Elections 2015 Hatukai mita 200 kufanya vurugu Bali tunakaa mita mia mbili kuzuia

eden kimario

JF-Expert Member
Jun 13, 2015
10,227
16,178
Kwanza niseme hatuko tayari kuvunja sheria zilizowekwa japo wakubwa hawa jk NEC na police wamedhamiria kuzivunja sisi vijana tunasema tupo tayari kwa lolote ili mradi sheria za uchaguzi zinafuatwa na si vinginevyo./

Lengo kuu la kukaa mita 200

Ni kulinda mtu yoyote atakaeingia kituoni akiwa na makaratasi ya kura hatutamruhusu kuingia kwa namna yoyote ile tunataka zile za kituoni zibaki hizo hizo hatutaruhusu mtu gari baiskeli pikipiki ziingize chochote kituoni wakati wa zoezi la kupiga kura.

Ndio maana ya kulinda kura
Sio zile zinazopigwa ndani ya kituo
Bali zinazotoka nnje ya kituo
Kwenda kujazilishia
Wakala kazi yake ni ndani na
Sisi wananchi kazi yetu ni kuzuia zile za nnje zisiingie ndani ya kituo

Nasema nitasubiri mita 200 kwa ajili ya kazi hiyo
Hilo bao la mkono mnaloshirikiana na tume halipo
 
kazi ya wakala wa chama ktk chumba cha uchaguz ni nini ?

unajua madhara ya mkusanyiko ?.

majibu, + na akili zako.
 
Naona mnataka kututafutia sababu, mmeanza vitisho vya hapa na pale kwamba, kama tutakaa vituoni mtatuonesha nguvu ya Chama Dola, sasa sisi hatutishiki kwani sheria inaturuhusu na hatuna lengo la kuleta vurugu lengo letu ni kusubiri matokeo mpaka yatakapobandikwa vituoni.

youngsharo
 
Last edited by a moderator:
Wakuu tupige kura hapa, kuonesha kuwa, kura tutazilinda kwa kufuata sheria.

Hatutaogopa washawasha, wala risasi za moto, damu itakayomwagika itaendelea kuwalilia wamwagaji maana mtaimwaga pasipo haki, hamtawamaliza Watanzania, Wataendelea kuwepo.

Hii ni nchi yetu sote.

Bonyeza like kulaani na kupinga kauli za JK kukataza watu kulinda kura.
 
Ndio na mimi nashangaa, hivi hayo matokeo yanayobandikwa vituoni wanayabandikia majini ndio yasome!!? Kama ni mpiga kura basi ni lazima aruhusiwe kuyaangalia kwani wakala anakuwa ameshayaona tayari.
 
:WAMESHATUGEUZA MAZUZU:
Yaelekea waliloamua ni UBABE UBABE TU!
MOLA TUONDOSHE DUBWANA HILI IN MYSTEROUSLY LIMETUNGANGANA,LINATAKA KUFA NA SISI!
 
Wakuu tupige kura hapa, kuonesha kuwa, kura tutazilinda kwa kufuata sheria.

Hatutaogopa washawasha, wala risasi za moto, damu itakayomwagika itaendelea kuwalilia wamwagaji maana mtaimwaga pasipo haki, hamtawamaliza Watanzania, Wataendelea kuwepo.

Hii ni nchi yetu sote.

Bonyeza like kulaani na kupinga kauli za JK kukataza watu kulinda kura.

Umetumwa na nani kuzungumzia umwagaji damu?

Itabidi Lowassa na vishoka waenzake waongoze katika kulinda kura.

Mbowe na Lowassa watakuwa zao London wakati nyie mkipgana kwa ajili ya maslahi yao.

Tanzania kwanza, Lowassa baadaye.
 
The National Election Act Cap 343 ,section 4(1) inasema.hairuhusiwi kukusanyika ,kuvaa sare za Chama, ndani ya mita200, wakati zoezi la Uchaguzi linaendelea, kwa hiyo Sheria inaruhusu
 
Jk aelewe tanzania ya sasa sio ya miaka ya zamaini......hii ni inch yetu sote....hii inch sio inch ya familia ya Jk.
 
Hatukati tamaa kwenda kupiga kura nitapiga kura na nitailinda kwa amani.

Sheria gani inayokuruhusu na kukupa nguvu wewe kuwa mlinzi? Sheria ya uchaguzi haikupi hiyo kazi uliyojitungia.Kazi hiyo ya wakala wa chama chako.Wewe usije vunjwa miguu bure.MBOWE wala LOwasa hawawezi kuja kukuwekea dhamana wala kulisha familia yako
 
Naona mnataka kututafutia sababu, mmeanza vitisho vya hapa na pale kwamba, kama tutakaa vituoni mtatuonesha nguvu ya Chama Dola, sasa sisi hatutishiki kwani sheria inaturuhusu na hatuna lengo la kuleta vurugu lengo letu ni kusubiri matokeo mpaka yatakapobandikwa vituoni.

youngsharo

Nendeni tu njia ni nyeupe, ila mawakala msiwaweke sasa kwasababu nyie mkiwa nje tayari mtaweza kulinda mpaka ndani ...tunawatakia kila la heri.
 
Last edited by a moderator:
2 Reactions
Reply
Back
Top Bottom