Hatuna Budi Kumpongeza Rais Jakaya Mrisho Kikwete:

kelao

JF-Expert Member
Sep 24, 2012
7,637
2,000
Habari za jioni wana JF,Kutokana na hotuba mh.rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania mh.dr.Jakaya Kikwete leo wakati wa kupokea rasimu ya 2 ya katiba mpya,ni wazi amegundua wabunge wengi hasa wa chama chake(CCM)hupenda sana ushabiki wa kisiasa wakati wa mijadala muhimu ya kitaifa.Kitendo cha mh.rais kutahadhari vyama vya siasa kupeleka mivutano ya kisiasa ndani ya bunge maalum la katiba ni ishara ya kiongozi aliedhamiria nchi kama nchi tupate KATIBA mpya ambayo siyo upande mmoja.Nakupongeza sana mh.Rais na wajumbe wa bunge hilo maalum la katiba hamna budi kufuata ushauri huo wa busara.
 

Tatu

JF-Expert Member
Oct 6, 2006
1,079
1,225
Alifikaje hapo alipo kama ndio kwanza anagundua kwamba wabunge wa chama chake ni wafuata upepo. Wote wamo katika gunia moja, mzigo.
 
  • Thanks
Reactions: BAK

Ngatele

JF-Expert Member
Jan 25, 2011
733
1,000
Yeye ni mwenyekiti wa CCM, anawezaje kujitoa katika lawama ya mivutano ya kisiasa, ana-save face kwani anaelewa kuwa chama chake kinaweza kuleta mvutano wa kijinga kwenye bunge la katiba. Hataki kupata lawama kwenye chama na pia anataka watanzania tumwelewe kwamba yeye si sehemu ya matatizo yanayoweza kutokea.
 

Toothpick

JF-Expert Member
Nov 14, 2013
348
250
Kama ameliona hilo la siasa bungeni naomba awakanye wabunge wake wote,kuanzia spika na wengine wote.Bunge si sehemu ya siasa ingawa waliopo ni wanasiasa,kazi ya bunge ni kutunga sheria na kusimamia shughuli za serikali.wabunge hawa ndiyo wliotufikisha hapa tulipo kwa kutokujua kazi yao na kuingiza siasa ndani ya bunge.Kama spika na naib wake wangekuwa wanajua vizuri majukumu ya bunge,hakika kusingekuwa na mtu maarufu,kwa sababu wangefuata maadili ya bunge na wala si mipasho na matusi ambayo tumekuwa tukiyashuhudia kupitia hawa viongozi wa bunge.Na sijui kwanini waliamua kujiita WAHESHIMIWA? Labda niwaulize wana jf je kuna wabunge ama mawaziri wanaojiheshimu wawapo Bungeni? Je;ni nini maana ya kujiita mheshimiwa wakati huo hujiheshimu?Bunge limepoteza maadili kulirudisha mahali pake linahitaji Spika mwenye kusimamia maadili ya bunge asiyeyumbishwa na upande wowote ule.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Similar Discussions

Similar Discussions

Top Bottom