My Son drink water
JF-Expert Member
- Nov 30, 2016
- 4,932
- 13,283
Kuna nyuzi nyingi mno humu hasa za mataga zikimshauri Rais Samia asimwachie huru Mbowe.
Kosa yote usikose akili, mataga hayajui kuwa Rais haruhusiwi kisheria kuingilia Mahakama, shauri la Mbowe lipo Mahakamani kwa hiyo Rais hahusiki.
Sisi wanachama wa Chadema hatutaki mwenyekiti wetu Mbowe aachiwe huru, tunataka Serikali iliyomshtaki kwa ugaidi iidhibitishie Dunia ugaidi wa Mbowe na siyo kumwachia huru.
Tunazo taarifa za kina na uhakika jinsi Serikali inavyowatuma wanafamilia ili wamsihi Mbowe akubali yaishe.
Kwa sababu kesi ipo Mahakamani siwezi kusema yote yanayoendelea.
Kifupi ni kwamba, Mbowe alijua kuwa atakamatwa, kwa hiyo hana cha kupoteza kabisa na yupo tayari hata kufa.
Wana CCM, mtake msitake, Mbowe ni Mandela wa Tanzania. Mkisikia hivyo it makes you go nuts, kesi mlianzisha wenyewe bila kutathimini madhara ya kutunga uongo, sasa hivi mnataka kuitema ndoana wakati imeshanasa uulimi
Pambaneni na hii kesi hadi mwisho, iweje mnataka suluhu na Gaidi?