Hatutaki Rais Kijana wala Mzee ila tunahitaji kiongozi atakaye heshimu katiba yetu, shida zetu na kutuheshimu Wapiga Kura

TumainiEl

JF-Expert Member
Jan 13, 2010
6,188
11,219
Nimeona nitoe ya moyoni kuelekea 2025 maana kwa Neema za Mungu tukikuwepo basi ningeomba swala la kutuchagulia vijana lisiwe agenda ila agenda iwe ni kumpata kiongozi mwenye busara na anaye heshimu katiba yetu na sheria zetu. Mvumilivu na mwenye kutambuwa sisi Watanzania ni waugwana hivyo asituburuze kama familia yake. Akumbuke kuna wapiga kura na kama kweli wamemchagua basi atawaheshimu.

Sera ya vijana imezua balaa kubwa na kufanya amani isiwepo katika jamii sisi tunasema hata kama huyo mtu ni mzee na siku zake za kuishi zimeisha basi kama ni mwenye kaliba ya hayo nimesema ndio apewe nchi.

Nasema hivi nikiamini ikiwa kweli ajaye atakuwa kijana ktk vijana hawa nawaona basi let pray. Tutakuwa na taifa la mihemko iliopitiliza na huenda watu watakosa furaha zaidi kwa taifa lao.

Hayo ndio maoni na maono yangu tunahitaji kiongozi atakaye kuwa na Utu na heshima kwa Raia wake na kukumbuka watanzania ni waugwana ila sio watu dhaifu ask Mwalim Nyerere.
 
Sisi tunataka rais mwadilifu mwenye maarifa na mchapakazi kama Magufuli.
 
  • Thanks
Reactions: tyc
Tanzania unayoiota utakufa bila ya kushuhudia unachokifikiria,labda generations ya wajukuu ndio watashuhudia hayo for now ni 5 yrs mengine
 
Bado sana, shida wananchi tuna nafasi finyu sana katika kuamaua nani atuongoze.
 
Aisee hii dunia ni duara. Natamani ikiwezekana mabadiliko ya katiba kisha kura maoni tuwe taifa moja serikali moja,Dr.Hussen Mwinyi awe Rais wa kwanza wa serikali ya muungano wa kitaifa wa Tanzania moja.
 
Nimeona nitoe ya moyoni kuelekea 2025 maana kwa Neema za Mungu tukikuwepo basi ningeomba swala la kutuchagulia vijana lisiwe agenda ila agenda iwe ni kumpata kiongozi mwenye busara na anaye heshimu katiba yetu na sheria zetu. Mvumilivu na mwenye kutambuwa sisi Watanzania ni waugwana hivyo asituburuze kama familia yake. Akumbuke kuna wapiga kura na kama kweli wamemchagua basi atawaheshimu.

Sera ya vijana imezua balaa kubwa na kufanya amani isiwepo katika jamii sisi tunasema hata kama huyo mtu ni mzee na siku zake za kuishi zimeisha basi kama ni mwenye kaliba ya hayo nimesema ndio apewe nchi.

Nasema hivi nikiamini ikiwa kweli ajaye atakuwa kijana ktk vijana hawa nawaona basi let pray. Tutakuwa na taifa la mihemko iliopitiliza na huenda watu watakosa furaha zaidi kwa taifa lao.

Hayo ndio maoni na maono yangu tunahitaji kiongozi atakaye kuwa na Utu na heshima kwa Raia wake na kukumbuka watanzania ni waugwana ila sio watu dhaifu ask Mwalim Nyerere.
Kiongozi bora hukemea maovu na huwa hawi sehemu ya maovu wale ambao ni wanafiki hawatufai kwani tumewaona wakijitoa ufahamu labda uchaguzi uwe kama ule wa wabeba mabegi yaliyo jaa
 
Jiwe ameturudisha primitive age za enzi ya Mwalimu,chama kimoja.Hata Mwalimu mwenyewe alishatoka huko na kuhitaji vyama vingi,hata kama kimagumashi!
 
Back
Top Bottom