Hatuhitaji madawati kusema tuna elimu bora, hiyo pekee haitoshi. Tunahitaji mfumo wa elimu nzima ubadilike uendane na ulimwengu wa sasa

feyzal

JF-Expert Member
Apr 20, 2016
6,784
12,590
Wazee nitoe angalizo mimi sio mzuri wa kuandika ila naomba tupige kelele angalau watawala wasikie katika elimu yetu hii kuna shida mahala.

Wazee huyu baba(kuna video hapo chini) hapa anazungumza kitu ambacho binafsi nakubaliana nae kwa asilimia kubwa, vipi wewe mdau?

Serikali hebu itupie jicho elimu yetu maana sijaona ikiongelewa kabisa kwenye hata ilani ya chama tawala. Hatuhitaji madawati ndo tuseme tuna elimu bora hiyo haitoshi pekee, tunahitaji mfumo wa elimu nzima ubadilike uendane na ulimwengu hata kama itatuchukua muda lakini angalau tuanzie mahala na mwishowe tutakua sehemu nzuri.

Kwenye Kampeni angalau Mh Lissu aligusia mapana kwenye elimu yetu basi si vibaya serikali iliyopo ikaangalia zile nondo jinsi ya kuzitumia kwa faida ya Tanzania ya baadae vinginevyo tunazidi kutengeneza taifa la watu mbumbu na tusiojielewa.

Imefika hata mtu kuhoji haki yake ya msingi anaogopa kabisa kutokana na ujinga tuliojazwa,leo mtu anasema nachukua kadi au nasifia chama tawala nami nipate uteuzi ili tumbo lijae yote kutokana na matunda mabaya ya elimu yetu vijana tumekosa hata kujiamini.

Mdau toa maoni nini kifanyike,hapa tuweke uvyama kando.

 
Back
Top Bottom