Hatutakubali!

Mlenge

R I P
Oct 31, 2006
2,125
2,291
Wandugu,

Leo (Juni 30 2010) ndio mwisho wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kama tunavyoifahamu, kwani kuanzia kesho (Julai mosi 2010) Tanzania itakuwa chini ya "Soko la Pamoja" la EAC. EAC ndiyo itakayokuwa imeshika hatamu za uongozi kwa vile maamuzi yake yatakuwa ya mwisho. Kwa Kiswahili kingine, huo ndio mwisho wa kuwapo kwa Tanzania kama dola na jamhuri ya muungano.

Iwapo kufuta Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ni jambo zuri au baya imefikia kuwa suala la mjadala, pengine watawala wetu waliofikia maamuzi haya wako sahihi, maana miaka ya zamani, na katika nchi nyingine, kufuta 'dola' ilikuwa ni suala wanaloliita 'uhaini', na dola zilizofutika yalikuwa ni matokeo ya kushindwa vita vya moto.

La kutia mashaka, ni pale ambapo hata watawala na 'wasomi' wetu hawaelekei kuelewa nini hasa maana ya EAC. Baadhi ya wachache wanapoeleweshwa maana halisi ya EAC huja juu kwa maneno "haiwezekani! hiyo itakuwa hatari! hatutakubali! maneno unayosema ni makali sana! watawala wetu hawawezi kusaini mikataba ya namna hiyo!" n.k. n. k. n.k.

Pasipotokea serikali ya Tanzania kuzinduka kungali na mapema na kujitoa EAC na soko lao la pamoja kabla ya Julai mosi (kesho), hatari yake si kidogo.

Common Market haiwezi kufuta dola....? kinachoweza kufuta ni Political union ambayo hata European Union hawajafika huko. Jua kuna hatua katika regional integration yo yote:
1-common market
2-free trade area
3-economic union
4-political union or federation
 
What? How? mbona sijakuelewa? Hebu tuelimishe zaidi hapa mkuu!

Mkosoaji,

Haya yameshasemwa sana humu... Tanzania has surrendered to EAC its sovereignty as starting from tomorrow... just dig for the past messages.

Mlenge
 
Common Market haiwezi kufuta dola....? kinachoweza kufuta ni Political union ambayo hata European Union hawajafika huko. Jua kuna hatua katika regional integration yo yote:
1-common market
2-free trade area
3-economic union
4-political union or federation

Lumbe,

Hiyo si ndio gia wanayoingia nayo, ambayo serikali ya Tanzania inajifariji nayo... umesoma mikataba ya EAC?

Mlenge, kiuhalisia situation ndivyo ilivyo, Tatizo kwa TZ watumishi watanzania walio EAC hawajaajiliwa kwa merits bali kwa ufisadi-kujuana, undugu, ngono etc. They know nothing abt adv and disadv. Na ndiyo maana wakenya, waganda na wanyarwanda hutuona sisi mabolizozo. Kwanza hata policy makers na wanasiasa wanaokwenda pale eac for policy meetings elimu zao ni za kughushi.....! inasikitisha inatisha sana.

To me it is better hata kujitoa tu. Hatuna watu wenye uwezo kitaaluma kuwakilisha maslahi ya Tanzania pale EAC.
 
You summed it up well. Tanzania kujitoa EAC is the only solution.

Na kweli wanatuona mabolizozo...

Mlenge
 
niliipata press release ya EAC about iyo kesho!!

unajua hiki EAC majority ya watanzania hawajawai isikia,au tumeisikia ila hatujaelewa,na wanaoielewa hawajatoa elimu ya kkwanini tunaingia EAC 2010 na mengineyo...

iyo mikataba ni siri ya serikali au???ili tujue adv na disadvs zake

kwakweli ndo maana tunatukanwa sana na majirani zetu
 
Sure...Tupo wengi tusiojua....Mimi nakiri mapungufu ya uelewa katika hili swala....Naomba Msaada.
 
Nina hakika nitaamka kesho Julai 1 2010 na Jamhuri ya Mwungano wa Tanzania itakuwa bado ipo hai na imara.
 
I really don't kind it... kwani mnayo nchi sasa hivi ili kiwe nini? Nina uhakika kama ingekuwa ni "common market" na US au UK au RSA tusingelalamika sana...
 
Mhhhh habari nyingine bwana.
Soko La pamoja lina manufaa sana. tatizo liko kwetu sisi watanzani utayari wetu na ufahamu wetu wa kuwa mbele katika hili soko. Mlene iweje upinge soko la Pamoja la EAC wakti hujasema kiu kuhusu hilo linaloitwa SOKO la dunia.

Ukweli Soko hili linaweza kuwa na manufaa sana if we know waht we want and how we want kwa manufaa ya nchi za afrika mashariki.
 
Tuelimishwe kwanza kbla ya kulazimishwa bila ridhaa yetu-matatizo ya kuzima moto na kutumia watu amabao upana wao wa kureason upo chini saana, mi nasema ikiwa itaanza,watakaonuafaika ni kenya na uganda na wengine na wala c watanzania!! Tutaishia kuwa maskini tu na kuambulia patupu.Mbona tuna matatizo mengi ya kusolve nchini mwetu-hilo shirikisho ni la nini kama c kuongeza matumizi yasiyo na tija? Hayo ni maoni yangu-kwa taarifa wakenya ndo wanshinikiza, bs they know how much they will benefit from it!!

As for me, I am not supporting the union
 
I really don't kind it... kwani mnayo nchi sasa hivi ili kiwe nini? Nina uhakika kama ingekuwa ni "common market" na US au UK au RSA tusingelalamika sana...

Agree with you mw kijiji

EAC is here to stay.katika ulimwengu wa leo umoja ndio jawabu.
 
Acheni woga wa bure. Kuna watu wanaogopa mno mabadiliko. Umoja ni nguvu.

Kuchanganya nguvu kuna ubaya kweli? Akija Mzungu mnampa hekta elfu 70 alime mpunga (na analima chache, nyingine anawapangishieni kwa gharama apendazo) lakini akitaka Mkenya hekta 10 alime vitunguu mnaanza kusema anachukua ardhi yetu!

Ningefurahi sana kama tungekuwa nchi moja.
 
Mhhhh habari nyingine bwana.
Soko La pamoja lina manufaa sana. tatizo liko kwetu sisi watanzani utayari wetu na ufahamu wetu wa kuwa mbele katika hili soko. Mlene iweje upinge soko la Pamoja la EAC wakti hujasema kiu kuhusu hilo linaloitwa SOKO la dunia.

Ukweli Soko hili linaweza kuwa na manufaa sana if we know waht we want and how we want kwa manufaa ya nchi za afrika mashariki.

Unaelewa maana ya soko la pamoja..au unasikia juujuu tu..?
 
Agree with you mw kijiji

EAC is here to stay.katika ulimwengu wa leo umoja ndio jawabu.

Umoja sio hoja. Kama ishu ni umoja tulikosa nchi za kujiunga nazo? Kuna wazambia huku wamalawi mozambique etc huku mimi naona wako poa zaidi and we share a good history with them.
 
Acheni woga wa bure. Kuna watu wanaogopa mno mabadiliko. Umoja ni nguvu.

Kuchanganya nguvu kuna ubaya kweli? Akija Mzungu mnampa hekta elfu 70 alime mpunga (na analima chache, nyingine anawapangishieni kwa gharama apendazo) lakini akitaka Mkenya hekta 10 alime vitunguu mnaanza kusema anachukua ardhi yetu!

Ningefurahi sana kama tungekuwa nchi moja.

Hamna anayeogopa kitu chochote, hivi kwanini mtu akiuliza maswali ya msingi anazushiwa vitu visivyo kuwa na maana?
 
.....soko la pamoja kinadharia ni zuri kwa maana ya kurahisisha biashara among the member states ila wanajamii wenzangu do we have anything in hand to trade competitively with them? sote tu mashahidi kwamba Tanzania we use what we dont produce and in real sense we dont produce. nchi imejaa wachuuzi na si wazalishaji. bidhaa ngapi za kitanzania na kwa wingi kiasi gani zinauzwa kenya na uganda? je, wakenya na uganda wana tendency ya kukumbatia kijinga wageni kama sisi iwe mzungu au mwafrika mwenzetu? level za uzalendo na political movements zao zipo vipi uki-compare na zetu? huku bado mafisadi wanatandikiwa zuria mekundu, je wao? hizo ndio challenge zetu wakati tunaingia kwenye ushirikiano huo. Serikali yetu haim-support kabisa mtanzania pale anapoonyesha kutaka kujikwamua ila mgeni atapewa favour kibaao ku-flourish.
 
Back
Top Bottom