Hatujachagua meya Arusha - CHADEMA | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Hatujachagua meya Arusha - CHADEMA

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by Rutashubanyuma, Jan 3, 2011.

 1. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #1
  Jan 3, 2011
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 159,018
  Likes Received: 420,655
  Trophy Points: 280
  Hatujachagua meya Arusha - CHADEMA


  na Halfani Lihundi, Arusha


  [​IMG] CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) mkoani Arusha kimekanusha kufanya mkutano wa kuchagua meya na kwamba hivi sasa halmashauri inatawaliwa na mameya wawili kutoka CHADEMA na CCM.
  Akizungumza na waandishi wa habari jana mjini hapa, Diwani wa Kata ya Kimandolu, Estomil Malla, ambaye ndiye aliyetajwa kuwa ndiye aliyechaguliwa kuwa meya kwa upande wa CHADEMA alisema taarifa hizo si za kweli na kwamba CHADEMA haijawahi kufanya uchaguzi kama huo.
  Malla alisema aliyetoa taarifa hizo ana lengo la kuipotosha jamii japo kuwa CHADEMA haimtambui meya aliyechaguliwa na CCM, lakini hawajafanya uchaguzi na hawatarajii kufanya, kwa kuwa wanajua kuwa uchaguzi wa kumchagua meya bado haujafanyika Arusha.
  Alisisitiza kuwa meya aliyechaguliwa na CCM si halali, kwani katika uchaguzi huo kuna kanuni za baraza la madiwani ambazo zimevunjwa na kubainisha kuwa CHADEMA inafuatilia suala hilo kisheria.
  “Wakati sisi tunafuatilia suala hili kisheria, hatuwezi kuvunja sheria, kwani kufanya hivyo ingekuwa kinyume cha taratibu, mimi sijui jambo hilo limetokea wapi, maana kila nikipita naona watu wanaiita meya huku wengine wakinishangilia, napenda kuwaambia wananchi wajue kuwa mimi si meya,” alisema Malla.
  Mbali na hayo, Malla alifafanua kuwa taratibu za kisheria wanazozifuata CHADEMA ni tofauti na mahakama, kwani njia za kisheria zipo nyingi si mahakama pekee.
   
 2. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #2
  Jan 3, 2011
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 159,018
  Likes Received: 420,655
  Trophy Points: 280
  Hizi habari zinajichanganya..........jana kwenye ITV huyu Estomih alinukuliwa akisema amejivua umeya wa Arusha............sasa tunasikia haya mengine............

  Pili kama hakuna uchaguzi wa umeya haujafanyika inakuwaje hata yeye Estomih alikuwa meya? Au anataka kusema alijipachika tu?

  Arusha inapaswa ifanye uchaguzi wa Umeya ambao utasimamiwa na NEC na wala siyo na watendaji wa manispaa ambao madiwani wanapaswa kuwasimamia...........................Where is NEC in all this?
   
 3. Michelle

  Michelle JF-Expert Member

  #3
  Jan 3, 2011
  Joined: Nov 16, 2010
  Messages: 7,364
  Likes Received: 196
  Trophy Points: 160
  Shida ya kuwa na wasemaji lukuki na media inayotumia hisia ndo hii.tunapata taarifa nyingi kila siku tunazidi kuchanganyikiwa.Mi nilijua situation ni kama Ivory kumbe ni kama Tanzania......lol
   
 4. Crashwise

  Crashwise JF-Expert Member

  #4
  Jan 3, 2011
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 22,172
  Likes Received: 862
  Trophy Points: 280
  Walikusudia kufanya uchanguzi siku moja baadaya uchanguzi ule uliofanywa na CCM lakini hawakufanya hivyo kwa ushauri wa watu mbalimbali kuwa kuwa wasi fanye makosa yanayofanywa na CCM hivyo chadema walikusudia kufungua kesi na kufanya mkutano ambao ungefatiwa na maandamano ambayo yalipangwa kufanyika tarehe 29-12-2010 lakini mkutano huo haukufanyika hivyo hata maandamano hayakufanyika…. baada ya uongozi wajuu kuzungumza na waziri mkuu Pinda kuwa watalifanyia kazi swala hilo mpaka kufikia tarehe 4-1-2011 na CDM wana weza kufanya mkutano wao tarehe 05-01-2011….
   
 5. N

  NasDaz JF-Expert Member

  #5
  Jan 4, 2011
  Joined: May 6, 2009
  Messages: 11,308
  Likes Received: 1,655
  Trophy Points: 280
  Nilishasahau ile methali ya mtaani kwetu isemayo ..."wewe ukisusa, wenzio.............!!"
   
 6. boma2000

  boma2000 JF-Expert Member

  #6
  Jan 4, 2011
  Joined: Oct 18, 2009
  Messages: 3,283
  Likes Received: 155
  Trophy Points: 160
  Hayo ni maneno ya Chadema tu, lakini vyama vingine vyote vinakubaliana na uchaguzi na deputy mayor ni wa TLP, Serikali tayari imekubaliana na matokeo maana haikuwa tayari kuona mayor pia anatoka upinzani
   
 7. tzjamani

  tzjamani JF-Expert Member

  #7
  Jan 5, 2011
  Joined: Oct 9, 2010
  Messages: 997
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Ruta unataka NEC wakafanye uchakachuzi mwingine? wako likizo baada ya kazi ngumu ya kumweka JK madarakani.
   
Loading...