Hatutarudia makosa ya Mwalimu Nyerere kwenye kuunda Katiba mpya

mzalendo iq1

JF-Expert Member
Mar 10, 2020
1,262
2,000
Habari na poleni na majukumu,

Kama kichwa cha habari kinavyo jieleza kua hatuwezi kurudia makosa ya Mwalimu Nyerere ya kuminya haki ya Watanzania wengi na kufanya maamuzi yake ambayo yanataka kuligharimu taifa.

Wote nina imani tunajua kabisa zilipigwa kura za maoni za kutaka Watanzania wachague mfumo wa uongozi kua wa vyama vingi au la. Watanzania walio wengi babu zetu walijua kabisa kwamba vyama vingi vitatuingiza kwenye matatizo ya kugombea madaraka Waka kataa mfumo wa vyama vingi.

Lakini Mwalimu Julius Kambarage Nyerere akaamua kupinga mawazo ya walio wengi ambao ndio wenye haki kikatiba akaamua awape wachache kwa mapenz yake ivyo ningependa kama watanzania tutapata chansi tisirudii makosa inabid tusikilize mawazo ya wengi Kwan katiba yetu inasema wengi wapewe Ila tukiendelea kuogopa taswira zetu wenyewe kwenye vioo tumeisha.

Kama kuna anayebisha kua watanzania walio wengi walinyimwa haki yao walioiomba abishe hapo chini ila ukweli utabaki kuwa wazee wetu hawakuwahi kubariki mfumo wa uongozi wa vyama vingi mpaka wamekufa.

Vyama vingi ni mwiba kwa utawala wa Africa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere alituongoza vyema sana lakini alifanya kosa kubwa kuamua juu ya maamuzi ya watu.
 

Los técnicos

JF-Expert Member
Sep 14, 2014
2,790
2,000
Binafsi nadhani kizazi kile na hiki cha leo ni tofauti kabisa. Labda ungetoa hoja iitishwe kura ya maoni mpya ili tuupime upepo upya
 

sblandes

JF-Expert Member
Apr 25, 2010
5,249
2,000
Kumbuka Nyerere ndie aliyevifuta vyama vingi mwaka 1962 na ndie aliyevirudisha alipoona anastaafu.
Wako watu wengi hawajui aliyekoroga demokrasia ni Nyerere, Alliyeuwa vyama vingi ni Nyerere ,Aliyebadiri katiba tunayoipigia kelele ni huyo huyo Nyerere.

Aliyeuwa tamaduni za makabila yetu ni yeye. Never trust a politician they are rattle snakes.
 

Qualbalasad

Senior Member
Jul 14, 2011
131
225
Labda ukiwa sio mtafiti utakuwa maisha yako yote ni mtu kulaumu. Kulikuwa ni usiku wa giza totoroo kiasi hata mwembe wenyewe hauonekani, kisha uruhusu wenye mawe waangue maembe. Wakati anachukua nchi haukua muda muafaka kwa vyama vingi
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom