MTENDAHAKI
JF-Expert Member
- Mar 3, 2011
- 4,013
- 1,443
Hakuna shaka kwamba Misri ndio babu wa umwagiliaji duniani. Hata hivyo tumeshajifunza kitambo toka kwao, na hata sehemu nyingine duniani kwamba umwagiliaji ni uhandisi unaotaka uwekezaji wa kutosha!
Siasa tamu za kusema wataalamu watanzania wanaweza kunufaika na ziara ya Rais wa Misri kwa kwenda kujifunza wenzetu wao walivyofanikiwa kwenye umwagiliaji ni upuuzi!
Inajulikana tatizo letu ni fedha, sio wataalamu!Tunao wabobezi wa umwagiliaji kila kona, kuanzia wizarani mpk ngazi ya kata!Wapo magwiji wa umwagiliaji vyuo vikuu wakiongozwa na SUA!
Wataalamu hawana cha kujifunza kutoka Misri, serikali inatakiwa ijifunze kutoa hela za umwagiliaji na isirushe mpira wa kitoto! Serikali haijawahi kutoa pesa za umwagiliaji kulingana na usanifu, nimefanya utafiti wa miradi kadhaa na kugundua serikali hutoa wastani wa chini ya 30% ya fedha ya usanifu wa mradi wa umwagiliaji, ndio maana hakuna mradi wa umwagiliaji uliojengwa ukakamilika toka Nyerere astaafu.
Kwa mito tuliyonayo, maziwa na mabwawa hakika Tanzania inatakiwa iwe mzalishaji mkuu wa mazao ya biashara na chakula duniani!Tanzania ni kati ya nchi zenye maji mengi zaidi yanoyofaa kwa kilimo cha umwagiliaji lakini ndio kati ya nchi zinazotumia umwagiliaji kwa kiwango cha chini kabisa!
Mpaka njaa itukomeshe, au mpaka apatikane kiongozi anayejua chakula ni kipaumbele cha kwanza ndipo tutakapopiga hatua! Hizi za kunufaika kutoka Misri ni siasa tamu za mgongo wa chupa!
Mtendahaki