Sokoro waito
JF-Expert Member
- Nov 21, 2014
- 2,201
- 2,587
Wale walio wanasheria au wajuzi wa sheria popote mlipo mnatambua kabisa kuwa kabla ya kupeleka hati za mashitaka au maombi ama kiapo mahakamani ili kufungua kesi au maombi yoyote, ni lazima kwanza uyapitie tena ili kuyahakiki na kuona kama kuna kitu au jambo limesahaulika.
Kwa mfano: Tarehe na sehemu ulipoapia kwenye kiapo na mengineyo yaliyo muhimu. Lakini hali imekuwa tofauti kwa wanasheria hawa waliopeleka maombi ya pingamizi la dhamana kuzuia tundu lisu asipewe dhamana.
Haiwezekani washindwe kirahisi kiasi hicho kujaza tarehe na sehemu walipoapia kiapo chao, ukizingatia kuwa hii ilikuwa ni kesi kubwa iliyohitaji umakini mkubwa, na hatahivyo walikuwa wanasheria zaidi ya mmoja, iweje sasa washindwe wote kukipitia kiapo hicho kabla ya kukipeleka mahakamani.
Badala yake wameiaibisha serikali kwa kushindwa katika hatua ya awali kabisa. Haliwezekani kufikirika jambo hili, wanasheria hawa wakamatwe wahojiwe kwanini washindwe kirahisi hivyo na waseme ukweli maana huenda hawa wanasheria wako pamoja na tundu lisu japokuwa walijifanya kumpinga mahakamani. Hatutaki wanasheria dhaifu