mzozaji
JF-Expert Member
- Jul 28, 2010
- 255
- 13
Wakuu nashangazwa sana na kasi ya hii serikali kushikilia kujenga mradi wa majumba ya kifahari Kigamboni kana kwamba ndio suruhisho la umaskini wetu. Nchi yetu haina maji safi sehemu nyingi na umeme wa mashaka kila siku lakini tunaona Mabilioni yakawekezwe kwenye majumba ambayo hatujui nani atapanga huku tukiwatimua watu toka makazi yao.Mimi kwa haraka naona kuna kitu kimejificha kwenye huu mradi mpaka unapelekwa puta hivi. Waziri wa ardhi katangaza bajeti ya mwaka huu kwenye huu mradi tena ni 10% ambayo ni Mabilioni na akasema hizo 90% zilizobaki 'watajua namna ya kuzipata'!! Hapa lazima kuna jambo.. Utaanzishaje mradi wakati hata fedha hujui utatoa wapi? Wenye kujua kidogo kuhusu huu mradi watujuze labda wengine tunashindwa kuelewa kwa akili ya kawaida.