Hatumshangai balozi, Tunastaajabu ya Dr. Shein

simplemind

JF-Expert Member
Apr 10, 2009
16,418
9,206
Written by Zdaima // 07/01/2016 // Habari // Maoni 3

Katikati ya mkwamo wa kisiasa hapa Zanzibar tumeona mengi hasa mwiezi miwili ya mwisho wa mwaka 2015 baada ya Jecha salim Jecha kufanya kile alichokiita kuufuta Uchaguzi na matokeo yote.

Yanayoendelea hapa kwetu ni muendelezo wa kukosekana mwelekeo wa muda mrefu wa watawala wetu (CCM kama chama tawala).

Kuhusu hili la mkwamo maajabu yanaendelea ingawa hatustaajabu tena, tumeshazowea vitimbwi vya watawala hawa.
Unaweza kujiuliza uhuni uliofanywa wa kufuta MATOKEO KINYEMELA nchi ikaingia katika mzozo mkubwa, watawala wetu wakajitia hamnazo badala ya kuwawajibisha walioleta mzozo ndio kwanza ubabe wa kunyamazisha watu ukazidi na kujitia hamnazo. nchi ikageuka ya matamko kwa kupishana kila ngazi na kila mmoja kuwa msemaji. Masikini Zanzibar yetu.

Tumemuona balozi akiwa ndio kila kitu. Kajipa mamlaka ya makamo mwenyekiti wa CCM Zanzibar kwa kuzungumzia mazungumzo yanayoendelea ikulu yumkini amejifanya yeye ndie Rais na Mwenyekiti wa kikao licha ya dr Sjhein kuwaambia waandishi kuwa yeye ndie mwenyekiti?

Alijigeuza mwanasheria mkuu wa serikali kwa kutetea Serikali iliyokwisha muda wake kikatiba na kujifanya yeye ndio muamuzi na mtoa ufafanuzi wa mambo ya kisheria ya serikali.Kwani Mwanasheria yuko wapi?

Alijigeuza kuwa Tume ya Uchaguzi na kusema uchaguzi upo ilihali uwezo huo uko kwa tume pekee.

Alijigeuza kuwa kamishna wa bajeti wa SMZ kwa kutueleza bajeti ya uchaguzi wa marudio.

Tunastaajabu, yote haya yanafanyika mkuu wa nchi ya Zanzibar yupo na makamu wake hana kisisi chochote, hajali wala haterereki na anachotaka kusema. Yaani utafikiri yeye ndio rais sio?

Hii hali si ya kawaida na LAZIMA TUSEME kuna jambo linafichwa. Haiwezekani atokee Rais wa Zanzibar na mwenyekiti wa baraza la Mapinduzi, makamo Mwenyekiti wa chama, mwenyekiti wa kikao cha mazungumzo na mkuu wa vikosi vya SMZ aseme mazungumzo yanaenda vizuri na yakimaliza wananchi watajulishwa halafu atokee mtu anaitwa Balozi Seif Ali Idd aje awaambie wananchi kuwa uchaguzi upo ilihali mazungumzo yanaendelea na watu WANASUBIRI KAULI NA AHADI ya viongozi.

Inakuwaje hali hii? Lazima tumshangae dr Shein. Hivi wananchi wamuelewe vipi? kwamba makamo wake hamuheshimu? au Dr shein anawadanganya walimwengu maamuzi yao tayari? au kuna nini huko ndani kwa viongozi wa CCM. Napata mashaka isije kuwa anafanya haya akijuwa mamlaka haipo imekwisha tokea Dec 3 2015. Napata wasiwasi sana.
Source mzalendo net.
 
Back
Top Bottom