Hatutumpata boazizi mwingine bongo kweli kwa mwendo huu? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Hatutumpata boazizi mwingine bongo kweli kwa mwendo huu?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by howard, Mar 2, 2011.

 1. howard

  howard Senior Member

  #1
  Mar 2, 2011
  Joined: Feb 21, 2011
  Messages: 188
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Akizungumza na waandishi wa habari jana katika eneo la tukio, maarufu kama ‘Big Brother’, Mwenyekiti wa Soko la Urafiki Mitumba, Idd Toatoa, alisema kuwa bomoa bomoa hiyo ilifanyika juzi majira ya saa sita usiku, ambapo katapila mbili ndizo zilizokuwa zikibomoa ili kupisha mradi wa mabasi yaendayo kasi (Dart).
  Mwenyekiti huyo alisema, bomoa bomoa hiyo imefanyika siku moja baada ya kupeleka barua yao katika ofisi za Halmashauri ya Kinondoni kwa ajili ya kuomba maeneo waliyokuwa wameyapendekeza kwa ajili ya kufanyia biashara zao, lakini kabla ya kujibiwa usiku wake ndipo tingatinga lilifika na kubomoa.
  Aliyataja maeneo ya wazi waliyokuwa wameyapendekeza kuwa yapo Shekilango, japo serikali iliwataka waende katika maeneo ya ‘Engle’ karibu na soko la ndizi, Soko la Makumbusho na Mburahati.
  “Maeneo yaliyopendekezwa na serikali hatukuwa tayari kwenda kwa kuwa katika soko la ‘Engle’ kule wanauza ndizi na nyanya, sasa mitumba na nyanya wapi na wapi?” alihoji na kuongeza kuwa, maeneo ya Soko la Makumbusho na Mburahati serikali ilitumia nguvu kubwa kuwapeleka wafanyabiashara kule, kwa kuwa hakuna biashara.
  Kwa maelezo ya mwenyekiti huyo, tukio hilo ni kubwa na ni janga la kitaifa, hivyo anamuomba Rais Kikwete aingilie kati, vinginevyo hawataiunga serikali yake mkono.
  “Ninamuomba Rais Kikwete aingilie kati suala hili, vinginevyo mimi kama kada wa CCM, kwa jinsi hii sitaweza kumuunga mkono,” alisema.
  Aliongeza kuwa, kutokana na suala hilo imeonyesha ni jinsi gani serikali inavyowadharau, hivyo wafanyabiashara hao hawatakuwa tayari kuirudisha tena serikali hiyo madarakani.
  Pia alisisitiza kuwa kwa hatua hiyo ilipofikia anaona rais Kikwete ndiye atakuwa mtawala wa mwisho katika chama chake cha CCM, kwa kuwa hakuna mtu atakayempigia kura mgombea mwingine.
  Mbali na hilo mwenyekiti huyo alisema kuwa bomoa bomoa hiyo imesababisha wizi wa mali za wafanyabiashara hao, ambao wengi wao wamekopa katika Chama cha Kuweka na Kukopa (Saccos), cha soko hilo.
  “Kutokana na umoja wetu huu wa kuuza mitumba, CRDB walitupa milioni 250, Self milioni 150 na Pride milioni 50, na pesa hizo wamekopeshwa wafanyabiashara hawa, sasa unafikiri watazilipaje?” alihoji mwenyekiti huyo.
  Katika hatua nyingine, mwenyekiti huyo alieleza kuwa bomoa bomoa hiyo ilipoanza alipigiwa simu na baadhi wa wafanyabiashara waliokuwa karibu na tukio, na alipokwenda kuwahoji wahusika alipigwa na kuumizwa maeneo mbalimbali mwilini mwake.
  SOURCE: TANZANIA DAIMA
   
Loading...