Hatuna jeshi la polisi, tuna genge la wahuni lenye utii kwa mafisadi wa CCM | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Hatuna jeshi la polisi, tuna genge la wahuni lenye utii kwa mafisadi wa CCM

Discussion in 'KATIBA Mpya' started by Mag3, Dec 21, 2010.

 1. Mag3

  Mag3 JF-Expert Member

  #1
  Dec 21, 2010
  Joined: May 31, 2008
  Messages: 9,094
  Likes Received: 6,188
  Trophy Points: 280
  Hivi kuna tofauti gani katika uongozi wa jeshi la polisi chini ya Saidi Mwema na genge la "green guards" chini ya CCM ? Je kwa vitendo vya polisi tunavyovishuhudia hivi sasa dhidi ya raia wema, jeshi la polisi kweli lipo kulinda usalama wa raia na mali zao ? Saidi Mwema, kwa nini maafisa wako hunywea hata kwa katibu tarafa wa CCM lakini hawasiti kumpa kibano Mtanzania mwenye itikadi tofauti hata akiwa mbunge bila sababu ? Hivi hali hii imesababishwa na uongozi lege lege au katiba isiyokidhi mfumo wa utawala bora unaozingatia haki na usawa ? Leo hii Mbunge wa Arusha anauguza majeraha kwa kosa la kudai na kufuatilia haki lakini aliyekuwa mgombea wa ubunge Shinyanga anatamba mitaani baada ya kumkata ngwala ofisa wa polisi.
  Taifa letu halina jeshi la polisi
  lina genge la wahuni
  lenye utii kwa mafisadi
  chini ya CCM !
   
 2. A

  Anaruditena Member

  #2
  Dec 21, 2010
  Joined: Apr 29, 2010
  Messages: 52
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  katiba mpya - ndio itakayotenganisha mipaka ya watumishi wa serikali na wachama tawala; sasa hivi ili uwe na cheo kikubwa serikalini au kufanya biashara za kiuni lazima uwe mwanachama wa CCM ( chama tawala)- hakuna ethics za kazi kabisa ni kupokea order tu. Nchi imefika mbaya sana. watu walio serious haya yote ni signs za nchi kuagamia.
   
 3. L

  LAT JF-Expert Member

  #3
  Dec 21, 2010
  Joined: Nov 20, 2010
  Messages: 4,523
  Likes Received: 86
  Trophy Points: 0
  mkuu..... kwanza kabisa.... hiki chombo cha dolla hakistahili kuitwa jeshi la polisi.... bali ni Police Services.... ni chombo cha kutoa huduma za kulinda amani na kuchunga sheria zinafuatwa...... policing does not necessarily need force

  south Africa wana best policing institution in the world called South Africa Police Services (SAPS)

  lazima tubadilishe yakwetu na kuweka watumishi ambao watafanya utendaji kutokana na malengo ya chombo husika.... tunawezakuita polisi ya Tanzania (TAPS) Tanzania Police Services... haya ni maoi yangu
   
 4. Mag3

  Mag3 JF-Expert Member

  #4
  Dec 21, 2010
  Joined: May 31, 2008
  Messages: 9,094
  Likes Received: 6,188
  Trophy Points: 280
  Vitendo vya kihuni vinavyofanywa na polisi wetu chini ya uongozi wa serikali ya CCM vimewezekana tu kwa sababu ya katiba mbovu.

  • Katibu inayotoa mwanya kwa watawala kutoweza kuwajibika kikamilifu kwa wananachi waliowaweka madarakani, haifai.
  • Katiba inayowezesha jeshi la polisi kutumiwa kuwalinda watawala badala ya wananchi waliowaweka madarakani, haitufai.
  • Katiba inayowapa jeshi la polisi jeuri ya kupambana na raia wema badala ya kuwapa ulinzi na kulinda usalama wao, haifai.
  • Katiba inayowalinda mafisadi na kuwapa nguvu kiasi cha kuitetemesha serikali na hivyo kuogopwa na vyombo vya dola, haitufai.
  • Katiba inayotoa fursa kwa wafanya biashara kutumia utajiri wao kununua haki na hivyo kufanya watakavyo bila kufuata sheria, haitufai.
  • Katiba inayomnyima mwananchi haki yake ya kuchagua na kuchaguliwa kwa sababu tu hakubaliani na kikundi cha watu, haitufai.
  • Katiba inayowagawa Watanzania katika madaraja makubwa mawili ya matajiri na masikini, haitufai.
  Katiba ya sasa ya Tanzania haifai, haifai, haifai na kamwe siyo tena ya kufanyiwa marekebisho - kama tuna dhamira ya kweli ya kulinusuru taifa kazi tuliyo nayo ni moja tu, kuandika katiba mpya.
   
 5. n

  nyantella JF-Expert Member

  #5
  Dec 27, 2010
  Joined: Dec 17, 2010
  Messages: 890
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 45
  Acheni matusi jamani!!!!

  kisiasa mnaona haliwafai ila wana kazi nzito sana kulinda amani ili watu waende na kurudi toka kwenye shughuli zao za kila siku and they are being paid miserably kwa kazi ngumu ya kupambana na majambazi pamoja na haowashabiki wenu wakorofi (even Slaa of all the people wala hakemei!! sometimes they are wrong and wanavunja sheria giving the police very little option of how to handle them including the MP just like one lema!! a very uncivilized MP you will ever meet in this land!).

  by the way mnafikiri ni rahisi to be in power!! and you think CDM ikipewa na madaraka kesho inaunda jeshi, police, usalama wa taifa, na kadhalika is that possible!!!

  Great Thinkers think before you leap! the landing might not as soft as you think!!
   
 6. D

  DENYO JF-Expert Member

  #6
  Dec 27, 2010
  Joined: Sep 14, 2010
  Messages: 699
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  nyantella -tuna mifano mingi jeshi la polisi limeshindwa kutumia akili na kutumiwa hovyo na ccm, tumeshuhudia mifano mingi jeshi linashindwa kumkamata chanzo cha vurugu na kuishia kumwaga maji ya kuwasha kwa watanzania wanaodai haki-labda nikupe mfano kati ya lema aliyekuwa anasimamia haki ya kufuata kanuni katika uchaguzi na mkurugenzi aliyepindisha kanuni kumchagua meya kutoka ccm nani alipaswa kukamatwa?? Watanzania waliokuwa wakidai matokeo kutangazwa kule arusha, ubungo, kawe, mwanza, shinyanga mjini, segerea, karagwe, na wakurugenzi waliochelewesha makusudi wakisubiri maelekezo ya wakubwa nani alikuwa chanzo cha vurugu hadi mabomu yatumike -hili jeshi la polisi kwa sasa ni tawi la ccm na wapo makamanda wanatafuta vyeo zaidi kwa kuwapiga mabomu wapinzani -mfano andenyenge anatafuta kuwa igp kwa kupitia kumpiga mabomu mh.lema.
  Jeshi la polisi limejaa wanafiki
   
 7. N

  Nimrod Member

  #7
  Dec 27, 2010
  Joined: Nov 5, 2010
  Messages: 27
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  yaap
   
 8. Kaa la Moto

  Kaa la Moto JF-Expert Member

  #8
  Dec 27, 2010
  Joined: Apr 24, 2008
  Messages: 7,666
  Likes Received: 166
  Trophy Points: 160
  Katiba mbofu chanzo cha yote haya alafu mwanasheria mkuu anasema haoni ubovu wake hivi ni mjinga kiasi gani kutoona jambo hili. Hisi this guy really went to school? maana wasomi wa sheria kama yeye, majaji na laymen kama sisi wote tunaona haja, yeye macho yake yako kwenye sufuria la kikwete tu? Katiba ni lazima na hiyo itaondoa ujinga wote huu wa polisi. To hell with ujinga they call maboresho. Tutaboresha kwa katiba kwanza.
   
 9. tartoo

  tartoo Senior Member

  #9
  Dec 29, 2010
  Joined: Jul 2, 2010
  Messages: 130
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ni genge la wahuni no less no more!!!!
   
Loading...