Hatuna dhamira ya kuing’oa Serikali - Mbowe | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Hatuna dhamira ya kuing’oa Serikali - Mbowe

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by EMT, Mar 21, 2011.

 1. EMT

  EMT JF-Expert Member

  #1
  Mar 21, 2011
  Joined: Jan 13, 2010
  Messages: 14,464
  Likes Received: 865
  Trophy Points: 280
  CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimesema kinajitambua kuwa ni chama cha kidemokrasia na kitaendelea kutafuta ridhaa ya wananchi ya kuunda Serikali kwa njia za kidemokrasia na kwa mujibu wa sheria za nchi, na wala hakina dhamira ya kuiondoa Serikali kwa njia zisizo za kidemokrasia.

  Kauli hiyo ya Chadema wameitoa wakidai kuwepo kwa kauli mbalimbali kutoka kwa viongozi wa Serikali kuwa chama hicho katika maandamano yake kimekuwa kikishinikiza kuwa kina azma ya kuing’oa Serikali madarakani na kimedaiwa wakati mwingine kuwashinikiza wananchi kufanya hivyo.

  Aidha, chama hicho kimepongeza hatua ya Rais Jakaya Kikwete kutoa kauli ya kushusha bei ya sukari kutoka Sh 2,200 hadi 1,500 na kumtaka aendeleze nguvu kuhakikisha kodi pia
  inashuka kwa kuwa uwezo anao kama rais kwa muswada kupelekwa bungeni.

  Akitoa maazimio ya kikao cha Kamati Kuu wa Chadema kilichokaa mjini Dar es Salaam, Mwenyekiti wa chama hicho, Freeman Mbowe aliwaambia waandishi jana kwamba kumekuwa na propaganda kuwa maandamano yao yanalenga kuwatia hofu wananchi na kuipindua Serikali, jambo alilodai si kweli.

  “Hatuna ajenda ya kuipindua Serikali, ielezwe bayana ni wapi tumewashinikiza wananchi au tumesema kuwa tutaipindua Serikali, azma yetu na ambayo tutaendelea nayo katika maandamano ya Kanda za Juu Kusini ni kuishinikiza Serikali itekeleze wajibu wake kiuadilifu na si vinginevyo,” alisema Mbowe.

  Maazimio mengine ya Kamati Kuu ya Chadema kama yalivyoelezwa jana ni kukanusha kufadhiliwa na mataifa ya nje ili wafanye maandamano wanayoyafanya na kudai kuwa watampeleka mahakamani Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto, Sophia Simba kama hatawaomba radhi na kukanusha kauli hiyo.

  Mbowe alidai pia kuwa Kamati Kuu imeipa Serikali siku 21 ikiwa ni hatua nyingine ya kuitaka itafute ufumbuzi wa kudumu suala la uchaguzi wa Meya katika Jiji la Arusha, na isipofanya hivyo, itakosa jibu kwa wananchi wanaoshinikiza majibu.

  Alipoulizwa kwa nini hawaendi mahakamani wakati Serikali imeshawapa uhuru kupinga uchaguzi huo ulioipa ushindi CCM, Mbowe alisema hawakubaliani na kwenda mahakamani kwa kuwa ni kuhalalisha ushindi batili na kudai msimamo wao ni uchaguzi urudiwe kwa kufuata utaratibu, kanuni na sheria.

  Pia alisema Kamati Kuu inapinga mpango wa Serikali wa kubadilisha Sheria ya Manunuzi ya Umma kwa kuwa mabadiliko hayo yanalenga kuwanufaisha watu wachache na kuruhusu nchi kuwa sehemu ya kutupa vitu chakavu na kuongeza.

  Kwa upande wake, Katibu Mkuu wa Chadema, Dk. Willibrod Slaa alimsifu Rais Kikwete kuchukua hatua ya mfumuko wa bei ya sukari na kudai kuwa wana uhakika ni zao la maandamano yao na kwamba wataendelea kushinikiza masuala yanayosababisha mfumuko wa bei nchini.

  HabariLeo
   
 2. Mphamvu

  Mphamvu JF-Expert Member

  #2
  Mar 21, 2011
  Joined: Jan 28, 2011
  Messages: 10,708
  Likes Received: 935
  Trophy Points: 280
  Nasema hivi, ikitokea Serikali imeng'olewa madarakani, si CHADEMA watakaoitoa, bali ni wananchi wanaopigika na hali ngumu ya maisha. CCM put the blame on us, ni sisi tunaotaka kuwaondoa madarakani kwa nguvu, si CDM. CDM hawakuwaweka ninyi madarakani, SISI wananchi ndio tuliowaweka, na ni kweli kuwa TUNATAKA kuwatoa madarakani kwa nguvu. Narudia tena, SISI WANANCHI tunataka kuitoa serikali iliyopo kwa kuwa imeshindwa kutumia kodi zetu kutuletea maendeleo. NIMESEMA!
   
 3. EMT

  EMT JF-Expert Member

  #3
  Mar 21, 2011
  Joined: Jan 13, 2010
  Messages: 14,464
  Likes Received: 865
  Trophy Points: 280
  Wananchi wakiongozwa na Chadema?
   
 4. H

  Haika JF-Expert Member

  #4
  Mar 21, 2011
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 2,318
  Likes Received: 62
  Trophy Points: 145
  Sisi wananchi ndio tumewaweka viongozi waliopo madarakani kwa njia tofauti; kutokupiga kura, kuwapigia kura, kupokea rushwa ili kuharibu uchaguzi, kushabikia udhalimu wa kiutawala nk.
  Kwa njia hii kwa kuamua kufanya kinyume na tulivyofanya hapo awali tutawatoa madarakani/ uongozini/ utawalani.

  CDM iko leo, personalities tunazoziona zipo leo na kesho hatujui kama zipo au la.
  Ila tunajua hakuna kurudi nyuma,
  Tunasonga mbele kudai nchi yetu.
  Tunawashukuru CDM kwa sasa,
  Mie siwezi kuapa kuwa mwanachama wa chama chochote, mimi naapa kuwa raia mwaminifu wa Tanzania.
   
 5. Filipo

  Filipo JF-Expert Member

  #5
  Mar 21, 2011
  Joined: Jan 6, 2011
  Messages: 9,329
  Likes Received: 210
  Trophy Points: 160
  Napenda sana jinsi cdm wanavyotoa statement zao maana wanajibu hoja na mashwali tuliyonayo na sio blabla kama za watani zetu!
   
Loading...