Hatukuwahi kujiandaa kubadilika

Pamputi

JF-Expert Member
Apr 22, 2016
982
723
Nadhani hatukuwahi kujiandaa kuyapokea mabadiliko na ndo asili ya kelele nyingi mitaani juu ya haya ayafanyayo rais wa jamhuri ya Tanzania Dr John Pombe Magufuli

Kwa miaka mingi sana watz tulikuaga tukipiga kelele juu ya habari na visa vya kifisadi ambavyo vililwishaanza kuota mizizi na tukatamani atokee mtu qa kufukua huo uozo,kufanya reformation ya mifumo lakini kumbe hatukuwahi kujiandaa kwa harufu kali za uozo huo mara utapoanza kufukuliwa

watz tuliaminishwa zaidi katika mabadiliko bila kuyaelewa vema hata mabadiliko tulokua tunayapigia kelele

FACT ni kwamba hakunaga mabadiliko yoyote duniani ambayo hayawezi kupitia changamoto, lakini bahati mbaya watz hawakuwahi kujiandaa na haya

Tulitaka mifumo mizuri ya ukusanyaji waapato,mifumo thabiti ya udhibiti wa mapato ,tukahitaji mifumo mizuri ya kiuchumi isiyo na mambo ya kiutegemzi,tukahitaji utawala bora na fact ni kwmba yote haya ndo yanafanyika tunayageuza maumivu kwa sababu hatukuwahi kujiandaa

Kwa waliosoma vzr sheria ukisoma Doctrine of Rule of Law vzr n kwamba sheria ikitiliwa maanani sana ndio udiktete yaani mtu anayefuata sheria na kuisimamia katika maamuz yake n rahisi kumuona ni dikteta na Kama taifa lina raisi mwenye hulka hzo ni rahisi kumhisi n dictator

Ubaya unakuja pale mnapokua na wapinzani ambao wao vision yao imelenga kwny kushka madaraka tu na sio kutumikia watu hapo inakua hatari zaidi

Rai yangu watz tuyapokee haya maana njia sahihi kuelekea kwny matarajio yetu japo tulichelewa kujiandaa

#GO_MAGU
 
unajua ndugu ni kweli umeongea baadhi ya mambo vizuri kabisa.

Lakini watanzania wanajiuliza, mapato ya serikali yana paa kila mwezi.

Mianya ya rushwa mingi imezibwa wananchi wanajiuliza tena wana hoja za msingi sana.

Mbona hiyo mipesa haiwafaidii? Wafanyakazi wa serikali hawa boreshewi Mishahara yao na kodi imeongezeka?
 
Mkuu mabadiliko yapi, vijana wetu kunyimwa mikopo?, ukosefu wa ajira?, na kama kuna nia njema kwa nini mnabinya haki ya habari na demokrasia
 
Sheria gani anafata yy budget hazifuatwi kama Bunge lilivyopitisha.Niambie kama kulikua na budget ya kununua ndege.afadhali asingefata budget Kweny Jambo ambalo linagusa watu wengi kama barabara hospital ama tren Maji unaweza kumwelewa.
 
Mkuu aya ya pili kutoka mwisho imepoteza mwelekeo wa hoja yako ambayo ulianza kuielezea vizuri. Huwezi kuvuka mto kabla ujaufikia. Unaionaje vision ya wapinzani ambao hawajashika madaraka ya urais kabla? Huyu aliyepo tayari ana mwaka na ni rahisi sasa kuona vision yake. Na watz wengi wao wameshaona tunakoelekea.

Halafu sio kweli kwamba kiongozi anayesimamia sheria huonekana kama dikteta. Hiyo ni dhana ya ajabu sana. Kwa nchi yetu rais anaapa kusimamia na kuilinda katiba(sheria) ya nchi. Ni ajabu kusema kwamba kiongozi anayesimamia sheria aliyoapa kuilinda aonekane dikteta. Kiongozi anaonekana dikteta pale anapoweka katiba aliyoapa kuilinda pembeni na kuongoza nchi kwa utashi wake, huyo ni dikteta tu, hana jina jingine.

Inawezekana kweli hatukujiandaa/ hatukuandaliwa kuyapokea mabadiliko kama kweli yapo. Nani wa kulaumiwa? Waluotutangazia mabadiliko, au sisi tuliokuwa tunashangilia neno mabadiliko bila kujua nini kinakwenda kubadilishwa!? Tuliulizwa tunataka mabadiliko ya aina gani zaidi ya pande zote mbili kudai zitaleta mabadiliko?
 
Hivi ukifanya mabadiliko kisha yakaongeza ugumu wa maisha yangu (Kwa mfano nilikuwa nanunua kilo ya sukari shs 1,800 kabla ya mabadiliko, na sasa baada ya kuanza mabadiliko nikawa nanunua kilo ya sukari shs 3,000), unatarajia bado nishangilie mabadiliko hayo??? Watu wengine akili yao ni matope plus plus...
 
Elimu bure na kuongezeka kwa bei ya korosho na Pamba ndio maana ya kutiririka pesa kwa wanyonge.

Ila Nyumbu hawatakaa waelewe hili.

Wako bize kupangusa viatu vya Lowasa
 
Pengine huko mbeleni Jamii Forums ianzishe mfuko wa kuchangia ili baadhi ya watu aina yako wakaoshe macho kwenye nchi zingine ili nati zenye kutu zilizofunga bongo zenu zilegee na zifunguke muanze kufikirika constructively.
Kwa akili zako hizo zilizofungwa unaweza kuelezea huo utiririkaji wa hela ulivyo kupitia elimu bure na bei mpya ya korosho?
Nina wasiwasi nyumbani kwako una doti kadhaa mpya za khanga za CCM ulizopewa mwaka jana kwenye kampeni.
Elimu bure na kuongezeka kwa bei ya korosho na Pamba ndio maana ya kutiririka pesa kwa wanyonge.

Ila Nyumbu hawatakaa waelewe hili.

Wako bize kupangusa viatu vya Lowasa
 
Kama 2020 watz watakusanyika na kusikiliza porojo za ccm kuna mawili either wamelaniwa kuwa watakuwa masikini maisha yao yote au watz wengi hawana akili kabisa yaani ni vichaa na utafiti ule wa watz wengi ni vichaa utasibitika.
 
Mkuu aya ya pili kutoka mwisho imepoteza mwelekeo wa hoja yako ambayo ulianza kuielezea vizuri. Huwezi kuvuka mto kabla ujaufikia. Unaionaje vision ya wapinzani ambao hawajashika madaraka ya urais kabla? Huyu aliyepo tayari ana mwaka na ni rahisi sasa kuona vision yake. Na watz wengi wao wameshaona tunakoelekea.

Halafu sio kweli kwamba kiongozi anayesimamia sheria huonekana kama dikteta. Hiyo ni dhana ya ajabu sana. Kwa nchi yetu rais anaapa kusimamia na kuilinda katiba(sheria) ya nchi. Ni ajabu kusema kwamba kiongozi anayesimamia sheria aliyoapa kuilinda aonekane dikteta. Kiongozi anaonekana dikteta pale anapoweka katiba aliyoapa kuilinda pembeni na kuongoza nchi kwa utashi wake, huyo ni dikteta tu, hana jina jingine.

Inawezekana kweli hatukujiandaa/ hatukuandaliwa kuyapokea mabadiliko kama kweli yapo. Nani wa kulaumiwa? Waluotutangazia mabadiliko, au sisi tuliokuwa tunashangilia neno mabadiliko bila kujua nini kinakwenda kubadilishwa!? Tuliulizwa tunataka mabadiliko ya aina gani zaidi ya pande zote mbili kudai zitaleta mabadiliko?
Kashikiwa akili huyu.,swali langu kwake ni moja tu.
Wakati watu wakiyalalamikia hayo aliyoyasema yeye hakuwa mmoja wa wale waliokuwa watetezi wa uozo huo?
Kama alikuwa team hiyo awezaje kutambua wakosoaji walilenga(walidhamiria)mabadiliko yepi???
 
Hivi ukifanya mabadiliko kisha yakaongeza ugumu wa maisha yangu (Kwa mfano nilikuwa nanunua kilo ya sukari shs 1,800 kabla ya mabadiliko, na sasa baada ya kuanza mabadiliko nikawa nanunua kilo ya sukari shs 3,000), unatarajia bado nishangilie mabadiliko hayo??? Watu wengine akili yao ni matope plus plus...
Kazi tunayo.,tukumbike tu kuna watu tunakumbana nao humu hawatembei,kusafiri(kuosha macho)hawasomi(majarida wala vitabu)hata kutembea dunia ukiwa umekaa hapohapo nyumbani(internet)kwenye mambo ya maana zaidi ya kuchungulia mambo yetu yale tuliyojaaliwa waafrica.
 
Kuna ka generation ka watanzania wanafiki, watu wa kulalamika lalamika tu, chochote watakachofanyiwa bado watatafuta kasoro tu, Magu hatakiwi kuwaendekeza watu wa sampuli hii, aendelee kukaza huku pesa ikienda kwenye miundombinu mikubwa, 2026 watakuwa wanamtukuza Magu huku wakimtukana Rais wa awamu ya sita.
 
Wewe ni mpumbavu ulizoezwa kuongezwa mshahara bira kuongeza ufanisi
Umepanic au? uongozi huu ni mbovu kama siyo sana ni zaidi na umempa sifa zaidi Kikwete na ameonekana kuwa kiongozi bora zaidi kuwahi kutokea TZ, na mimi nasema Kikwete ni rais wangu wa muda wote. Wakati wa Kikwete tulikuwa tumeiva bhana, no stress at all, leo vijana wadogo tunatembea na stress kibao za kazi na za familia zetu na tumekauka kama siyo kusinyaa na kama tukienda ivi uzee TZ utaanzia miaka 40 na life span ya mtanzania itashuka sana.
 
upandishiwe mshahara kwa kazi ipi unayofanya,kutwa upo JF
Ule utafiti wa kati ya watz 4 mmoja wao ni kichaa uko sahihi kabisa, yaani pamoja na ubovu wote wa serikali hii ambao ukiaanza kuuelezea kurasa 1000 hazitoshi bado kuna watu mnaona eti wanafanya kazi na wako sahihi bila shaka na wewe ni kichaa.
 
Back
Top Bottom