Hatutarajii mawe tena Z’bar-JK | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Hatutarajii mawe tena Z’bar-JK

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Luteni, Feb 20, 2010.

 1. Luteni

  Luteni JF-Expert Member

  #1
  Feb 20, 2010
  Joined: Jan 9, 2010
  Messages: 2,274
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  RAIS Jakaya Kikwete amesema baada ya maridhiano kati ya Chama cha Wananchi (CUF) na Serikali ya Mapinduzı ya Zanzibar, hali ya kisiasa, itazidi kuwa nzuri visiwani humo.

  Mbali na hilo, amesema watu wasitarajie sasa kusikia amri za wanasiasa za kuchochea vurugu visiwani humo.

  Akizungumza na wanafunzi wanaosoma nchini Uturuki juzi, Rais Kikwete alisema ''baada ya mazungumzo hali ya Zanzibar itazidi kuwa nzuri zaidi. Matumaini yetu amri za wanasiasa kupiga mawe hazitakuwapo tena.”

  “Kawaida wanasiasa ndiyo wanaogombana na si wananchi,” aliongeza Rais Kikwete. Rais Amani Abeid Karume na Katibu Mkuu wa CUF, Maalim Seif Shariff Hamad walikutana Ikulu Zanzibar, Novemba 5, mwaka jana na kuzaa maridhiano ya kisiasa visiwani humo na sasa kunaandaliwa kura ya maoni kwa ajili ya kuundwa kwa mfumo wa Serikali ya Mseto.(Habari Leo)

  My take
  Kumbe alikuwa anajua wanaoanzisha vurugu ni viongozi alikuwa wapi sasa kukemea hizo amri hadi baadhi ya wananchi wasio na hatia kupoteza maisha yao au alikuwa hawajui kwa majina si viongozi tu bali hata ukimya wake pia ulisababisha kuchochea vurugu
   
 2. a

  alibaba Senior Member

  #2
  Feb 20, 2010
  Joined: Jun 24, 2009
  Messages: 185
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Luteni,
  Unamulika Nyoka anzia miguuni pako, umesahau kuwa Kikwete naye ni Mwanasiasa? waarabu wa Pemba hao ..........................!
   
 1. This site uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
  By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.
  Dismiss Notice
 1. This site uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
  By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.
  Dismiss Notice
Loading...