Hatumtaki James Millya Arusha Mjini: Tunasema NOOO, big NOOOO. Take note Mh: Godbless Lema

people change.
he might be a mole, he might have honestly switched sides.
As Arusha resident, Milya has witnessed a wind of change.
What if he has been, beyond reasonable doubt, swayed by the wind?

Ujumbe upo clear.... Usihangaike kuunyambua
 
Lema na Millya ni marafiki sana, nakumbuka hata ile siku daily news ili andika wazee kumkataza lema kwenda kupiga kampen arumeru nilimkuta lema na millya wakiwa pale kwenye mgahawa wa Millya VIAVIA, nikajua kuna kitu tu hapa,sas kama lema ataleta urafiki wake ndan ya chama atafurahi maana nadhan anaelewa misimamo ya watu wa arusha.Milya hana kitu alihonga mpaka kuwa rais wa Tumain University.ye akae hapo kuimarisha mambo.
 
Millya, atulie ajifunze mila na desturi zetu za Chama, akiweza kuzifuata kwa uaminifu, baadaye atapewa uongozi. Ila sasa atulie amefika kwa wazalendo kama anataka kuwa mzalendo tutamfunza.
 
Msimamo wangu juu ya Edward Lowassa na watu wake wote unafaahimka wazi. One of such people ni James Millya. Yes amehamia CDM lakini swali langu ni je atakuwa mwaminifu zaidi kwa Edward Lowassa au CHADEMA? Akiwa CCM alijiainiasha kama mtu aliyekuwa tayari kufanya chochote alichoagizwa na Edward!

Hofu yangu ni kuwa baada ya kubaini hawezi kuweka mbunge kupita CCM (alishindwa kwa Batilda, akashindwa kwa Sioi) sasa amebaini njia pekee ni kupitia CHADEMA! Hivyo Millya avuke huku awe mbunge wa Arusha mjini kupitia CDM.

CDM chama kilichojiainisha kupambana na ufisadi kamwe kisikubali kuingia kwenye mtego huu. Tunafahamu Millya amekuja na mamilioni kadhaa ambayo si yake, tunajua yalipotoka, tunajua nia yake. Mh Mwenyekiti Freeman Mbowe tumeona tamko lako jana kumpokea James, nafahamu umezungukwa na watu wanaompigia debe Millya kwa sababu mbali mbali na wengine wamekuwepo kwenye chama kwa muda mrefu na unawaamini. Ninapata hofu kubwa you are being misled on this. CDM Arusha na watu wa Arusha kwa ujumla tutamkataa James Millya kama atasimamishwa kugombea ubunge kwa tiketi ya CDM kama tulivyomkataa Mama Buriani tukifahamu fika ni nani kamtuma.

Mh Goodbless Lema, usijaribu kumbeba Millya, ngoja tukuambie wazi, tunakuheshima sana na tumekupigani wewe (tumekipigania chama chetu) vile ulibeba bendera ya chama. Ukisimamishwa baada ya rufaa tutakupigania wewe tutakipigania chama chetu. Ukimleta James Millya (iwapo mahakama itakuzuia kugombea) tutamkataa yeye na jua fika your credibility will be eroded! na hiki kitakuwa kifo chako cha kwanza kisiasa, of course in "politics one can die many times"

Kama tumekose kwa namna tunavyomwona Millya, fine give us time tujionee kuwa Millya amebadilika na si yule wa Lowassa. Tutahitaji muda kujiridhisha kuwa kweli yupo loyal to the course, yupo loyal to CDM na kweli ameachana na baba yake Lowassa. Msituletee sasahivi kwenye ubunge,

Chonde! chonde! chonde!

Nafikiri tunajenga woga usio na sababu, yaani mambo ya kufikirika tu yamnyime mtu haki yake ya kikatiba ya kujumuika? no! No! tutoe muda wa kkuhakikisha hayo. Tutoe benefit of dooubt.
 
Lema na Millya ni marafiki sana, nakumbuka hata ile siku daily news ili andika wazee kumkataza lema kwenda kupiga kampen arumeru nilimkuta lema na millya wakiwa pale kwenye mgahawa wa Millya VIAVIA, nikajua kuna kitu tu hapa,sas kama lema ataleta urafiki wake ndan ya chama atafurahi maana nadhan anaelewa misimamo ya watu wa arusha.Milya hana kitu alihonga mpaka kuwa rais wa Tumain University.ye akae hapo kuimarisha mambo.
 
mimi nashauri millya asipewe cheo chochote mpaka baada ya 2015 ili tuone mikakati ya lowasa dhidi ya ccm katika uchaguzi ujao.
 
Millya akipewa chance arush mjini najitoa mhanga.hawezi yule,anaweza kule simanjiro.ila nawaamini viongozi wangu hawatkurupka.a town 4 lema only..
 
Ndugu shukrani kwa changamoto zako ulizofafanua,mimi binafsi ninamfahamu Millya na nilikuwa naye kabla haja kuwa kiongozi wa uvccm na nikapoteana nae niliporudi ndio nikakuta ameingia kwenye siasa,hata mimi naona Milya asigombee nafasi ya kumrithi Lema,watafutwe watu wengine ambao tayari walikuwa kwenye chama na wana uzoefu.Milya atakuwa mzuri sana kugombea ama monduli au simanjiro 2015 na anao watu wengi sana kwenye jamii ya wamasai,ikumbukwe chadema bado haina ngome imara katika jamii ya wamasai,na ni jamii inayo hitaji elimu sana,hasa ikizingatiwa baadhi yao hawajui kusoma wala kuandika.Japokuwa mimi sio mkabila ila chadema inakubalika kwenye dola za wameru,wachaga,wakurya,wasukuma,wa iraq,watu wa mbeya na jamii ya watu wa mjini kwenye miji yenye wasomi wengi kama Dar centre-ubungo,kawe,segerea,Iringa na baadhi ya sehemu chache sijazitaja kama jamii ya kigoma n.k
Lakini Bado kuna maeneo bado watu hawana uelewa sana na chadema na hawajui jinsi ya kuitoa CCM,wamasai,wagogo,watu wa pwani,yaani lindi,mtwara,pwani, na maeneo yaliyo athiriwa na usultani kama Tabora,Zanzibar na Tanga.Maeneo mengine upepo unaweza badilika saa yoyote kama moro,ruvuma, njoluma,katavi sumbawanga,na singida
Kwa hiyo kwa mawazo yangu mi naona Milya atasaidia kwenye jamii ya kimasai na Chadema wanakazi ya kufundisha demokrasia,hasa kipengele cha kupiga kura na kulinda kura na kutafuta njia stahili ya kusimamia kura za uraisi.wanaweza wakalinda kura za wabunge wakasahau kura za urais!!!!


WOOOOOORD!! umesema mkuu
 
Please update me, what is the minimum time for a member in CDM, is supposed to be a 'live and active' member before he is allowed to contest for any position? be it MP or Party's
 
Subira kidogo, kukua ni pamoja na kukutana na changamoto mpya kila kukicha inawezaka wasiwasi wa mtoa hoja ni sawa ila there is something on nothing inategemea na atakavyotumiwa. Ila wadhifa aliokuwa nao CCM na jinsi alivyotoka pamoja na kuhama kwake his integrity no doubt should be kept in question, anaweza fanya lolote at any time t
 
Mwacheni Millya aje CDM, kwanini tuamini viongozi wetu hawajakaa na kufanya tathmini ya kina kabla ya kumpokea kuwa mwanachama. Tuwaamini viongozi wetu na tuiamini intelligence system ya ndani ya chama, ingawa haiwazuii wanachama wanaokitakia mema chama chetu kutahadharisha. Tumeumwa na nyoka - Shibuda ametusumbua baada ya kupata ubunge kupitia cdm. Sisi wanachama wa CDM pia yatupasa kuwa makini kwani hili suala linaweza kutumiwa na adui zetu kutuvuruga. Tuwaamini viongozi wa Chama but let us be WATCHFUL.
 
Jamani give kamanda Millya a brake, huyu atapelekwa Simajiro hiyo haina mjadala anaimarisha CDM kwanza halafu 2015 anapewa Simanjiro kupambana na hasimu wake mkuu wa siku zote!
 
Umetoa wapi hizo taarifa?. kuna gazeti la leo limemnukuu Lema akifurahi kwa kumkaribisha Millya cdm. Tena amehaidi kuzunguka nae nchi nzima kumwaga sera za CDM.

Afanye hivyo tu ila wasijempatia wadhifa
 
Sasa tosha, mwacheni Milya apumzike na hayo mambo ya kugombea tena sasa hivi yanatokea wapi? kwani rufaa ya Lema imeshasikilizwa na ameshindwa? Je Millya ameshatangaza kuwa anagombea Arusha mjini. Isije ikawa ni kimhemhe cha vijana wa Nape baada ya Millya kufanya maamuzi magumu. Suala la kwamba alikuwa upande wa Lowasa kwangu sioni kama ni hoja kubwa sana, je nani anaweza kutaja CCM nani msafi kwenye makundi yao? Hata hao kina January makamba wanamakundi yao huko hivyo kwakuwa wengi Millya mnafahamu ebu anzeni kuupima mwenendo wake kuanzia sasa, na historia isiwafunge sana bali iwasaidie katika kuupata ukweli wa sasa.
 
Mamluki wa ccm ndani ya cdm mh! hii sasa hatari, kama EL hakukutana na Vasco Da Gama kwenye ile mitaa ya Lisbon basi undani wao waweza kuwa mpana sana zaidi ya tufikiriavyo. Hawa wawili wanaweza kuwa wanapanga mikakati ya kuiporomosha cdm kabla ya 2015, unajua ccm ni wahuni wasio na adabu miaka yao yote ya uongozi wamekuwa wakitawala kwa hila na uovu hawaoni taabu kuongopa, kuua, kupindisha haki ili tu wapate madaraka ya kufisadi raslimali za taifa bila kujali hali duni za watu wanyonge, hawana hata chembe ya ubinadamu, shetani anaweza kuwa na chembe kubwa ya huruma zaidi ya mafisadi wa ccm. Kama Millya kweli amekuja kwa jaribio hilo akiuungana na wale ambao misimamo yao ndani ya cdm tayari haieleweki sawasawa akina shibuda, zitto kabwe na wengine tusiowatambua basi kazi kabla ya 2015 itakuwa nzito, tusubiri matamko tatanishi kama ya nia ya kugombea uraisi, mtei amefirisika kimawazo, mbowe na ukabila nk nk nk nk kuongezeka. We never know labda january, nape, le mutuz @ dodoma city wapo mbioni kuongeza majeshi ya ccm ndani ya cdm. Hakika ccm na mashushushu (tiss) wake hawatakubali demokrasia ichukue mkondo wake na chama makini kinachobeba matumaini ya watanzania kichaguliwe kihalali na watanzania, The Road to 2015 is very very very rough, wapiganaji wa kweli fungeni mikanda!!!
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom