Elections 2010 HATUDANGANYIKI kuwa kauli mbiu ya Waislamu kuelekea Uchaguzi Mkuu

Ninavyowajua hawa ndugu, wasije wakaanza kuchapana humo msikitini wenyewe kwa wenyewe kabla waraka haujaanza kutoka.

Nani kasema waislamu wana umoja?

ina maana wakati wanaahidiwa hawakujua kuwa ni kinyume na katiba??, HII AIBU HATA WAO KUISEMA!

Kazi ipo, elimu jamani!
 
Mi ni mkristo kamili kabisa.......ila hii kauli mbiu yao sioni kama ina ubaya kama ikichukuliwa ya kitaifa kuliko kidini zaidi........lkn kutakuwa tunabomoa kama tutaanza kuseme dini hii ndio ilileta uhuru......hii ndio ilileta hki na kile.

Ni kweli kabisa. Msimamo wa HATUDANGANYIKI utawafaa wananchi wote wa Tanzania bila kujali dini zao. Mimi nadhani tuchukue ule waraka wa wakatoliki tujumlishe na msimamo huu wa 'HATUDANGANYIKI', ninaamini hakuna fisadi atakayekatiza!
 
Mie nangoja waraka wao .
Kwa nini hawa ndugu zangu wao mifano yao yote ama mara nyingi huwa ni kwa wanawake tu ?
 
Hivi kuna haja ya viongozi hao kushindwa kwenda kuhudhuria futari?si kuna msemo usemao usikatae wito kataa neno? nini shida sasa?
 
Inakuaje ule waraka wa mwanzo ukaitwa wa Wakatoliki na huu wa sasa tunakimbilia kuuita wa Waislamu?.

Inamaana kuna asasi inayowaunganisha waislamu wote wa Tanzania imeubariki waraka huo ama ndio mazoea yaleyale ya kuwa wepesi kukimbilia, waislamu hivi, waislamu vile na tukija kwa wakristo tunaheshimu utafauti wao?

Shura ya Maimamu na Muungano wa Taasisi za Jumuiya za Kiislamu ni makundi tu ya waislamu na sio ndio waislamu. Na hivyo unapswa kutambulika kama waraka wa Shura ya Maimamu na Muungano wa Jumuiya za Kiisalamu na sio vinginevyo.

Kesho tutasikia waislamu wamefanya hivi mkiristo, waislamu wamemfranya vile mpagani, waislamu wamefanya haya....mambo ambayo tayari yamekuwa yakiendelea katika jamii yetu na tunaona ni ya kawaida.....

Ukivunja MISINGI uwe tayari MISINGI kukuvunja wewe....

omarilyas
 
Unasoma hapa kila siku bado hujaelewa kwa nini umeitwa waraka wa wakatoliki ? Duh pole sana
 
mimi nadhani hakuna ubaya kwa mtu kuweza kueleza alichonacho na hili ni kweli lipo maana hata vyombo mbali mbali vimeandika kuhusu waraka huo, tena hadi kwenye nguzo za simu wamebandika, kwa hiyo tusubiri huo uzinduzi ndiio tutajua kunani humo ndani. Kingunge alitabiri haya, nchi inapotea hii, mwishowe kila dini itasema ichague watu wa dhehebu lao, sio mwanzo wa machafuko huu kweli jamani? Na sidhani kama Nyerere angekuwepo angeyakubali haya yanayotokea sasa. mie yangu macho
 
Machafuko yamesha kuwepo sana na zaidi unasema waraka ulete machafuko ? CCM ndiyo walio leta machafuko na si waraka .Yes kila dhehebu watoe uwe kama wa wakatoliki kupinga ufedhuli wa CCM na siasa za kijinga , wizi wa mali za wana wa Tanzania na msije na hadithi za amani kutoweka .Watu wanakufa njaa , majongwa ya kijinga , hawana elimu, maji safi , ajira hakuna , huku CCM na vinara wake wanaongezeana mishahara na kubana haki za watanzania .CCM ndiyo kinara wa vurugu kwa kudhani buyu la pesa laweza kukaa mlangoni miaka 100 .Hakuna kitu cha hicho. Juzi kuna msomi Mbunge wa Msumbuji alisema neno juu ya CCM na huo ndio ukweli .
 
Kwa kuwa Waislamu nchini wamekuwa wakihadaiwa na kila kiongozi anayeingia madarakani masheikh wanataka kuhamasisha Waislamu nchi nzima kukataa katakata tabia ya kudanganywa kama watoto.

Embu waelimike leo basi. Toa kura yako kwa kiongozi atakayeleta maendeleo kwa jamii nzima, sio kiongozi atakayeleta maendeleo kwenye dini yako. Hii ni nchi ya wote, hivi hili ni gumu kuelewa?

Kesho wasabato wapige kura kumchagua kiongozi mwenye ahadi nzuri kwa wasabato, hivyo hivyo wakristu ... na wapagani nao si watafuata nyuma ... tunajenga au kubomoa nchi?

Hii ni tabia ya ubinafsi, na kama waislam wanataka viongozi waache tabia ya kuwahadaa, basi nao waache tabia ya kuchagua kiongozi atakayetimiza matakwa yao ... alafu tuone next time watahadaika na nini!
 
Kingunge alitabiri haya, nchi inapotea hii, mwishowe kila dini itasema ichague watu wa dhehebu lao,

THIS WILL NEVER HAPPEN!!
Pamoja na Watz kuitwa Wadanganyika na majina mwengine...Watz wameamka na hawawezi kuwa wajinga kiasi hiki... kiongozi mzuri anaweza kutoka dini/imani yoyote hata kama ni imani tofauti na ya yule anayepiga kura.Ninashangaa ni kwanini kuna watu wanapinga kitu kizuri kwa sababu tu kimetolewa na mu wa imani tofauti.Watanzania tuonyeshe ukomavu wa fikra na tuache woga usiokuwa na msingi!
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom