Hatutaki Rais Kijana wala Mzee ila tunahitaji kiongozi atakaye heshimu katiba yetu, shida zetu na kutuheshimu Wapiga Kura

TumainiEl

JF-Expert Member
Jan 13, 2010
4,610
2,000
Nimeona nitoe ya moyoni kuelekea 2025 maana kwa Neema za Mungu tukikuwepo basi ningeomba swala la kutuchagulia vijana lisiwe agenda ila agenda iwe ni kumpata kiongozi mwenye busara na anaye heshimu katiba yetu na sheria zetu. Mvumilivu na mwenye kutambuwa sisi Watanzania ni waugwana hivyo asituburuze kama familia yake. Akumbuke kuna wapiga kura na kama kweli wamemchagua basi atawaheshimu.

Sera ya vijana imezua balaa kubwa na kufanya amani isiwepo katika jamii sisi tunasema hata kama huyo mtu ni mzee na siku zake za kuishi zimeisha basi kama ni mwenye kaliba ya hayo nimesema ndio apewe nchi.

Nasema hivi nikiamini ikiwa kweli ajaye atakuwa kijana ktk vijana hawa nawaona basi let pray. Tutakuwa na taifa la mihemko iliopitiliza na huenda watu watakosa furaha zaidi kwa taifa lao.

Hayo ndio maoni na maono yangu tunahitaji kiongozi atakaye kuwa na Utu na heshima kwa Raia wake na kukumbuka watanzania ni waugwana ila sio watu dhaifu ask Mwalim Nyerere.
 

kmbwembwe

JF-Expert Member
Aug 16, 2012
7,238
2,000
Sisi tunataka rais mwadilifu mwenye maarifa na mchapakazi kama Magufuli.
 

Nkanini

JF-Expert Member
Jun 6, 2017
1,964
2,000
Tanzania unayoiota utakufa bila ya kushuhudia unachokifikiria,labda generations ya wajukuu ndio watashuhudia hayo for now ni 5 yrs mengine
 

parts

JF-Expert Member
Mar 31, 2018
1,717
2,000
Bado sana, shida wananchi tunanafasi finyu sana katika kuamaua nani atuongoze.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom