Hatuna serikali, tuna mizigo Tanzania

Sir R

JF-Expert Member
Oct 23, 2009
2,175
298
Katika ziara zao Kinana na Nape waliibuka na hoja ya mawaziri mizigo. Katika hoja hii hawakuwa wa kweli kwani hawakuzungumzia mambo yanayowadhuru wa wananchi. Mfano mzuri mateso waliyofanyiwa watu katika operesheni tokemeza, hawakuzungumzia kabisa. Waliibuka na hoja nyepesi nyepesi.

Watanzania tuwashukuru hawa viongozi kuonesha kuwa chama tawala hawana dhamira ya dhati katika kushughulikia matatizo ya wananchi. Walisema wazi kuwa mawaziri ni mizigo, hii kauli ingetolewa na wapinzani watu wangesema ni kawaida yao.

Kwa kuwa ni viongozi wa ngazi ya juu wa CCM wamesema hilo, ni wajibu wa kila mtanzania kutokuwa tayari kuendelea kubeba mizigo hii. Tumebebeshwa mizigo vyakutosha, sasa inatosha, ni muda wa kuchukuaa hatua ya kufanya mabadiliko katika chaguzi zijazo.

Nani aseme ndio tuelewe kuwa hatuna serikali, tuna mizigo tu. Mh Rais aliijadili mizigo ya awali bila kujua kuna mizigo mingine mingi. Jana Rais kaumbuka. Kila awamu serikali inaanguka.


Watanzania tuchukue hatua, tunadharauliwa sana na mataifa mengine.
 
Back
Top Bottom