimu za watu; elimu hizo wengi wanazo lakini umasikini uko pale2. Kuna nchi hazijui kingereza lakini zimeendelea kuliko uingereza! Siamini kama kingereza ndiyo Uchumi/ kigezo cha nchi kuendelea! Sera/sasa za wakubwa haziwezi kukuruhusu wewe uendelee, Kama huamini jaribu kuendelea uone moto wake!
 
Uzi mzuri, nimejifunza mengi, asante.
Watanzania ujamaa umetuharibu. Kweli!
Hatutaki competition, tunategemea serikali itusaidie kwa kuzuia competitors.
Ingependeza tungepambana, ili serikali ituboreshee mazingira kielimu na kisera ili tuweze kumudu ushindani.

Tuna serikali inayotumia dola kutawala, tumejaa nidhamu za uoga na unafiki.
Ndiyo maana tunapata mtu mmoja n.a. kikundi chake cha wachache. anauaminisha umma wa watz kuwa maskini ni uzalendo, na watz kama makondoo wanashabikia.

Everyday is Saturday............................... :cool:
Kabisa mkuu umeeleza vema. Kama hakutakuwa na mabadiliko kwenye mfumo kama ulivoeleza, hatuwezi toka kwenye hili shimo.
 
Hivi kila siku mnaijadili nchi jirani hamchoki! Nchi zinatofautiana kule mabepari wamewekeza sana na nchi inachukua kodi, ndiyo kinachowasaidia. Sasa povu jingi kusema elimu za watu; elimu hizo wengi wanazo lakini umasikini uko pale2. Kuna nchi hazijui kingereza lakini zimeendelea kuliko uingereza! Siamini kama kingereza ndiyo Uchumi/ kigezo cha nchi kuendelea! Sera/sasa za wakubwa haziwezi kukuruhusu wewe uendelee, Kama huamini jaribu kuendelea uone moto wake!
Ni lazima tutaendelea kujadili nchi nyingine, ili itusaidia kujifunza kwa wanaofanya vizuri.

Unasema 'Kule mabepari wamewekeza' --> unadhani ni kwanini huku Tanzania hawawekezi?

Kuhusu elimu, nimesema wazi kwamba elimu yetu haimsaidii mtanzania kujiamini na ku explore the world ambayo inaleta exposure na ina drive uchumi.

Kiingereza ni nyenzo ya kuwarahisishia watu kupata exposure na urahisi pia wa watu ku interact na nchi nyingine, kwa nchi masikini kama Tanzania unahitaji watu kupata exposure na ku interact na watu wengine.

Unaposema eti 'Kuna nchi zimeendelea na hazizungumzi Kiingereza' -- mimi ntakutajia hizo nchi kwamba ni kama Korea, China, Japan.. lakini hapo hapo unashindwa kuelewa kwamba hizi nchi growth zake zimekuwa triggered from within ndo mana kiingereza haikuwa muhimu kwao, ila unapoongelea Tanzania, development yetu kwa namna ya structure ya uchumi wetu na hata nchi nyingine za Kiafrica, growth inakuwa determine from outside ikiwa na maana hizi ni exports, imports, FDI, misaada etc.. so moja kwa moja unahitaji watu wako wajue lugha ya Kiingereza ili iwe rahisi ku interact na watu wa nje.
 
Ulichokiandika kiongozi ni sahihi,Hapa Tz hatupendi kuchukua maamuzi ya mmoj mmoja kwa tuliowengi kwenye kutaka mabadiliko ya kweli ya kimaendeleo,na ndio maana inapotokea jambo lolote la kimahusiano tunakuwa walalamishi Sana,Ikiwa kama tutaacha kuwalaumu wengine na kuwaona ni maadui badala ya kuwatumia kama fursa ndipo tutakapo pata maendeleo ya kweli.Inawezekana viongozi wetu ndio wanaotutengeneza kuwa na tamaduni hizi tulizo nazo leo
 
Ulichokiandika kiongozi ni sahihi,Hapa Tz hatupendi kuchukua maamuzi ya mmoj mmoja kwa tuliowengi kwenye kutaka mabadiliko ya kweli ya kimaendeleo,na ndio maana inapotokea jambo lolote la kimahusiano tunakuwa walalamishi Sana,Ikiwa kama tutaacha kuwalaumu wengine na kuwaona ni maadui badala ya kuwatumia kama fursa ndipo tutakapo pata maendeleo ya kweli.Inawezekana viongozi wetu ndio wanaotutengeneza kuwa na tamaduni hizi tulizo nazo leo
Umeongea point mkuu, 'ulalamishi' ni sumu hata kwa maisha yetu ya kila siku..haikiwi kabisa
 
Wasalauumu wakuu!!

Uzi huu nilianza kuuandaa wakati Mama Samia anaenda Kenya, lakini sikuweza kuumaliza kwa wakati, nimeamua niuweke kwa sasa, japo muktadha wa sasa haupo kuijadili Kenya, ila itabidi niuweke kwasababu kuna mambo ambayo yapo relevant sana.

Imekuwa ni kawaida sana hapa jamvini kuona nyuzi ama comment za ‘wakuu’ kuishambulia sana nchi ya Kenya na wamekuwa wakitumia neno ‘Manyang’au’ kwa kunasabisha chuki zao dhidi ya Kenya ambazo pia zimekuwa zikichagizwa na hatua stahiki za viongozi wetu waandamizi dhidi ya Kenya. Mwelekeo wa maoni ya wadau na fikra za viongozi wengi wa ngazi za juu za Tanzania ni kwamba ‘Kenya imekuwa ikiihujumu Tanzania’ hivo ni jirani ambaye lazima atiliwe shaka.

Binafsi ntakuwa mmoja wa watu wachache wasiokuwa na ubaya wowote na Kenya, na ntakuwa wa mwisho duniani kuamini kwamba ni Kenya ndio imekuwa ikiihujumu Tanzania mpaka nchi yetu ipo hapa leo ilipo na Kenya ipo pale walipo. Nimefurahi pia sana kwa Mama Samia kuchukua hatua ya kuhuisha mahusiano yetu na Kenya. Kiongozi yeyote mwenye akili lazima angefanya kama Mama Samia. Ni kwasababu gani kwanza uwachukie Kenya?

Kama kichwa kinavosema, uzi huu ni mahsusi kuwapasha wale wote wenye mtizamo hasi juu ya Kenya. Na ujumbe ni kwamba ‘Kenya haiwezi kamwe kulaumiwa kwa matatizo yetu sisi watanzania, Tanzania inafaa kujilaumu yenyewe’

Ukifuatilia kwa makini, utofauti wa kiuchumi unaoonekana leo, kati ya nchi ya Tanzania na Kenya, umeanza kuonekana haswa miaka takribani 15 iliyopita – maana yake ni kwamba mwaka 2005 kurudi nyuma uchumi wa Kenya na Tanzania ulikuwa kwenye levels ambazo ni sawa kwa kuangalia urari wa pato la taifa kwa nchi hizi mbili.

View attachment 1805845

View attachment 1805846

So mpaka hapa, hoja ya msingi ni: Je? Wakenya wamefanya nini cha tofauti ambacho Watanzania hatukutilia maanani kuanzia mwaka 2005 mpaka sasa, kiasi cha uchumi wao kutuzidi kwa karibu USD 32 Billion (TZS 74 Trillioni) wakati mwaka 2005 tulikuwa nao sawa?

Kwa mtizamo wangu wa jicho la kiuchumi, niliweza kung’amua masuala yafuatayo. (Na tathmini yangu inaanzia mwaka 2005 kuja mbele) ambayo waKenya wameyafanya na ambayo waTanzania tuliyazembea.

1. Kuongozwa na viongozi wenye uelewa wa namna uchumi unavofanya kazi (Kuongozwa na vichwa wa kiuchumi)

‘Never underrate knowledge and what it can do to development’

Nimekuwa na mahaba makubwa na Marais wa Kenya kuanzia kwa Mwai Kibaki na hata kwa Uhuru Kenyatta, nakumbuka mwaka 2002 wakati Mwai Kibaki anamuangusha Daniel Arap Moi na chama chake cha KANU, nilikuwa darasa la sita kwa wakati huo, ila nakumbuka nilikuwa nikifuatilia utangazwaji wa matokeo ya urais kwenye redio na sikuweza kubanduka, nilimfurahia sana Mwai Kibaki bila sababu yoyote.

Ila ni wakati huu wa ukubwani, ndo nakuja kutambua haswa Mwai Kibaki alikuwa mtu wa namna gani, naweza sema ndo ambaye ameweka foundation yah ii rapid economic growth ya wakenya ndani ya hii miongo miwili. Na ndio umuhimu wa kuwa na viongozi wanaoelewa vema namna ya kukuza uchumi.

Mwai Kibaki -----> CV“ …. Kibaki instead attended Makerere University in Kampala, Uganda, where he studied Economics, History and Political Science, and graduated best in his class in 1955 with a First Class Honours Degree (BA) in Economics.[4] After his graduation, Kibaki took up an appointment as Assistant Sales Manager Shell Company of East Africa, Uganda Division. During the same year, he earned a scholarship entitling him to postgraduate studies in any British University. He consequently enrolled at the prestigious London School of Economics for a BSc in public finance, graduating with a distinction. He went back to Makerere in 1958 where he taught as an Assistant Lecturer in the economics department until 1961…..”

Baada ya Mwai Kibaki 2013, akamufuata Uhuru Kenyatta – exposed person, economist, bepari, mzalendo wa ukweli, opportunist. Huyu mwamba amefanya makubwa sana kwa Kenya.

Uhuru Kenyatta ---> CV “….After attending St. Mary's school, Uhuru went on to study economics, political science and government at Amherst College in the United States.[8][9][2] Upon his graduation, Uhuru returned to Kenya, and started a company Wilham Kenya Limited, through which he sourced and exported agricultural produce…..”

Kwa Tanzania, kutoka kwa Mkapa mpaka kwa Kikwete, tulikuwa at least heading in the right path, kwa sababu ni viongozi ambao walikuwa wanajua ni namna gani ya kukuza uchumi, na sera zao za uchumi wa soko ndio haswa zilisababisha booming ya private sector in Tanzania.

Laiti kama aliyempokea kijiti Kikwete angekuwa ni mtu dizaini ya Uhuru Kenyatta, Tanzania ingekuwa ya tofauti sana, hicho ndo nnachoamini. Ndo mana daima ntaamini kwamba, ujio wa Rais Magufuli ambaye hakuelewa vema the role of private sector to economic growth, itabaki kuwa janga la kihistoria kwa nchi ya Tanzania, as a result of Magufuli regime, kuna dynamics nyingi sana za kiuchumi zimebadilika ambazo zilisababisha huu uchumi uchechemee kwa at least 5 years, while in the same time, uchumi wa Kenya ulikuwa unapaa, chini ya MasterMind Uhuru Kenyatta.


2. Cost of doing business (mazingira ya ufanyaji wa biashara na uwekezaji)

Ni biashara na uwekezaji ndo unakuza uchumi wa taifa, nchi ya kenya imekuwa iki improve sana kwenye mazingira ya ufanyaji wa biashara na uwekezaji kwa miaka ya hivi karibuni kulinganisha na nchi ya Tanzania. Hii imepelekea mazingira rahisi ya kibiashara na uwekezaji kwa wakenya wenyewe na wawekezaji wa nje.

View attachment 1805847
View attachment 1805848

Ukiangalia hizi takwimu za ease of doing business kwa nchi ya Tanzania na Kenya, unaweza kuona kabisa kwamba kwa miaka mitano iliyopita, nchi ya Kenya imeweza ku improve in cost of doing business kwa points 15.21 wakati kwa Tanzania improvement ya mazingira ya kufanya biashara na uwekezaji yaliongezeka kwa points 4.77. (Ni kama kwenye era nzima ya Magufuli, ambayo unahesabu kuanzia mwaka 2017 kwa sababu hizi takwimu zinatolewa mwaka mmoja kabla, ni kwamba hakukuwa na improvement yoyote katika mazingira ya ufanyaji biashara na uwekezaji)

Kwenye hizi takwimu za mazingira ya ufanyaji biashara, huwa wanaangalia viashiria vifuatavyo

  • Paying Taxes – mazingira ya ulipaji kodi
  • Getting credits – kupata mikopo, riba za mikopo etc
  • Starting a business – leseni ya biashara, vibali etc
  • Construction permit – vibali vya ujenzi
  • Getting electricity
  • Registering properties
  • Protecting minority investors
  • Trading across borders
  • Enforcing contracts.
  • Resolving insolvency
Bila kuingia kwa ndani kabisa, kwenye hivo vigezo hapo juu, ila tuelewe tu kwamba Kenya walifanya improvements kubwa sana kwenye kuboresha mazingira kama ya upatikanaji wa mikopo (mfano bunge la Kenye lilileta sheria ya ku cap interest rate at 13% ambayo kwa kiasi fulani ilisaidia sana wakenya ku access mikopo) bila kusahau uraisi wa kufungua kampuni Kenya ambapo nadhani sheria yao, inaruhusu mtu kuanzisha kampuni bila kuwa na capital. Wameweza pia kuwa na uboreshaji mkubwa wa sheria za kodi.

Kwa Tanzania sote tunajua mambo yaliyotokea miaka ya hivi karibuni, na unaweza kuona ni namna gani mazingira yetu ya kufanya biashara yamakuwa ni mabovu mno na hii imekuwa na matokeo yake kwenye shuhuli za kiuchumi.


3. Elimu yenye tija kwa watu wake na lugha ya kiingereza.

Mfumo wa elimu wa Kenya umeimarika sana, sijui ni kwasababu ya mchango wa lugha ya ‘Kiingereza’ ila Wakenya wengi waliosoma tena shule na vyuo vyao vya ndani, wamekuwa ni watu wakujiamini sana, hii imepelekea miaka ya hivi karibuni wakenya wengi waende kufanya kazi nje ya nchi yao, as a result wengi wamepata exposure kulinganisha na watanzania ambao wengi ni waoga kutoka nje ya nchi yao kwa sababu ya kutokujiamini partly inawezekana ni kwasababu wengi wa watanzania Kiingereza imekuwa ni tatizo, kwahiyo wanaogopa kuvuka boda.

Mwisho wa siku impact inaonekana kwenye uchumi, ukiangalia kwenye takwimu za remittances flow, utakubaliana na huu ukweli ambao mimi nauhusianisha na ‘elimu na lugha ya kiingereza’ – whether ukubali au ukatae, ndo ukweli huo.

View attachment 1805850

So basically, Tanzania is paying the heavy price kwa vitu ambavyo tunakuwa tunavipuuzia na ambavyo wakenya wanavipa kipaumbele. Tumekuwa nyuma sana Tanzania na wanasiasa wetu bado hawajatambua namna ya kubadilisha.


4. Katiba, sheria, na miongozo

Kipindi cha Mwai Kibaki, Kenya walibahatika kupata katiba bora sana ambayo imeweza kutoa mazingira bora ya kufanya shughuli za kiuchumi kwa wakenya. Imefanya wakenya ku embrace ubepari ambao ndo mfumo unaofanya kazi katika kukuza uchumi, while Tanzania bado tunagandana na ujamaa usiofanya kazi.

As a result, katiba ya wakenya ambayo ime grant freedom of thinking imekuwa chachu ya kufungua akili za wakenya, no matter hata ukiona trend ya remittances flow, inakuambia kitu fulani.

Huku kwingine Tanzania, na vyombo vya kutuga sheria wamekuwa wapo busy kuzidi kukandamiza watanzania kwa kutunga sheria ambazo zinaminya uhuru wa fikra ambayo ni chachu ya kukuza uchumi na kufanya innovation.

Ni kama vile wanasiasa na watunga sheria wa Tanzania wamekuwa wapo busy kuonesha wao ni miamba na miungu watu, utaangalia type ya viongozi kama Magufuli, Ole Sabaya, Paul Makonda, Job Ndugai and the likes.. yaani ni kama walikuwa na uadui na watanzania wakati wangetakiwa kuwa busy kufikiri ni namna gani wataboresha mazingira wao walikuwa busy kuwakomesha watu – Take it or leave.. ndo ukweli ambao wengi tunaochambua haya mambo tutabaki kuushika.


Hitimisho
So all in all, sioni ni kwanini tuwe tunaendelea kulaumu Wakenya au Mabeberu kwa matatizo ambayo watanzania wenyewe tunayalea na tumeyatengeneza wenyewe.
  • Wakenya au mabeberu hawakutuambia tuwe na mazingira magumu ya kufanya biashara na kuwekeza – tulichagua wenyewe kuwa sheria kandamizi za uwekezaji.
  • Sio wakenya au mabeberu waliotuambia tuendelee kuwa na elimu ambayo haiwapi watu kujiamini kuvuka border na ku explore the world – tulichagua wenyewe
  • Sio wakenya au mabeberu walituambia tuendelee kuwa na mfumo wa kijamaa usiofanya kazi – tulichagua wenyewe
  • Sio wakenya au mabeberu walituambia tuwe na viongozi wanaokanyaga sheria – tulichagua wenyewe
  • Sio wakenya au mabeberu walituambia tununue ndege cash wakati kuna vipaumbele vingine ambavyo tungeweza kuwekeza na kutoa return nzuri kwa jamii – ni sisi wenyewe tulilipa pesa cash hawakutushika mkono
  • Sio wakenya au mabeberu walituambia tununue ndege halafu tuandike ‘Hapa kazi tu’ badala ya kuandika ‘Karibu Tanzania nchi ya Mlima Kilimanjaro’ – ni sisi wenyewe
So, watanzania wenzangu, tuache hii tabia ya kupenda kuwatwisha mizigo Kenya na nchi nyingine hata Mabeberu, kwa matatizo ambayo ni sisi wenyewe tunayasababisha, tunayakumbatia, na tulichagua kuwa nayo.

Maisha yamenifundisha kwamba, ‘you will always pay the price of your mistakes’ iwe kwenye mahusiano, iwe kwenye kitu chochote, utalipia makosa yako. So watanzania wenzangu wenye akili, adui wentu hawezi kuwa Kenya, adui wetu hawezi kuwa Mabeberu, adui wetu ni hawa ambao mpaka sasa hatuna katiba ya kueleweka, demokrasia ya kueleweka, sheria kandamizi, na wapo wanadunda kila siku tunawaona. Ni hawa hawa ndio wanakesha wakituaminisha kwamba Wakenya ni wabaya, mabeberu ni wabaya, wakati wao ndo wabaya.

Wako katiba ujenzi wa Taifa
N.Mushi

Sababu yako namba 3. Hizo ni hisia zako na si uhalisia.
Hivi unajua ni kwa nini watu hutoka nchini mwao na kwenda nchi nyingine?? Kwa taarifa yako, kwa ukanda huu wa A. Mashariki Somalia na Ethiopia ndiyo nchi zinazoongoza kuwa na watu wengi sana nje ya mipaka ya mipaka yao. Ukizunguka ulaya utawaona wengi mno wakifanya kazi za kawaida mpaka kuwa walimu wa vyuo vikuu. wengine wanaendesha subways na wengine askari. Kwa hiyo unataka kuniambia elimu ya somalia na ethiopia ni bora sana ndiyo imefanya watu wavuke mipaka?
Kwa taarifa yako, kama raia wa nchi fulani hawapendi kukaa nchini kwao, bali wanapenda kutoka nje. Hiyo siyo credit, hilo ni tatizo. ndiyo maana huwezi kuta waigereza, japan, ujerumani, nchi za skandinavia wanakimbia nchi zao na kwenda kwingine. Factor kubwa ni social and political unrest. kama unakumbuka kwenye historia, wangoni waliondoka A. Kusini kwa sababu ya mazingira magumu. ni kama osmosis movement from high concentration to low. Kwa hiyo watu wanaondoka kenya kwa sababu ya ugumu wa maisha. ndiyo maana kuna wengine mayaya walitelekezwa kule sana nchini yemen.
 
Ni lazima tutaendelea kujadili nchi nyingine, ili itusaidia kujifunza kwa wanaofanya vizuri.

Unasema 'Kule mabepari wamewekeza' --> unadhani ni kwanini huku Tanzania hawawekezi?

Kuhusu elimu, nimesema wazi kwamba elimu yetu haimsaidii mtanzania kujiamini na ku explore the world ambayo inaleta exposure na ina drive uchumi.

Kiingereza ni nyenzo ya kuwarahisishia watu kupata exposure na urahisi pia wa watu ku interact na nchi nyingine, kwa nchi masikini kama Tanzania unahitaji watu kupata exposure na ku interact na watu wengine.

Unaposema eti 'Kuna nchi zimeendelea na hazizungumzi Kiingereza' -- mimi ntakutajia hizo nchi kwamba ni kama Korea, China, Japan.. lakini hapo hapo unashindwa kuelewa kwamba hizi nchi growth zake zimekuwa triggered from within ndo mana kiingereza haikuwa muhimu kwao, ila unapoongelea Tanzania, development yetu kwa namna ya structure ya uchumi wetu na hata nchi nyingine za Kiafrica, growth inakuwa determine from outside ikiwa na maana hizi ni exports, imports, FDI, misaada etc.. so moja kwa moja unahitaji watu wako wajue lugha ya Kiingereza ili iwe rahisi ku interact na watu wa nje.
Its all about perspective...maendeleo ya nchi ni relative..kujilinganisha na nchi zingine tutajidanganya na ndio maana tunafeli...ni km mtoto asiejitambua yuko wapi ametoka wapi na anataka kwenda wapi...kila kiongozi akija anafanya lake...

Mwingine perspective yake ni ujamaa wote ni kitu kimoja tufanye kazi kwa bidii kwa manufaa yetu wote

Mwingine kila mtu na akili yake kichwani..survival of the fittest/private sector watu waje wawekeze,hatuwezi wote tukawa sawa, km unauwezo wakupiga piga, ila mradi kuonekane kumechangamka..pesa ina zunguka transaction zinaonekana hata km hazi reflect uhalisia..twende kazi

Mwingine hapana hii si sawa Tanzania ni yetu wote, rasilimali zote ni zetu zitatumika kutunufaisha wote, tumefanywa shamba la bibi, watu wanaiba wanajinufaisha wakati mwananchi wa kawaida hapati haki za msingi...

sasa katika kila stage hapo juu lazima victim atalalamika...kwahio kusema tusilaumu mabeberu ni relative pia...

Mimi mtazamo wangu ni tukae chini tujitambue...strength na weakness zetu..halafu tusimamie strength tusonge mbele...

Kwa mfano tuna ardhi yenye rutba ya kutosha Mungu wetu tusamehe juzi kwenye radio kuna sehemu sijui uko sumbawanga kama sikosei wanasema miwa inakubali hatari hawajui waipeleke wapi inaoza shambani huku tunalia hatuna sukari tuna import...kinachotushinda nini kuwezesha kufungua kiwanda cha sukari kule..mimi naona labda kuna laana inatutafuna...tunaviongozi kila kona ya nchi..sijui RAS sijui katibu tawala..sijui mtendaji wanini wote hawa km hawako ujasiriamali minded kwa ajili ya rural development..

Kwa kifupi nobody can fix us but ourselves, sasa viongozi km hawalitambui hilo kazi ni kupigana vijembe huyu yuko hv, yule mshamba, huyu diplomat, huyu CCM B, huyu sukuma Gang..basi ili mradi tafrani..

Kenya hv, Kenya vile wale Urafiki yao tokea enzi za Nyerere inaendelea bado..maviwanda tokea enzi hizo bado zipo operational zinachapa kazi..sie sijui tunaviwanda vingapi vyakujilinganisha..tutauza mali ghafi tuambulie chenji tu..wakati wao wanazalisha wanapata manoti

Sasa tunawatafutia soko la products zao wakati sisi hatuna products za kucompete nao..mwisho wa siku tunauwa viwanda vilivyoanza kujikongoja...km vile tunaenda mbele kumbe tunarudi nyuma sababu hatujielewi..tutabaki kutoa mapovu tu huku kwenye mitandao
 
Juzi nasikilizia bbc jioni.. kenya sasa imerahisisha taratibu za kufungua kampuni ambapo watu wataweza kufungua kampuni chini ya saa 24 process zote zinakuwa tayari.

Ukija Tz kusajili jina la biashara tu kimbembe
 
Juzi nasikilizia bbc jioni.. kenya sasa imerahisisha taratibu za kufungua kampuni ambapo watu wataweza kufungua kampuni chini ya saa 24 process zote zinakuwa tayari.

Ukija Tz kusajili jina la biashara tu kimbembe
Ndo mambo yanatakiwa kufanyiwa improvements.. ipo ndani ya ease of doing business. Ukiweka urahisi wa kufungua kampuni maana yake ni kwamba unawapa fursa raia wako na wawekezaji wa nje kuongeza shughuli za kiuchumi ambazo zinakuza uchumi kwa ujumla na kutoa ajira.. ndo ipo hivo
 
Back
Top Bottom