singidadodoma
JF-Expert Member
- Nov 11, 2013
- 4,394
- 1,536
KATIKA matukio yasiyotarajiwa wala kutegemewa, baadhi ya watu wameanza kuhusisha suala la ulipaji wa kodi za serikali na masuala ya kisiasa, jambo ambalo si sahihi.
Dalili au chembechembe hizo mbaya zimejitokeza katika kipindi cha hivi karibuni, baada ya baadhi ya wanasiasa kudai kuwa kuna uonevu, vitisho na kuongezewa kodi kwa wafanyabiashara walioonekana kuunga mkono vyama vya upinzani.
Hata hivyo, tayari wanasiasa waliotoa madai hayo wamepata majibu yao kutoka kwenye mamlaka mbalimbali ambapo kwa ujumla wake wameshauriwa kuacha kuendeleza siasa za majukwaani na badala yake wamuache au wamuunge mkono Rais John Magufuli afanye kazi yake ya kuwabana wakwepa kodi.
Bila kuwataja wanasiasa waliotoa madai hayo, mahali walipotolea madai hayo wala kujua uhalali na ushahidi walionao katika hilo, sisi kama chombo cha mawasiliano kwa umma, wenye jukumu kubwa katika kuelimisha umma, msimamo wetu ni kuonya juu ya uingizaji wa siasa kwenye ulipaji wa kodi.
Tunasema hivyo kwa kuamini kuwa duniani kote, suala la ulipaji wa kodi ni suala la lazima na wananchi katika mataifa mbalimbali wanachukulia suala hilo kama utamaduni wao na wala si suala la kulazimishwa au kuhisi kuonewa au kutishwa.
Hakuna taifa lolote duniani linaloweza kujiendesha kwa mafanikio kama halitaweka misingi imara ya kusimamia ukusanyaji wa mapato kutoka kwa raia wake, wakiwemo wafanyabiashara wadogo, wa kati na wakubwa.
Kwa misingi hiyo suala la kodi huchukuliwa kuwa suala linalowaunganisha wananchi kuwa kitu kimoja na si kuwagawa kwa matabaka yoyote yale iwe ni dini, rangi au siasa.
Tunao uhakika kwamba hivi karibuni wakati Rais John Magufuli alipowakaribisha Ikulu wafanyabiashara na kuwasisitiza umuhimu wa kulipa kodi, alifanya hivyo bila kusukumwa na utashi au itikadi za kisiasa, bali alifanya hivyo kwa kufahamu kuwa ulipaji wa kodi ni suala la lazima kwa watu wote kwa maendeleo ya Taifa.
Wakati wapo wanasiasa kutoka upinzani wanaamini kuwa waliokuwa wanawaunga mkono ndio wanaoonewa na kutishwa, pia wapo wana CCM ambao nao wanalalamika kuwa waliokuwa wakiwaunga mkono na hata kuwachangia, hivi sasa wanaandamwa na serikali ili walipe kodi.
Hatua hii inadhihirisha wazi kuwa wapo watu wanaochanganya siasa na suala la ulipaji wa kodi, jambo ambalo halipaswi kuendelea kuachwa likaota mizizi.
Badala yake tuchukue nafasi hii kuwaomba wanasiasa wa vyama vyote kutumia nafasi wanazozipata wanapozungumza na jamii, kumuunga mkono Rais Magufuli katika juhudi zake za kuhakikisha kuwa anawabana wafanyabiashara wote ambao wamekuwa wakijihusisha na ukwepaji wa kodi kwa makusudi kutokana na nguvu au jeuri ya fedha waliyonayo.
Kwa miaka mingi Watanzania tumekuwa na kilio cha kuwa na bajeti ambayo kwa kiwango kikubwa inategemea fedha kutoka kwa wahisani, jambo ambalo limekuwa linachangia kushindwa kukamilika kwa mipango tuliyojiwekea, hivyo ili tuepukane na hilo ni lazima tuanze kuwaelimisha wananchi ili watambue umuhimu wa kuwa na utamaduni wa kulipa kodi kwa hiari kwa maendeleo ya taifa lao.